Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa

 Ilipoishia
Nilimuuliza victoria baada ya yeye kushindwa kuzungumza kitu kinacho mfanya asimame nje ya mlango wetu, akaanza kuvunja vinja vidole vyake kwa aibu, akamtazama john, ambaye hakuwa amezungumza kitu cha aina yoyote, akamshika john shati lake, kisha akamvuta karibu yake na kumpiga busu la mdomo na kunifanya nibaki nikiwa ninamshangao

“I need you john”(john, ninakuhitaji)

Victoria alizungumza huku akimsukumia john ndani ya chumba, changu, kama simba mwenye njaa victoria akamsukumiza john kitandani na kuanza kumvua shati, lake, kwa aibu ikanilazimu mimi kutoka ndani ya chumba nikawaacha waendelee na mambo yao

Endelea
Nikaelekea moja kwa moja jikoni, nikachukua maji ya kunywa kwenye friji lililopo humu jikoni, kisha nikakaa kwenye kiti kirefu ambacho nacho kipo humu ndani ya chumba.Mawazo yakaanza kurudi upa juu ya mtu aliye mteka mke wangu na kumuua kinyama kwa kumlipua kwa bomu

“nilazima nilipize kisasi kwa yoyote aliye husika katika hili”

Nilijiapiza kimya kimya huku nikiyatazama maji yaliyopo kwenye glasi niliyo ishika mkononi mwangu, nikaitazama saa ya ukutani na kukuta ikionyesha ni saa sita kasoro dakika ishirini, usiku

“hawamalizi na sasa hivi”

Nilizungumza huku nikinyanyuka kwenye kiti na kutoka nje, na kuwakuta walinzi wakizunguka zunguka kaimarisha ulinzi wa jumba hili la baba yangu, sikutaka kuzungumza na mtu wa aina yoyote zaidi ya kubatazama mandhari mazuri yalipomo kwenye eneo hili

“hei”
Nilimuita mlinzi mmoja aliye kuwa anakatiza karibu yangu
“ndio bosi”
Kwa bahati nzuri mlinzi huyu alinijibu kwa kiswahili
“ninaweza pata usafiri muda huu”
“kivipi?”

“nina maanisha ninaweza kupata gari, lolote lenye funguo”
“unataka kwenda wapi usiku huu?”
“kuna sehemu ninahitaji kwenda”
“kwa hapo, ndugu siwezi kukusaidia kwani bosi hajatoa ruhusa ya mtu yoyote kutoka na usafiri, tena muda huu wa usiku”

“ahaa powa asante”

Nikaachana na mlinzi na kurudi ndani, nikafika hadi mlango wa kuingilia chumbani kwangu, nikaweka sikio la upande wa kulia, nikasikia miguno ya mahaba ikiwa inaendelea ndani ya chumba change.
“mmmm kazi kweli kweli”

Nikapata wazo la kwenda chumbani kwa victoria japo kuegesha kichwa change kidogo, hii ni kutokana na uchovu mwingi.Nikaingia na kuwasha taa, kitu cha kwanza nikakutana na mwanga wa simu ya victoria, ikionyesha ni muda mfupi kuna meseji au simu ilipigwa.Nikapiga hatua hadi kitandani ilipo, nikaichukua na kutazama, na kukuta missed call na namba ambayo haikuwa na jina lolote.Nikafungua kipochi chake kilicho kuwa pembezoni mwa simu, nikakuta noti kumi za dola mia mia

“yess, kazi yangu imeanza kukamilika”

Nikazichomoa noti hizo, na kuzidumbukiza kwenye mfuko wa jinzi langu, ambapo kuna simu ya john, aliyo nikabidhi muda wa mchana.

Nikatazama salio kwenye simu ya victoria nikakuta lipo lakutosha, nikaiweka mfukoni, nikafungua kabatini kwake na kukuta makoti mengi makubwa ya baridi.Nikachukua koti jeusi na kulivaa, nikachukua kofia ya kuzuia baridi na kuivaa, nikatoka nje ya chumba cha victoria.Kutokana ni mzoefu sana wa jumba hili la baba haikuwa, ngumu sana kwangu kutoroka pasipo walinzi kunioa, nikatoka nje ya ukuta wa jumba hili, kwa kuuruka, nikaanza kutembea kuelekea barabara kuu, kwa bahati nzuri nikapata taksi

“nipeleke kwenye uwanja wa ndege, wa ‘johannesburg’, itakuwa ni bei gani?”

“dola mia”

“sawa”

Kutokana nina kiasi cha kutosha cha pesa, sikuwa na haja ya kumbembeleza dereva huyu, japo ninatambua amenipiga kizinga, kutokana na ugeni wangu, tukatumia dakika ishirini kufika uwanja wa ndege.

“unaweza kunisubiri?”

