Mwanamuziki wa Injili nchini, Martha Mwaipaja amefunguka kuhusu tetesi za kuachana na mume wake, Mchungaji John Said baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa wawili hao wametengana.

Martha amesema kuwa, kila jambo atalizungumza kwa majira yake kwakuwa, muda ndio kila kitu na ukifika ataweka wazi kila kitu ili watu waelewe.

“Kila jambo na majira yake, suala la mimi kutalakiana na mume wangu ntaliweka wazi muda ukifika, kwasasa siko tayari”, amesema Mwaipaja.

Martha ameongeza kuwa kila mwanadamu anakutana na vitu tofauti tofauti katika maisha, na maandiko yanachukia talaka hivyo inategemea katika maisha ya ndoa unapitia kitu gani au aina gani ya maisha.

Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii, zilizagaa taarifa zilizodai kuwa mwanamuziki huyo wa Injili amemwagana na mumewe ambaye pia ni mchungaji.

Advertisements