Kamati Kuu Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imempitisha Ramadhani Hamza  Chande kuwa mgombea wa uwakilishi wa Jang’ombe katika uchaguzi mdogo  utakaofanyika Oktoba 12.
Taarifa iliyotolewa  na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole imesema kamati hiyo chini ya Mwenyekiti Rais John Magufuli iliketi katika ofisi ndogo za chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam.
Katika taarifa hiyo, alisema CCM imerudia kuwaonya wanachama wake wanaokiuka Katiba na kanuni za uchaguzi kwa kuanza kufanya kampeni za chinichini za urais wa Zanzibar.
“CCM imetoa karipio la mwisho kwa wana CCM wanaokiuka Katiba, kanuni za uchaguzi, kanuni za uongozi na maadili kwa kuanza kufanya kampeni za kificho na za wazi za urais wa Zanzibar na kwenda kinyume na utamaduni na desturi njema za chama chetu ambazo kwa pamoja hutuongoza kuwapata viongozi wa CCM na Serikali zake,” imesema taarifa hiyo.
Advertisements