“bili shaka”

Nikampa dereva taksi pesa yake, nikaelekea sehemu ya huduma kwa wateja, na kuwakuta dada kadhaa wakiwa wamejipanga wakizungumza na baadhi ya abiria waliopo kwenye eneo hili

“samahani dada”

“bila samahani, nikusaidie nini?”

“juzi usiku, kuamkia jana nilifika hapa na ndege ya shirika la nchini philipines, kuna kitu ninahitaji kukipata kwenye kwenye safari ile”

“kitu gani?”

Dada huyo alinijibu kwa umakini, huku akinitazama usoni

“nahitaji video zilizo rekodiwa kwenye safari nzima, kutoka philipines hadi hapa south africa”

“eheeeee, kaka yangu, mbona hiyo ni kazi kubwa sana, na kwakitengo changu, mimi siwezi kukusaidia”

“unaweza, nitakupa pesa yoyo……”

Mngurumo(vibration) wa simu ya vivtoria, ukaanza kutetemesha mfuko wangu, ikanilazimu kuitoa simu yake na kukuta meseji ikiwa imeingia, nikaifungua ila nikakutana na batani nyingi zikiniomba niiingize neno la siri ili niweze kuifungua meseji hiyo

“akhaaaa”

Nilijisemea mwenye baada ya kushindwa kuifungua meseji hiyo, nikamgeukia dada niliyo kuwa nikizungumza naye, nikakuta akimalizia kumnong’oneza rafiki yake, aliye kaa kiti cha pembeni yake

“niambie sasa dada, inawez……”

Akanikatisha mazungumzo yangu, kwa kunikonyeza kwa jicho lake kubwa kiasi, akanionyeshea ishara kwa macho nitazame juu yangu, nikakuta kameta ya ulinzi ikinirekodi

“nifwate”

Alizungumza kwa sauti ya chini, akajinyanyua kwenye kiti alicho kalia, akatoka kwenye chumba walichopo nikaanza kuongozana naye kuelekea anapo kwenda yeye, tukapandisha kwenye ngazi, sikujua ni wapi ananipeleka.Tukafika kwenye moja ya ukumbi wenye viti vingi, vya kupumzikia.Akatafuta sehemu iliyo tulia na kuniomba nikae

“eheee kaka ulikuwa unasemaje?”

Nikamuelezea nini ninacho kihitaji, akaniomba nimsubiri kama dakika kadhaa atarudi na kitu ambacho ninahitaji, ila akaniomba nimpatie malipo ya awali, na tulikubaliana nimpatie dola mia tano kwa kazi atakayo nifanyia.Nikaito simu ya john na kufungua upande wa picha, nikajikuta nikistuka baada ya kuzikuta picha za john na victoria wakiwa pamoja, kwenye fukwe za bahari, ila sikujua ni nchi gani.Nikazidi kwenda mbele na kukuta picha nyingi wakiwa pamoja, hapa ndipo nikagundua kuna mahusiano ya kimapenzi kati ya john na victori

“ahaaa, ndio maana nilivyo kuwa ninawatambulisha john alistuka, kumuona victori….”

Nilijisemea mimi mwenye, kimoyo moyo, huku nikiendelea kuzitazama picha walizo piga pamoja, nikaingia upande wa namba za simu na kuanza kuandika jina la victoria na kukuta likiwa limeandikwa ‘my wife v’, nikajaribu kuipiga namba, ikaingia kwenye simu ya victoria na kutokea jina la ‘baby john’

“wamejuana juana vipi?”

Ni moja ya swali lililo anza kuniumiza kichwa change, kabla sijajipatia jibu kichwani mwangu, muhudumu akarudi akiwa ameshika laptop ndogo mkononi mwake.

“chukua hii, nenda chooni, katazame kuna video nimeiiba ndani kwenye chumba cha mawasiliano”

“powa”

“fanya haraka mimi ninakusubiria hapa, nenda moja kwa moja kwenye ile kordo kunja kulia, utakuta vyoo”

Nikanyanyuka katika sehemu nilipo kaa, moja kwa moja nikaelekea katika sehemu alipo nielekeza muhudumu huyu, nikaingia kwenye choo cha wanaume, nikaifungua laptop aliyo nipa na kukuta faili moja lili andikwa video, nikalifungua

Nikaanza kuona mkanda wa video, katika ndege ya shirika la philipines, video hii imerekodiwa kwa kamera za ulinzi lilizipo kwenye ndege tulio kuja nayo, nikaanza kuona abiria wakiingia, ikiwemo mimi na phidaya.Ikanilazimu kuisimamisha video mara moja baada ya kumuona victoria akiingia ndani ya ndege hii, ila alikaa siti ya nyuma kabisa, pamoja na abiria mwengine.Katikati ya safari nikamuona john akiwa anazungumza mara kwa mara na victoria, pia nikaona jinsi john alivyokuwa akizungumza na mimi.Hadi ndege inafika, na sisi tunatoka kwenye ndege nikaumuona john akizungumza na victoria, wakakumbatiana kwa pamoja na kila mmoja akaondoka zake

Kwa kamera zilizopo nje ya uwanja wa ndege, nikamuona victoria akiingia kwenye moja ya gari jeusi na kuondoka huku, mimi na phidaya tukiwa tumekaa katika sehemu tuliyo kuwa tumekaa na kuondoka pamoja na john.Nikashusha pumzi nyingi, nikapata kumbukumbu za haraka kuhusiana na gari ambalo aliingia victoria kwani nililiona likiwa kwenye maegesho ya hoteli tuliyo kuwa tumefikizia.

