AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Nikabaki nikiwa nipo kimya, kama nimemwagiwa maji ya baridi, swali la kwanza kujiuliza kichwani ni mbinu gani waliyo itumi hadi mimi leo nipo hai.Nikiwa ninaendelea kuliwazia ninalo liwaza nikamuona Olvia Hitler akiwa amesimama nyuma ya Rahma huku macho yake yakimwagikwa na machozi ya damu
ENDELEA
Nikabaki nikiwa nimeduwaa, pasipo kuzungumza kitu chochote, Olvie akaanza kutingisha kichwa taratibu huku machozi ya damu yakiendelea kumwagika kwa wingi, akauinua mkono wake mmoja na kuanza kuniita taratibu, hapa ndipo nilipoiona mkono wake ukiwa umejaa damu nyingi.
“Walipo niambia kwamba umekufa, ikanilazimu kufanya kitu ambacho kingeurudisha uhai wako, kutokana sikuhitaji uweze kupotea kiurahisi maishani mwangu, wakati bado sijaisha nawe vya kutosha”
Hata Rahma alicho kizungumza sikukitilia maanani kwa maani macho, na akili yangu zote zilikuwa zipo kwa Olvia aliye simama nyuma ya mke wangu Rahma.Olvia Hitler akaunyanyua mkono wake wa pili juu na kuendelea kuniita kwa ishara kiasi kwamba nikazidi kuchanganyikiwa kwa vitendo vyake
“Niliamua kwenda, India kwa wanganga wanao tumia nguvu za kienyeji.Ambapo kuna mganga mmoja ambaye ni maarufu sana aliweza kunisaidia sana, hadi akaurudisha uhai wako”
Nikayahamishia macho kwa Raham, kisha nikayarudisha tena macho yangu kwa Olvia Hitler
“Mganga yule, alikupandikiza roho ya nyoka, na kila katikati ya mwaka na mwisho wa mwaka nilazima ugeuke kuwa…….”
Rahma alisita kidogo kuzungumza kitu anacho kizungumza na nikabaki nikiwa nimemtazama kwa umakini
“Utageukuwa kuwa nyoka mkubwa, na ninatakiwa kukupa watu wawili, uwale ili uweze kuongeza maisha ya kuishi la sivyo utakufa kabisa na nitakukosa mume wangu”
Rahma alizungumza huku akimwagikwa na machozi, nikaanza kujitazama kiungo kimoja baada ya kingine kwa maana sikuamini kama hapa mimi nilipo nimekuwa na pumzi ya nyoka.Olvia Hitler akapiga hatua moja nyuma kisha akasogea hatua nyingine moja kushoto, hapo ndipo nikamshuhudia utumbo wake ukiwa umechomoza nje, na ameushika na mkono mmoja ili usiguse chini
“Eddy”
Olvia Hitler aliniita pasipo Rahma kuisikia sauti yake kwani, Rahma hakutikisika wala kugeuka nyuma.
“Nisaidie, tafadhali”
Olvie Hitler alizungumza kwa shida, huku machozi ya damu yakizidi kumwagika kwa wigi.Nikasimama kwenye kiti na kuanza kupiga hatua za kuelekea alipa simama Olvia Hitler, huku Rahma akibaki akiduwaa
“Eddy unakwenda wapi?”
Sikujiu swali la Rahma zaidi ya kumuacha akinishangaa, kabla sijamfikia Olvia Hitler, Rahma akanyanyuka kwa haraka na kinishika mkono
“Eddy, unakwenda wapi?”
