Msanii wa filamu Shamsa Ford ambaye ni mama wa mtoto mmoja, amedai vijana wengi wa Dar es salaam ni chawa, wambea na vibenten kwa kuwa walikosa elimu ambazo zingewawezesha kwenda kushindana kwenye soko la ajira.
Muigizaji huyo amedai mwanaume anatakiwa kuwa na misimamo na muonekano wa kiheshima katika jamii na sio kuonekana wakifanya mambo ya ajabu.
“Wanawake wenzangu tujitahidi sana kuwapa elimu ya kutosha watoto wetu wote haswa watoto wa kiume.
“Nimejikuta kuwa na huruma zaidi na watoto wa kiume kwasababu wa kwangu ni wa kiume. Huwa naumia sana nikiona mtoto wa kiume anavyohangaika kupata riziki,” aliandika Shamsa Ford kupitia Instagram yake.
Aliongeza, “Mtoto wa kiume asipokuwa na elimu ya kutosha au ujuzi wowote mwisho wao huwa ni mbaya kuliko watoto wa kike.
“Sasa hivi vijana wengi ambao hawana kazi au hawakubahatika kusoma ndo WAMBEA,WAPAMBE,VIBENTEN MARA CHAWAAA”
Muigizaji huyo ameongeza kwa kusema atahakikisha kwa upande wake anatimiza majuku yake ipasavyo ili mtoto wake asiingie kwenye makundi hayo.
““Kuwa mwanaume ni heshima kubwa sana kama ukisimama kwenye misingi ya kiume..Nitauza vitumbua, madira hata kufagia barabara ilimradi mwanangu apate elimu,” alisema Shamsa.
Advertisements