Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kwa mara ya kwanza amejibu sakata la kuvaa cheni za miguuni almaarufu kama Kikuku ambapo amesema  kuwa kitendo hicho kinatafsiri mbali mbali kulingana na nchi husika.

 
Diamond kupitia Wasafi TV amesema kuwa kwa Marekani au nchini nyingine mtu kuvaa cheni mguuni anaonekana kama shujaa ambaye ametoroka jela.
“Kila nchi ina tamaduni zake na kila nchi ina tafsiri yake. Ukivaa cheni ya mguu kwa ambao wamekaa jela, ukiwa na kesi kubwa unafungwa cheni miguu yote miwli, kwa tafsiri yake ni mtu aliyefungwa jela halafu akatoroka,” Diamond ameiambia Wasafi TV.

“Lakini kwenye nchi nyingine unatafsiri vitu vingine, kwa hiyo anayetafsiri ndiye anakosea, anayekifanya hakosei. Naamini mtu hawezi kunipangia nivae kitu gani, atapoteza muda wake, kila mtu na fashion yake na haiwezi kukutafsiri wewe ni mtu wa namna gani,” amesisitiza zaidi.

Utakumbuka msanii mkongwe, Dudu Baya alijitokeza na kupinga vikali kitendo cha Diamond Platnumz kuvaa kikuku kwa kueleza kuwa muimbaji huyo anaharibu muziki wa Bongo Fleva.

Advertisements