Diamond Platnumz amevunja ukimya kuhusu Zari The Bosslady kwa kumshukuru kuwa mama mzuri kwa watoto wake wawili.
Ujumbe huu unakuja mara baada ya takribani miezi nane tangu walivyoachana na kila mmoja kuendelea na maisha yake. Hiyo ni katika kumtakia Kheri ya siku yake ya kuzaliwa.
 
Diamond amemueleza Zari siku zote amekuwa akimuheshimu ndio maana hakuna siku amefanya interview kuzungumzia ni kitu gani kilitokea kati yao hadi kuachana. 
Kupitia ukurasa wake Instagram ameandika;
 
“A very special Birthday to the Mother of my Beloved kids…Thank you for blessing me with 2 amazing & cute Kids and thank you for continue being a good Mother to my Kids….Trust me, no matter how crazy & a proud man you think i might be, but am always grateful and i do respect you for that.
 
“That why, you’ve never heard or saw me on any interview talking anything about you….not even talking about my side point of what happened to us!!…coz the kids you blessed me with, means a lot to me…..and that is what made Love, respect and take you more than a blood sister / Brother for Life….May God bless you with long life, Happiness, and More Winning!!!”
 
Kauli ya Diamond unakuja ikiwa ni siku mmoja imepita tangu Hamisa Mobetto ambaye ni mzazi mwenzie na muimbaji huyu pia, kufanya Mahojiano na kipindi cha The Playlist cha Times FM na kueleza yote yalitokea kati yao hadi kuachana, ugomvi wa kifamilia na shutuma za kulogana.