Jeshi la Polisi mkoani Tabora linamshikikia askari E.9301 Koplo Almas kwa tuhuma za kumuunguza kwa pasi mwanafunzi shule ya sekondari Cheyo, Jumanne Hussein (17).

Akizungumza leo Ijumaa Desemba 28, 2018 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ,Emmanuel Nley amesema tukio hilo limetokea Desemba 25, 2018.

Amesema mwanafunzi huyo alituhumiwa na Almas kuwa anataka kufanya mapenzi na binti yake.

Amebainisha kuwa baada ya askari huyo kumhisi mwanafunzi huyo alianza kumpiga na kumuunguza na pasi sehemu mbalimbali mwilini.

Kamanda Nley amesema tayari polisi imechukua hatua za kinidhamu kwa askari huyo ikiwa ni pamoja na kushtakiwa kijeshi na atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.

Advertisements