Nikaifunga laptop, na katikti yake nikaweka noti tatu za dola mia mia, ili kukamilisha malipo ya dola mia tano, kutokana tayari nilisha mlipa dola mia mbili kama utangulizi wa kazi, nikarudi na kumkuta akiwa ananisubiri.Nikakaa kwenye kiti nilicho kuwa nimekalia, wakaingia askari wawili ndani ya ukumbi tuliopo, wakatutizama kwa umakini mimi na muhudumu na kuanza kupiga hatua za kuja sehemu tulipo kaa

Nikastukia kumuona muhudumu akinishika mashavu yangu, akaanzak kuinyonya midomo yangu, huku macho yake yakiwatazama askari wanao karibia kufika kwenye meza yetu

“mmgghhh”

Askari mmoja aliguna na kumfanya muhudumu huyo kuniachia taratibu, akatabasamu na kuwafanya askari hao watabasamu, akazungumza nao kizulu

“sizibuna ukuthi kungani muna?”(mbona munatabasamu?)
“sibona lapho nabasekweni”(tunaona upon na shemeji)
“yebo, nabasemzini zakho lokhu”(ndio shemeji yenu huyu)
“siyakubongela thina kudlule”(hongera sisi tunapita)
“esizayo efanayo”(sawa baadaye)
Askari wakaondoka na ku kutuacha sisi tukiwatazama
“haita jirudia tena”

Muhudumu alizungumza huhu akijifuta mdomo wake, kwa kitambaa

“pesa yako nimeibananisha katikati ya laptop, asante”

“sawa”

Nikanyanyuka na kuondoka, nikatoka nje ya uwanja wa ndege na kuingia katika taksi niliyo kuja nayo, nikamuomba dereva anipeleke ilipo hoteli tuliyo fikizia, njia nzima moyo wangu ukawa na maswali mengi kati ya john na victoria wamejuana vipi

“ahaaa, ila inaweza kuwa ni mambo ya kidunia”

Nilijisemea mwenyewe na kumfanya dereva taksi kunitazama, tukafika kwenye hoteli, tukasimama kwenye maegesho yamagari, nikashuka kwa bahati nzuri nikaliona gari alilo ondoka nalo victoria, nikapiga hatua hadi lilipo na kuchungulia kwenye dirisha, lake, sikukuta mtu ndani.Mlio wa mbwa na tochi za walinzi zikanistua, wakaniamuru nisimame kama nilivyo huku mikono yangu nikiinyoosha juu

Wakafika katika sehemu nilipo simama na kunza kunikagua, ila askari mmoja akastuka baada ya kuniona, akawanong’oneza wezake, ambao walikuwa wameninyooshea bunduki zao, wakazishusha chini

“samahani bwana bosi”

Askari huyo alizungumza huku akijaribu kutengeneza tabasamu la kinafki usoni mwake, huku akionekana kutahayari kwa kitendo walicho nifanyia

“hii gari ni yanani?”
“ahaa, hili gari ni la mkurugenzi victoria”
“yeye yupo wapi?”
“alikuja nalo juzi usiku, ila kutokana sikuingia mchana zamu sijajua aliondoka vipi”

Nikajaribu kuuvuta mlango wa gari upende wa dereva na likafunguka.Nikaufunga mlango nikaondoka na kuwaacha walinzi wakiulizana maswali kadhaa, nikafika kwenye chumba cha kurekodia video zote zinazo chukuliwa na kamera za ulinzi.Sikuamini macho yangu baada ya kuwakuta wafanya kazi wawili wa chumba hichi, wakiwa uchi wa mnyama, wakifanya mapenzi na msichana, anaye onekana ni kahaba                               

   *****sory madam*****(70)

Walipo niona wakastuka, na kila mmoja akasimama sehemu yake, huku msichana wanaye fanya naye mapenzi akiziwahi nguo zake zilizo kuwa juu ya meza, na kujifunika katika sehemu zake za siri.Nikawatizama jinsi wanavyo babaika, sikutaka kuwasemesha kitu cha aina yoyoye zaidi ya kwenda zilipo computer nyingi

“kuna video ninazihitaji”

“sawa sawa bosi”

Akawasha computer moja, nikamuelezea, video ninayo ihitaji ni ile ya siku nilipokuwa ninafika hapa hotelini, nikaanza kuyaona matukio yote tangu nikiwa ninaingia na phidaya sebleni, katika usiku ule nilimshuhudia john akizungumza na victoria katika sehemu ya vinywaji, baada ya mimi na mke wangu kuingia ndani ya chumba chetu cha kupumzikia.Nikawaona wakiingia kwenye moja ya chumba ambacho si kile john alicho kichukua

“mnamjua huyu?”