“Eheee”
Nilizungumza huku macho yangu yote nikiyaelekezea alipo simama Olvie Hitler
“Baby, niangalie mimi”
Rahma akanigeuza kichwa changu na nikiwa ninamtazama yeye, akanishika mashavuni kwa viganja vyake vilaini na taratibu akajivuta, karibu yake na kunibusu mashavuni
“Eddy mume wangu, nimefaya hivyo kwa sababu ninakupenda sana.Sikuweza kuishi peke yangu, kama ningeishi peke yangu naamini hadi sasa hivi ningekuwa marehemu”
Rahma aliendelea kuzungumza huku machozi yakimwagika, Olvier Hitler akapotea kwenye uwepo wa macho yangu
“Eddy forgive my husband, I did not mean to get you to be so bad you are, But all is because of love”(Eddy nisamehe mume wangu, sikuwa na maana mbaya ya kukufanya  wewe kuwa hivyo ulivyo, Ila yote ni kwasababu ninakupenda)
Rahma alizungumza huku akinikumbatia kwa nguvu, na kuuminya mwili wangu.Sikujua hata cha kumjibu zaidi ya mimi machozi kunimwagika, nikamnyanyua na kumbeba Rahma hadi chumbani kwetu.Tukapanda kitandani, kutokana na mawazo mengi kichwani mwangu sikuwa na hata hamu ya kumsogelea Rahma.Taratibu Rahma akanisogelea na kichwa chake kukilaza kifuani na sote tukapitiwa na usingizi mzito
                                                                                 ***
Siku zikazidi kwenda mbele huku nikiwa ninafurahia maisha yangu ya ndoa nikiwa na mke wangu Rahma, nikaanza kusahau hata yale mambo magumu ambayo niliyapitia.Siku ya mkutano kati yangu na waandishi wa habari ikawadia.Waandishi wa habari wapatao ishirini kutoka vyombo mbali mbali vya habari wakafika nyumbani kwangu huku wote wakiwa na furaha kubwa ya kuhitaji kuzungumza na mimi
Rahma akishirikiana na wafanyakazi watatu wa ndani, wakaandaa eneo zuri la kufanyia mahojiano katika bustani yetu ya maua, iliopo katika eneo la jumba letu la kifahari, Rahma akanitolea suti nzuri iliyo nipendeza na kuniomba nivae, huku akinisaidia kuweka weka sawa sehemu za kola ya shati langu jeupe pamoja na tai nzri aliyo ichangua
“Mume wangu umetoka chikopa”
“Wacha wee”
“Eheee, ila kuwa makini kuna waandishi wa habari wadada wazuri wamekuja hapo sema tuu ndio hivyo tena”
“Acha wivu mke wangu”
“Wivu lazima, tena sana”
“Haya baby, wangu vipi wewe huojiwi?”
“Hapana, mimi nitasimama nyuma ya kamera zao”
Tukatoka, huku tuomeongozana na Rahma na kuwakuta waandishi wa habari wakiwa wamekaa kwenye  viti wakinisubiria, huku kamera zao wakiwa wameziweka tayari za kuchukua kila tukio ambali litakalo tokea eneo hili
“Habari zenu”
Niliwasalimia, na wote wakaitikia kwa furaha.Nikakaa kwenye kiti changu ambapo mbele yake kuna meza ndogo ilio na maji pamoja na glasi, kisha na kuwatazama wote na wakatabasamu kwa mmoja mmoja
“Jamani karibuni, hapa ndio nyumbani kwangu na mpenzi wangu, mahabuba wangu, chocolate wangu, utamu wangu, pumzi yangu, ubavu wangu, chakula changu, mke wangu Rahma”
Maneno yote ya kumsifia mke wangu Rahma yakawafanya waandishi wa habari kupiga makofi kwa furaha
“Yaaa ninamependa sana mke wangu, na popote nikiwa nilazima nimtaje mke wangu kama mtu muhimu sana kwenye maisha yangu, japo hata wengine pia ni muhimu sana kwenye maisha yangu”
“Sasa ninakaribisha maswali”
Akanyoosha kidole muandishi wa habari mmoja na nikampa ruhusa akasimama huku akiwa ameshika kikaratasi kidogo mkononi mwake
