Mrembo Zari The Bosslady amezidi kutoa ushauri kwa wale wanaomfutialia kwenye mitandao ya kijamii.
Zari kwa sasa ameshauri kuwa hakuna ulazima wa kuendelea kuwa na watu ambao wanaondoa furaha yake kwenye mitandao ya kijamii.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;
“Sio lazima kunga’anga’nia mtu anaesumbua na kuondoa amani yako katika mitandao ya kijamii na hata maisha kwa ujumla futilia mbali watu kama hao.”-Zari
Zari The Bosslady ambaye anaishi Afrika Kusini na familia yake ni miongoni mwa warembo wenye ushawishi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii akiwa na followers zaidi ya Milioni 4 kwenye ukurasa wake Instagram.
Advertisements