Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Rayvanny ameishukuru Bodi ya Baraza la sanaa Taifa (BASATA) kwa kuwaruhusu kuendelea na show zao nje ya nchi licha ya kufungiwa.

Rayvanny na Diamond Platnumz walifungiwa na baraza hilo kufuatia kutumbuiza wimbo wao uitwao Mwanza licha ya wimbo huo kufungiwa. Hiki ni kile alichoandika Rayvanny kupitia ukurasa wake wa Instagram;

“Nichukue Nafasi Hii Kushukuru Basata, Hususani Bodi Ya Basata Kwa Kutupatia Ruhusa Ya Kufanya Matamasha Tulioyafanya Nchini Comoro , Nairobi Na Mombasa. Matamasha Tulitakiwa Tusiyafanye Kutokana Na Makosa Tuliyoyatenda Ila Kwa Upendo Wenu Mlituruhusu Kuyafanya.

“Nitoe Shukurani Zangu Za Dhati Kwenu Maana Bila Nyie Kutupa Ruhusa Ni Mengi Yangetukuta Vijana Wenu, Lakini Pamoja Na Yote Yaliotokea Kwetu Ni Kama Darasa La Kujua Wapi Tulipoteleza, Ili Mbeleni Lisijirudie Kosa Kama Tulilolifanya.

“Tuna Ahidi Kua Vijana Bora Na Mfano Kwa Jamii Hususani Katika Maadili Naamini Basata Na Bodi Ya Basata Mnatupenda Vijana Wenu Na Mnatamani Kuona Tunafika Mbali Katika Sanaa, Tunaomba Sana Hekima Zenu Katika Hili Vijana Wenu Tuendelee Kuchapa Kazi Kama Anavyosisitiza Mh. Rais Magufuli …… By Raymond Shaban / Rayvanny ”


Advertisements