Nilimuonyesha john kwa kutumia kidole changu’’

“huyu ndio tunamjua, mara kwa mara huwa anakuja na mkurugenzi victoria”

Nikaona mwanamke mwengine akiingia ndani ya chumba alichokuwa john na victoria, huku akiwa amevaa baibui lililo mficha sura yake na kumbakisha macho tu

“huyo aliye ingia ni nani?”

Jamaa akairudisha nyuma video, hadi sehemu anayo ingia mwanamke huyo ambaye, ndiye aliye mteka na kumuua mke wangu.

“mlimuona kipindi akiingia ndani ya hicho chumba?”

“hapana bosi”

“iendeleze”

Jamaa akaiendeleza video, inayo onyesha watu wakiingia na kutoka kwenye vyumba vyao, kutokana  na camera hizo zimetengwa kwenye kordo ya hoteli hii.Baada ya muda nikamuona john akitoka ndani ya chumba hicho, akaondoka zake, baada ya dakika chache akatoka victoria na kuondoka, ila msichana huyo hakutoka hadi inatimu muda wa asubuhi ndipo naye akatoka, hapa ndipo nilipo ipata picha kamili kwamba kuna mchezo ambao ninachezewa na john pamoja na victoria.Nikajikuta nikiwa ninahasira dhidi ya john na victoria ambao wanaonekana wana siri kubwa sana waliyo ificha

“huyo msichana alikwenda wapi?”

Wakanionyesha video ambayo tuliiangalia muda baada ya mke wangu kutekwa na msichana huyo ambaye hadi sasa hivi sura yake sikuweza kuijua

“hembu nitolee hizo picha zake”

Jamaa akanitolea picha za msichana huyo aliye vaa baibui, kwa kutumia mashine ya ‘printing’ nikaikunja karatasi yenye picha ya msichana huyo na kuiweka mfukoni mwangu, nikatoka nje ya chumba na kurudi nilipo muacha dereva taksi, huku moyoni mwangu nikiwa ninahasira ya kwenda kutembeza kipigo kati ya john na victoria hadi waseme ukweli ni wapi alipo mke wangu.

“nirudishe kule tulipo anzia safari yetu”

Nilimuambia dereva taksi naye akatii, safari ikaanza kwa mwendo wa kawaida huku saa iliyopo kwenye simu ya john ikionyesha ni saa kumi na moja na dakika kumi, alfajiri.

“ongeza mwendo dereva tuwahi kufika”

Nilimuamrisha dereva taksi, akazidisha mwendo kasi wa gari kutoka spidi ya themanini hadi mia moja na thelathini, gafla nikastukia kumuona derava taksi akipiga kichwa kwenye mskani wa gari, huku akitoa mlio wa maumivu, makali, gari ikayumba na kutoka kwenye barabara, huku vitu vigumu vikipiga kwenye kioo cha mbele cha gari, na upande wa pembeni wa gari.

Kwa akili ya haraka nikagundua kwamba ni risasi zinazo piga kwenye gari letu, lilili poteza muelekezo na kusababisha lizunguke kutokana na miguu ya dereva kufunga breki za gafla na kuyazuia matairi yote kutembea.Nikabaki nikiinama chini, huku nikijitahidi kuushika mskani wa gari kuhakikisha gari haizidi kupoteza muelekeo.Risasi zisizo ni milio ya bunduki zikazidi kumiminika kwenye vioo vya gari tulilopo, sikujua hata zinatokea wapi.Chakumshukuru mungu, gari ikapiga kwenye mti mkubwa ulio pembezoni mwa barabara na kulisabaisha lisimame na kutulia.Mianga mikali ya taa za pikipiki nikaziona zikija kwa kasi kwenye sehemu gari lililopo

“nimepona…….?”

Nilizungumza huku nikijipapasa mwili mzima, sikujihisi maumivu yoyote kwenye mwili wangu, zaidi ya vioo vingi, vidogo vidogo vilivyo vunjwa kwa risasi, kuniangukia kwenye koti nililo livaa pamoja na suruali yangu, kwa haraka nikajirusha kwenye siti ya nyuma ya gari, jamaa wenye pikipiki wakazidi kulisogelea gari nililomo.Sikutaka kujua kwamba dereva taksi ni mzima au amekufa, nilicho kifanya ni kuufungua mlango wa nyuma upande ambao gari imepiga kwenye mti.Nikatambaa haraka hadi nyuma ya mti na kujibanza, huku nikihema sana.Nikachungulia nikawashuhudia majamaa kama sita wenye pikipiki kubwa, wakiwa wamevalia makoti, makubwa meusi, huku wakiwa na bunduki mikononi mwao zilizo fungwa viwambo vya kuzuia sauti

