Watoto wawili wa familia moja wakazi wa kijiji cha Tabaruka wilayani Sengerema wamefariki dunia wakati wakiogelea kwenye kisima kilichopo kijijini hapo.

 
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole amewataja watoto hao kuwa ni Given Aloyce (14) na Tekla Aloyce (12) waliokuwa wakisoma shule ya Msingi Tabaruka.
 
Kipole amesema tukio hilo limetokea Septemba 29, 2018  saa 11:00 jioni kijijini hapo walipokwenda kwenye kisima kufua sare za shule.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna amesema hajapata taarifa hizo lakini anafuatilia.
Advertisements