Msanii wa muziki Bongo, Harmonize ameweka wazi ni kipindi gani hasa ataoa baada ya kuonekana kwa kipindi kirefu akiwa na mpenzi wake, Sarah.

Muimbaji huyo akizungumza na Wasafi TV kutokea nchini Kenya ameeleza kuwa ataoa ufikapo mwaka 2025.
“Hapana, muda mwingi tunahitaji kujirusha mimi na mpenzi wangu, kwa hiyo nafikiri kuoa ni 2025 ila tunahitaji hata kuwa na watoto wawili,” amesema Harmonize.
Kwa sasa Harmonize anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Paranawe ambao amemshirikisha muimbaji mwenzake kutokea WCB Rayvanny.
==>>Msikilize hapo chini

Advertisements