Mwanamitindo Hamisa Mobetto ameeleza sababu ya kum-block Diamond Platnumz kwenye ukurasa wa Instagram wa mwanae.
 
Kwenye Mahojiano na The Playlist ya Times FM, Hamissa amesema amefikia uamuzi huo kutokana na Diamond kumuingiza mtoto kwenye mambo yao na pia kushindwa kumuheshimu.
 
“Kwenye page ya mtoto sio kumfuta tu mpaka kum-block kwa sababu anakuwa kama mtu hajielewi, hata we have issues usimuingize mtoto ama mama mtoto wako,’ amesema.
 
“Unajua sisi kwetu wanasema jitahidi umsitiri mtu aliyekuzalisha, mtu uliyemzalia ama mke wako wa ndoa, mume wako wa ndoa kwa sababu aibu yake ni ni yako pia,” amesema Hamisa Mobetto.
 
Hamisa Motto ni mama wa watoto wawili, mmoja akiwa amezaa na Diamond Platnumz.
Advertisements