Meneja wa mkali wa Bongo fleva, Rajabu Abdul Kahali maarufu kama Harmonize, Mr Puaz ameacha rasmi kazi ya umeneja kwa msanii huyo.

Akizungumza na Alasiri Online, Puaz amesema kuwa ameachana na mwanamuziki huyo kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri ya usimamizi.
“Ni kweli kwa sasa mimi na Harmonize hatufanyi kazi pamoja kwa sababu ya kupishana kauli, lakini haimaanishi mimi na WCB hatufanyi kazi au hatutafanya kazi,” amesema Puaz.
“WCB ni familia yangu ambayo ukaribu wangu na wao ulitokana na urafiki wangu na Diamond hivyo siwezi kuiacha, panapo kuwa na nafasi ya mimi kuhitajika kutoa mchango wangu nitaendelea kutoa kama mwanafamilia,” amesema Puaz.
Puaz akiwa anamsimamia mwanamuziki huyo alitoa nyimbo
kali kama vile Bado, Aiyola, Matatizo, Atarudi na Nishachoka.

==>>Msikilize hapo chini

Advertisements