Dada wa hiari wa msanii Diamond Platnumz, Halima Kimwana amesema kuwa muimbaji huyo kubadili wanawake kila mara ni kitu ambacho hakimsumbui.
Akizungumza na Wasafi TV amesema mwanaume kubali wanawake ni jambo la kawaida hivyo hawezi kuona ni kitu cha tofauti.
“Mimi mdogo wangu akibadilisha wanawake siwezi kukasirika kwa sababu mdogo wangu ni mwanaume na mwanaume anatakiwa abadilishe wanawake,” amesema.
“Mwanamke yeyote atakayekuja kwa mdogo wangu ni wifi yangu siwezi kumchagulia mwanamke,” amesema.
Muimbaji Diamond Platnumz ameshakuwa na mahusiano na warembo kadhaa maarufu kama Wema Sepetu, Penny, Zari The Bosslady na Hamisa Mobetto.
Advertisements