Muimbaji kutoka nchini Nigeria, Timaya ameweka wazi kuwa Alikiba ni miongoni mwa wasanii watakaoshiriki kwenye EP yake ambayo ipo mbioni kutoka.
EP hiyo ya Timaya inakwenda kwa jina la Chulo Vibe, kupitia ukurasa wake wa Instagram ndipo Timaya ameeleza hili.
“My Brother Alikiba from Tanzania came through on the EP Chulo Vibes,” ameeleza.
Ukiachana na hilo, pia kuna taarifa za Alikiba kutoa albamu kwa mwaka huu ingawa bado hilo halijathibitishwa.

Advertisements