Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz amesema Wasafi Festival itafanya mambo makubwa Dar es Salaam.

Muimbaji huyo kutoka WCB ameeleza hayo baada ya tamasha hilo kumalizika nchini Kenya hapo juzi.

“Dar es Salaam Mwenyez Mungu akijaalia, Nawahidi kwa pamoja tutaandika Kumbukumbu ambayo itaiweka Bongo Fleva yetu kwenye kumbukumbu ya dunia,” ameandika Diamond Instagram.

Hadi sasa Wasafi Festival imepita kwenye mikoa ya Mtwara, Morogoro, Iringa, Mwanza, Sumbawanga na visiwani Zanzibar.

Advertisements