Mbunge wa Bunda Mjini (CHADEMA), Ester Bulaya ambaye pia ni Waziri Kivuli (Ofisi ya Waziri Mkuu) wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, amewataka Waziri Jenista na Mkurugenzi wa SSRA kujiuzulu, baada ya Rais Magufuli kuufuta mswada wa mabadiliko ya sheria ya utoaji mafao kwa kwa wastaafu.

Tayari uteuzi wa Mkurugenzi wa SSRA umeshatenguliwa na Rais Magufuli Usiku huu.
Bulaya amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa twitter ambapo amesema kuwa Waziri Mhagama na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) wajiuzulu kwa kuwa wameshindwa kuwatetea wafanyakazi.
“Mh Jenista, na Mkurugenzi wa SSRA, mjiuzulu nimewashinda, hamkuwatetea wafanyakazi”, ameandika Bulaya.
Advertisements