Baada ya kuwasili nchini India kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa unaomsumbua, msanii wa Bongo Fleva, Hawa Mayoka ‘Hawa wa Nitarejea’, amefanyiwa vipimo na kubainika hana tatizo la ini bali ana tatizo la moyo ambalo limekuwa likifanya tumbo lake kujaa maji kila wakati.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Meneja wa Diamond Platnumz, Hamis Taletale ‘Babu Tale’, ambaye ndiye amempeleka Hawa nchini India ameandika:
“Asante Mungu tumefika salama India na tumefanya vipimo vyote upya salama na jibu lililotoka kwa wataalamu kwa asilimia 95% hawajaona tatizo linalohusiana na ini kwa mgonjwa ila ni moyo ndiyo uliyokuwa unapelekea mgonjwa kujaa maji mwilini.
“Hivyo basi kutahitajika kufanyika upasuaji mkubwa ambao utakuwa na uangalizi mkubwa wa wataalamu, then wametuhakikishia baada ya hapo mgonjwa atapata nafuu na inawezekana hizo 5% zilizobaki itakuqa poa na tatizo la ini halitokuwepo.
“Kikubwa tunaomba mtuombee dua na msiache kumuombea pia @diamondplatnumz apate nguvu ya kuendela kumsaidia kwa maana kutoa ni moyo. Kikubwa sana naomba tumuombee Hawa sababu anaingia kwenye upasuaji mkubwa na hii ni hatua ya yeye kuqa salama. Mungu tusimamie.”
Hivi karibuni Diamond alijitolea kumsaidia Hawa matibabu nchini India ambayo yatagharimu shilingi milioni 50 ikiwa ni baada ya kuugua kwa muda mrefu na kudaiwa kusumbuliwa na ugonjwa wa inim jambo ambalo imeonekana ni moyo.
Advertisements