Msanii wa bongo movies Steve Nyerere ameonyesha kukerwa kwake na tabia ya baadhi ya wasanii kutumia miili yao kama kiki katika sanaa hasa kwa kukaa uchi jambo ambalo limekuwa likifanywa sana na wakina dada katika tasnia ya sanaa.

Steve Nyerere anasema kuwa haamini hata kidogo kama msanii mkubwa kama Irene Uwoya anaweza kutumia mwili wake kuweka wazi kwa ajili ya kupata kiki katika mtandao ilihali swala hili linadhalilisha sana hadhi yake  na watu wake wa karibu.
Katika ukurasa wake wa instagram , steve nyerere aliandika “Sitaki kuamini kuwa kiki inapatikana kwa kukaa uchi au ili uwe star  lazima ufanye kitu ambacho jamii na familia yako itakuona  wewe kama kituko na kitu cha ajabu basi wewe hapo ukajiona star , hapana hapo hata waliokuzunguka watakuona kituko.”
“Sifa ya msanii ni moja tu , msanii ni kioo cha jamii,kuburudisha na kuelimisha kupitia sanaa ama kipaji chake,  inapotokea mtu anafanya kinyume na katiba yetu huyo anatuchafua wote, hata wenye maadili wanaonekana walewale.”
Wikiend iliyopita, mwana dada Irene Uwoya aliweka picha katika ukurasa wake wa instagram na Kuacha watu mdomo wazi baada ya picha hiyo kumuonyesha akiwa mtupu na sehemu kubwa ya mwili wake ikiwa wazi ilhali heshima yake katika jamii ni tofauti na yale anayoyafanya.
Advertisements