“Kwa jina mimi ninaitwa Godwin ninatokea kituo cha habari ITV, kwanza ninashukuru sana bwana Eddy kwa kuweza kutujali na kutupa nafasi ya kuzungumza na sisi waandishi wa habari.Kwana ninapenda kutanguliza pole kwa yale yote ambayo yalikupata, pia hongera kwa kuweza kujitoea kwa hali na mali katika kukuokoa mji wako”
“Swali ambalo ninapenda kukuuliza, ni jinsi gani uliweza kupambana na jola kubwa ambalo kusema kweli lilikuwa ni tishio kubwa sana kwa mji pamoja na dunia hii,ASANTE”
Godwin akakaa kwenye kiti chake
“Kwana, asante kwa pole ulizo nipa, nimezipokea.Hata asante pia nimezipokea.Niende kwenye jibu lako, kitu ambacho kilinisaidia ni Mungu tuu kwa maana kwa uwezo wangu wa kibinadamu nisingeweza kufanya kitu cha aina yoyote mbele ya joka hilo”
“Lilikuwa linafananiaje”
Dada mmoja aliniuliza na kuwafanya wezake kumgeukia
“Linatisha na lilikuwa na vichwa kumi na mbili”
“Kabla ya hapa nyuma, ninasikikia ulikuwa unamiliki majini, kuna ukweli wowote katika hilo”
Jamaa mmoja aliniuliza, nikamtazama kwa muda kisha nikamjibu
“Ukweli huo upo, nikweli nilikuwa ninawamiliki majini ila ni kutokana na kurisithwa”
“Ulirisithwa na nani?”
“Nikizungumza watu wengi hamuta amini ila, ndio ukweli wenyewe.Nilirithishwa na mfalme Suleiman”
Waandishi wa habari wakatazama
“Ila mfalme huyo si alifariki kipindi kirefu cha karne za enzi hizo, kabla ya kristo?”
“Ndio, ila yeye mwenyewe alidai kwamba hajafariki, ila watu wengi walizani kwamba amekufa”
“Ulikutana naye wapi?”
“Kwenye moja ya handaki la msitu ambao hadi sasa hivi siujui jina lake”
“Pia niliwahi kusikia kwamba mke wako alibeba ujauzito na kujifungua kiumbe cha ajabu”
Swala lamuandishi huyu wa kiume likanifanya nimtazame Rahma ambaye baada ya macho yetu kuyakutanishwa kwa pamoja akayaiinamisha kichwa chake chini
“Hapana, hakuwahi kubeba ujauzito”
“Kwa habari ambazo zinaendelea huko mtaani, kwamba wewe ulisha kufa siku nyingi?”
“Nani kakuambia?”
Sikujibu swali zaidi ya kumuuliza huyu muandishi wa habari, kwani swali lake limeanza kunikera moyo wangu
“Hii nikutokana na wajibu wa madaktari walio kupokea na kukupima vipimo vyote na kusadikika kwamba wewe ulikuwa mfu”
Nikakaa kimya kama dakika mbili, nikikosa jibu la kujibu
“Bwana Eddy?”
Muandishi mmoja aliiniita na kunifanya ninyanyue sura yangu kumtazama
“Sio kweli, laiti kama ningekuwa mimi ni mfua sidhani kama leo mungekuwa munanihoji, ninahisi hao madaktari akili zao hazina akili”
“Je nasikia mke wako, alikuwa ni mwanafunzi wako?”
“Nani?”
“Rahma”
“Kwani kua ubaya?”
“Hapana”
“Basi ni ndio”
“Kutokana na kupendwa, sana na kujipatia umaarufu kwa wananchi wako wa mji wa Tanga, je unampango wa kugombania Ubunge kama wananchi wanavyo hitaji?”
“Siipendi siasa, na sidhani kama ninaweza kuwa mbunge”
“Je kuna ukweli wowote kwamba wewe umepandikizwa roho ya nyoka?”
Swali la muandishi huyu wa habari likanifanya niiname chini ya meza kwani nilijikuta nikikasirika sana jambo ambalo taratibu nikanza kuhisi mabadiliko kwenye mwili wangu, ubaridi mkali ukaanza kunitawala, huku ukiambatana na mikono yangu kuanza kubadilika jambo lililo anza kuniogopesha
                                                                                            ITAENDELEA
Advertisements