Wakasimama mita chache kutoka lilipo gari, na kuanza kulishambulia tena kwa risasi, na kuzidi kunipa woga mwingi.Dakika kama tano hivi zikakata kwa majamaa kulishambulia gari letu kwa risasi, nyingi, nikachungulia kidogo, nikamuo jamaa mmoja akipiga hatua za taratibu hadi ilipo gari na kuichungulia ndani, na kuonekana akistuka sana

“hayupo muhusika”

Alizungumza kwa sauti ya juu, huku akiwatazama wenzake, anaye onekena ni mkubwa wao akatoa simu, na kuminya minya na kuiweka sikioni, gafla simu ya victoria ikaanza kutetemeka mfukoni mwangu, kutokana kuweka mlio ulio katika mfumo wa mtetemeko(vibration).Nikaitoa kwa haraka mfukoni mwangu na kwabahati nzuri ikawa imesha jipokea kotokana na kuibabatiza kwenye mfuko wangu wakati ninaitoa kwa haraka mfukoni mwangu, kutokana ni ‘screan touch’ nikasikia sauti ikitoka kwenye simu iliyo pigwa ikizungumza kwa sauti ya juu kidogo

“bosi muhusika hatujampata”

Maneno hayo yanafanana na jamaa anaye piga simu hiyo, nikachungulia na kumuona jamaa akiishusha simu yake kutoka sikiooni mwake

“vipi”
“bosi azungumzi chochote”
“inakuwaje sasa?”
“hivi mnauhakika hii ndio taksi, tuliyokuwa tukiifwatilia aliyo ipanda huyo eddy?”
Mkubwa wao aliuliza
“ndio hii, hembu mpigie bosi, kwenye ile namba yake nyingine”

Jamaa mmoja alimshauri mwenzake na kuinyanyua tena simu yake na kuiweka sikioni, nikajikuta nikiitumbulia mimacho simu ya victoria nikisikilizia kuingia kwa simu hiyo.Ila haikuingia nikamsikia akizungumza

“bosi tumemkosa eddy”
“tumefwatilia, tumefanya shambulio la gafla ila hatujamuona”
“sawa, bosi”
Jamaa akakata simu na kuwatazama wezake
“oya jumbe, bosi anasemaje?”
“anasema tuhakikishe tunarudi na kichwa cha eddy, la sivyo atavikata vichwa vyetu”
“mmmm”

Jamaa mmoja akaguna, huku akishusha pumzi nyingi, mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio, hapa ndipo nikapata uhakika wa victoria ndio adui yangu namba moja na ndio yupo nyuma ya mpango mzima wa kumuua mke wangu akishirikiana na john, rafiki yangu wa karibu

“kama atakuwepo atakuwepo eneo, haya tumt……..”

Kabla ya mkuu wao, anaye itwa jumbe hajamalizia sentesi yake, sote tukastushwa na sauti ya simu ya john, iliyopo mfukoni mwangu.Nikasimama kwa haraka huku nikiwatazama jamaa, ambao nao wakanitazama huku akionekana kutokuamini macho yao, nisawasawa na mtu aliye okota embe dodo chini ya mti wa mpapai

“kamaataaaaaaa mshenzi yule”

Jumbe alizungumza huku akininyoosheaa kidole, kwa haraka nikaanza kukimbia nikieleka kwenye msitu huu, ambao ulikuwa na barabara tuliyo kuwa tunapita.Taa za pikipiki wanazo ziendesha jamaa, zikazidi kunifwata kwa nyuma kwa mwendo wa kasi, nikazidi kukimbia kuelekea nisipo pajua huku nikikatisha katisha kwenye miti, nikikwepa risasi nyingi zinazo kuja nyuma yangu

“eheee mungu wangu, nisadie mie”

Nilizungumza huku nikiendelea kukimbia, nikafanikiwa kupandisha kwenye kilima chenye mawe mengi makubwa ambayo si rahisi kwa pikipiki kupita, nikazidi kuongeza mwendo wa kukimbia, huku nikihema sana, nikazidi kupandisha mlima huku nikijitahidi kwa kadri yangu, kutafuta sehemu ambayo ninaweza kujibanza na kuwakwepa jamaa wana nitafuta

