Ndoa ya mastaa wawili bongo, Mwanamuziki Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ na Muigizaji Irene Uwoya inaonekana kuzidi kuchafuka zaidi kutokana na wanandoa hao kuweka maneno ya vijembe kwenye kurasa zao za kijamii huku zikitafsiriwa kwamba wanatupiana.

Usiku wa kuamkia leo katika ukurasa wa Instagram wa Msanii Dogo Janja, aliandika bora uonekane kwamba huna hela kuliko kutumia hela nyingi ili kuwaonyesha kwamba uko vizuri.
Katika muendelezo wa ujumbe wake, ‘hit maker’ wa Banana amerusha jiwe gizani kwa kutoa ushauri kwa mtu huyo anayedhaniwa kuwa ni mkewe, kwamba aache kuishi maisha ya kuigiza.
“Acha Kufake Fake Life. Its better to live your real life hujazaliwa kufrahisha kila mmoja, Komaaa” – Dogo Janja.

Mashambulio hayo ya gizani ya Dogo Janja yanatafsiriwa kwa haraka kuwa yanakwenda kwa muigizaji Uwoya kutokana na aina yake ya maisha anayoishi na kwamba inadaiwa ni msanii anayeishi maisha ghali sana tofauti na biashara ya sanaa ilivyo kwa sasa nchini.
Hata hivyo baada ya ujumbe huo wa Dogo Janja, Uwoya amerudisha mapigo yanayodhaniwa kwamba ni dongo kwa mume wake kwamba amegeuka mwimba taarabu.
“Kutoka kufanya hiphop mpaka taarab. ohhh shame” ameandika Uwoya.

Advertisements