Msanii wa muziki, Amber Lulu amedai wanaume wamemfanya aogope kuingia kwenye mahusiano ya mapenzi.
Muimbaji huyo wiki hii ameuambia mtandao wa Pro24Djs kwamba amepotezewa sana muda na wanaume ambao hawana msimamo katika mapenzi.
“Kama kutoka kimapenzi na mtu ambaye hajui thamani yako, ndio kitu ambacho huwa nakifikiria kwasababu nimepoteza sana muda,” alisema Amber Lulu.
“Huwaga hicho kitu kinaniumiza sana,  muda ambao nilikuwa naupoteza na nguvu ambazo ningeziweka kwenye muziki wangu ningefika mbali sana,”
Aliongeza, “Ndio maana watu wanasema ni bora mtu akupende kuliko umpende, kwa sababu ukimpenda inakuwa ni shida. Vitu kama hivyo vimenipelekea kufanya vitu vya ajabu, unakuwa na watu ambae haujawataka, inakuwa kama ni hasira kwahiyo imenifanya nisitamani kumuona mwanaume yeyote katika macho yangu,”
Advertisements