Nikafanikiwa kuingia kwenye moja ya mwamba wenye tobo kubwa, sikujali kama kunaweza kuwa na kutu cha hatari ndani ya mwamba huu, zaidi nilicho kijua mimi ni kujibanza huku, jasho jingi likinimwagika, kutokana na mwanga mzuri wa mbalamwezi nikawaona watu hao wakiendelea kutazama huku na huku na kuzidi kwenda mbele wakiamini kwamba nimekimbilia juu kabisa kwenye milima.Walipo potea kwenye macho yangu, nikaanza kurudi nyuma tulipo toka, safari hii nikijitahidi kufunga breki za miguu yangu, kuhakikisha sianguki kwani kasi niliyo nayo ya kushuka mlimani si ndogo, ikitokea bahati mbaya nikakosea kushuka nilazima kichwa kipige chini, hapo kuna mawili, kuvunjika vunjika mifupa au kufa kabisa

Simu ya john ikaanza kuita mfukoni mwangu, nikaitoa na kukuta jina la ‘my victoria’ huku pembeni kukiandikwa namba 2.Ikimaanisha ni namba ya pili kuwekwa kwenye simu hii, nikajibanza sehemu, yenye jiwe kubwa na kuitazama kwa muda, huku nikijaribu kuyalazimisha mate kupita kwenye koo langu lililo kauka kwa kiasi kikubwa, na taratibu nikaipokea na kuiweka sikioni

“hahahaaaa, eddy, rafiki yangu, si kila unaye muona kwako ni mwemaaaaa, wengine ni maadui.Kumbuka tanzania wewe ulijifanya ni mjanja kunionea na kunidhalilisha kwa kunipiga, sasa ni muda wako wakudhalilikaaa, ahahaaaaaaha”

Sauti ya john ilisikika huku, akizungumza kwa dharau na kucheka sana.Asira ikazidi kunipanda huku mwili mzima ukinitetemeka kwa hasira iliyo kali

“ohhhh kaka eddy, kumbuka mimi sio ndugu yako.Baba yako kwa nyege zake alimchukua mama yangu kutoka mikononi mwa baba yangu, kwa kutumia pesa zake, kisha wewe ukamtesa mama yangu na kumfanya afe, you’re a loser…………”(….., wewe ni mpotezaji)

Sauti ya victoria ilisikika huku wote wawili wakionekana kufurahia ushindi walio upata dhidi yangu

“wait bro eddy, ukirudi nyumbani utamkuta baba yako ni maiti, love you baby boy eddy, mwaaaaaaa”(subiri kaka eddy……., nakupenda eddy mtoto wa kiume,……)

Nikajihisi, mwili ukipasuka kwa hasira nikataka kupiga hatua moja mbele, ila kuna kitu kigumu kikanigusa kwenye kichwa changu upande wa kulia

“ohhhh lete simu yako”

Ni sauti nzito ya mmoja wa majambazi walio tumwa na victoria, kuja kuniangamiza.Taratibu akapita mbele yangu, huku bunduki yake akiwa ameielekeza kichwani kwangu

“utanaka simu eheeee”

Nilizungumza kwa kujiamini, huku nikimtazma kwa macho yaliyo anza kudondosha machozi ya asira pamoja na uchungu mwingi.Kwa haraka nikairusha simu juu, na kumfanya jambazi kuiangalia jinsi inavyo kwenda juu kwa kasi, nikaushika mkono wake wenye bastola, na kuvivunja vidole vyake vya mkono ulio shika bastola, akainama huku akitoa maumivu makali ya kuumia huku akilalamika.Nikampiga kigoti cha mso na kumfanya asimame, huku akiyumba yumba.Ngumi niliyo ikunja vizuri, ikatua kwenye shingo yake, ikampeleka chini, simu yake ya upepo aliyo kuwa ameishika na mkono mwengine ikaanguka chini huku sauti ya mkuu wake ikisisika

“g umepatwa na nini, eheeee”

Akanyanyuka na kutema mate pembeni yaliyo changanyikana na damu, ikiashiria kuna sehemu kwenye kinywa chake imepata itilafu.Akarusha teke, nikainama chini, na kujizungusha kwa haraka, nikaichota miguu yake na kumbwaga chini kama mzigo wa kuni.

Macho yangu yakatua kwenye bastola iliyo anguka karibu yangu, nikaiokota kwa haraka, jamaa akanishika mguu wa kulia na kuuvuta, ikapelekea mimi kuangukia mgongo na kuichia bastola ikasogea pembeni kidogo.Jamaa akaniwahi kunikalia tumboni, akaanza kunikaba koo kwanguvu nyingi kwa kutumia mkono wake ambao sijauvunja vidole, nikajitahidi kuminyana naye, huku mkono wangu mmoja nikiupeleka ilipo bastola, jamaa akazidi kuniminya koo langu, hadi nikajihisi kuanza kufanya mawasiliano na malaika mtoa roho

‘ukiwa mwanaume hutakiwi kukata tamaa kirahisi, pambana hadi dakika ya mwisho, hata kuua ikibidi fanya hivyo, ili tu uwe mshindi’

