Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Nape Nnauye amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akilitumia aina ya Land Cruiser VX (nyeupe) lenye namba za usajili T349 DEL, kupata ajali na kupindukua asubuhi ya leo Septemba 24, 2018.

Nape amepata ajali hiyo wakati alipokuwa anaelekea wilayani Liwale kuungana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Taifa Dkt. Bashiru Ally anayezuru wilayani Liwale

Aidha, inadaiwa hakuna madhara makubwa yaliyotokea kwa waliokuwa ndani  ya gari ambapo kwa sasa Mbunge Nape amepatiwa usafiri mwingine ili kusudi aweze kuendelea na safari yake ya kuelekea wilayani Liwale.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema wameanza kuchunguza chanzo cha ajali hiyo licha ya kuwa eneo lililotokea ajali hakuna hitilafu ya aina yoyote

Advertisements