Mkazi wa Igalula wilayani Uyui mkoani Tabora, Shaban Juma, ameigonga treni jana saa mbili asubuhi na kufariki dunia.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Emmanuel Nley ameeleza hayo leo Jumatatu Januari 7, 2019. Amesema tukio hilo limetokea jana saa 2 asubuhi na kwamba marehemu alikuwa akitembea kwa miguu kwenye njia ya treni na kuigonga.
Amebainisha kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hispitali ya Rufaa ya Mkoa Tabora, Kitete na kwamba uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.
Advertisements