Nimaneno ya baba yangu mkubwa mzee godwin, kipindi alipokuwa akinifundisha mazoezi ya kupigana, nilipokuwa kijana wa umri mdogo sana, na maneno yake haya alikuwa akiniambia pale anaponizidi ikiwemo kunipoga kabala.Nikazidi kuupelekea mkono wangu sehemu yanye bastola, kidole change kimoja cha katikati, mkono wa kulia, kikaanza kuivuta taratibu bastola, hadi ikafika kwenye vidole vyangu vyote vitano vya mkono wa kulia.Sikuuliza zaidi ya kuvuta traiga, ya bastola mara sita na kuziruhusu risasi sita kutoka kwenye bastola, na kupenya kwenye mbavu za jambazi huyu, akaanguka pembeni yangu huku akivuta pumzi yake ya mwisho

Nikasimama na kumtizama jambazi huyu jinsi anavyo hangaika hangaika, nikafyatua risasi mbili, zikaingia kichwani mwake, akatulia tuli, nikaiokota simu ya john pamoja na simu ya upepo ya jambazi iliyo anguka

“upo wapi g wewe, tukufwate?”

Suti ya mkuu wao ambaye anaitwa jumbe, ilisikika vizuri kwenye spika za simu hii

“zamu yenu inafwata”

Nilizungumza kwa sauti nzito iliyo jaa mikwaruzo mingi, nikaipiga simu ya upepo kwenye jiwe kubwa, ikapelekea kuchanguka changuka vipande vingi.Nikakaanza kushuak kwenda chini, kwa bahati nzuri nikakuta sehemu walipo zisimamisha pikipiki zao, nikapanda kwenye moja ya pikipiki, nikaiendesha kwa kasi hadi umbali kidogo na zilipo nyingine, nikashuka na kurudi zilipo nyingine, nikaziangusha chini zote, nikazifungua mifuniko ya matanki ya mafuta, kisha nikarudi nilipo iacha pikipiki niliyo ichukua.Nikafyatua risasi mbili, zilipo pikipiki na kusabisha zilipuke zote

Nikaondoka kwa kasi, huku nikiotea otea njia ya kurudi barabarani, nikafanikiwa kutokeza kwenye barabara niliyo ifahamu, kwani ndio barabara kuu ya kurudi nyumbani kwa baba.Nikazidi konyeza mwendo kasi wa pikipiki, kimoyo moyo nikiapa kuwaua john na victoria kwa mkono wangu mimi mwenye.Hadi ninafika nyumbani kwa baba imesha timu saa kumi na mbili asubuhi

“nifungulieni geti nyinyi”

Niliwafokea walinzi wa getini, waliokuwa wakinihoji maswali, ikanilazimu kulivua kufia la pikipiki, ndipo wakanitambua ni mimi, wakafungau geti na kuingia ndani kwa kasi, walimzi wakabaki wakinishangaa, nikafika mlangoni na kuisimamisha pikipiki, kwa haraka nikashuka huku bastola yangu ikiwa mkononi, nikapandisha  ngazi kwa haraka nikielekea kwenye chumba change, nikaupiga teke mlango, ukafunguka, chumbani sikukuta mtu zaidi ya kitanda kilicho changuliwa mashuka.Nikaelekea chumba cha victoria, ila sikuwakuta.Nikaelekea chumba cha baba yangu, nikawakuta walinzi wake wawili wakiwa wamesimama mlangoni, ila mmoja akanizuia nisiingie

“mzee amepumzika, hadi muda wake wa kuamka ukifika ndio, unaruhusiwa kuingia”

“nini wewe”
“hiyo ni sheria na si ombi”
“unajua mimi ni nani?”
“hata kama, ila muda wa mzee kuamka ni sambili kamili kwa sasa jaturuhusu mtu kuingia ndani ya chumba hichi”

Nikamshika tai mlinzi anaye nisemesha upuuzi wake, nikamvuta na kumuangusha chini, mwenzake akataka kunishika ila kwa haraka nikaielekeza bastola yangu, kwenye pua yake, akabaki kimya akinitumbulia mimacho yake.Nikausukuma mlango wa chumba cha baba, nikamkuta akiwa anazunguka zunguka kwenye feni lililo juu, huku akiwa amefungwa kwa kamba ngumu, mdomoni mwake akiwa amefungwa kwa plasta kubwa, huku miguu na mikono yake ikiwa imefungwa kwa kamba.Nikabaki nikiwa nimeduwa, nikastukia walinzi nilio gombana nao mlangoni wakinipita kwa kasi na kukimbilia anapo ning’inia baba na kuanza kumshusha huku wakiwasiliana na wezao kuomba msaada.Machozi ya uchungu yakaanza kunimwagika, walinzi wakazidi kujazana chumbani kwa baba yangu, huku daktari wake akijitahidi kumpatia baba huduma ya kwanza

