Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz amesema kuwa yupo kwenye mchakato wa kumpeleka Hawa kutibiwa India.
 
Hatua huyo imekuja baada ya hivi karibani mama mzazi wa Hawa kuweka wazi kuwa muimbaji yupo kwenye hali mbali kiafya.
 
“Niko namshughurikia now kwenda india kutibiwa, ila sikutaka kutangaza coz staki watu wachukulie msaada wangu ni kiki but kwakuwa maswali yamekuwa mengi juu yake, imebidi nijibu, na matibabu yake si chini ya milioni 50 na nitadeal nayo tu,” ameeleza Diamond kupitia mtandao wa Twitter.
 
Utakumbuka Diamond alimshirikiwa Hawa kwenye wimbo wake unaokwenda kwa jina la Nitarejea ambao ulifanya vizuri kabisa.

Advertisements