Nikamuona daktari akitingisha kichwa baada ya kuweka sikio lake kwenye, kifua cha baba, na kukuta mapigo yake ya moyo yakiwa yamesimama, ikiashiria kwamba ni marehemu tayari.Sikutaka hata kukisogelea kitanda cha baba, nikatoka ndani ya chumba, huku nikiwa nimefura kwa hasira kali.Sikujua hata walipo john na victori, na wao ndio wamesababisha mauji ya baba yangu.Simu ya john ikaita, na kukuta ni namba ngeni ndio inayo ita, nikaipokea haraka

“edddyyyyyyyyyy upo wapi kaka”

Sauti ya john ilisikika kwenye simu

“mshenzi, mpumbavu, nikikukamata nitakunyonga kama mulivyo fanya kwa baba yangu”

“hhaahahaaaaa kumbe umefika nyumbani….Ohhhhh boy, huwezi fanya chochote kwani hujui nilipo”

“kaka eddy, mwaya samahani kwa kumuua baba yako”

Sauti ya victoria ilisikika, alizungumza kwa dhara kubwa sana.Sikutaka kumjibu chochote, nikaikata simu, na kuingia kwenye mtandano wa goole, nika ‘download’, apps inayoitwa google map pamoja na ‘mobile location tracker’, inayo saidia kujua ni wapi namba ya simu iliyo pigwa inapatikana.Nikaiingiza namba ya simu iliyo nipigia, kitendo cha dakika moja nikafanikiwa kuletewa alama inayo onyesha ni wapi namba hiyo ya simu ipo na kuna umbali gani kutoka hadi sehemu nilipo.Nikatoka nje ya kupanda pikipiki yangu, na kuondoka kwa kasi, huku nikifwata jinsi simu inavyo nielekeza sehemu ninapoweza kuwapata john na victoria

Ndani ya nusu saa nikawa nimefika kwenye moja ya mtaa, wenye watu wengi wanao onekana ni wavuta bangi, na sehemu niliyo simama pembeni kuna kundi la vijana walio choka choka na maisha, huku mmoja akiwa aimeishika simu ambayo alitumia john kunipigia, nikashuka kwenye pikipiki kwa kujiamini sana hadi sehemu walipo simama.

Nikawasalimia ila hapakuwa na aliye ijibu salamu yangu, nikagusa bega aliye ishika simu akageuka, huku sura yake akiwa aimeikunja, akavuta fumba kubwa la msokoto wake wa bangi, kisha taratibu akaupulizia usoni mwangu, kitendo chake kikanipandisha hasira dhidi yake, nikampiga kidoti na sehemu za siri na kumfanya atoe ukelele, wezake wakataka kuingialia huku wakichomoa visu vyao, nikatoa bastola, nikawaelekezea moja baada ya mwengine akaanza kuondoka kwa kukimbia, akijaribu kuyaokoa maisha yake, nikabaki na mwenye simu

“nani kakupatia hii simu?”
“ehhheee?”

Nikamzaba kofi la shavu, hadi nikahisi na mimi maumivu makali kwenye kiganja change, kutokana nakutumia nguvu nyingi, jamba lililo sababisha vidole vyangu kujitokeza kwenye shavu la jamaa huyu

“ni dada mmoja hiviii”
Jamaa alizungumza huku akilia, kama mtoto mdogo
“huyo dada yupo wapi?”
“sijui mimi”

Nikaikoki bastola yangu, na kuisokomeza mdomomi mwake, macho yangu yaliyo jaa asira yakazidi kumtazama jamaa huyu, ambaye mwanzoni alijihisi ni mbabe sana

“na..Ongea….”
Nikaichomoa bastola yangu mdomoni, ili kumpa nafasi ya kuzungumza

“alimpa mtoto mmoja hivi, nikampokonya na kuichukua mimi”
Jamaa aliendelea kuzungumza huku akimwagikwa na machozi mengi
“unanidanganya….?”
“kweli, ila nawafahamu wale”
“wanapatikana wapi?”
“kuna godauni moja lipo hapo mbele, ndipo zilipo biashara zao”
“twende unipeleke”

Nikaiacha pikipiki, tukaanza kutembea kwa miguu kuelekea lilipo godauni analo lizungumzia jamaa, hapakuwa mbali sana, tukafika kwenye moja ya jengo kubwa lenye  geti kubwa

“simama na ugonge”

Jamaa akasimama na kuaza kugonga, mimi nikasimam pembeni kodogo, huku nikiwa nimejificha.Geti likaanza kufunguliwa kwenda juu, akachungulia mlinzi mmoja mwenye bunduki mkononi mwake, sikutaka kuuliza zaidi ya kufyatua risasi iliyo tua kichwani mwa mlizi huyo, jamaa niliye kuja naye akaanguka chini kwa presha, nikaingia ndani ya godauni hili, lenye maboksi mengi, walinzi waliopo humu ndani wakanza kunishambulia kwa risasi, zilizo nikosa kutokana na kujificha kwenye nguzo moja,

“stop fireee”

Niliisikia sauti ya victoria ikiwaamrisha watu wake kuacha kupiga risasi, nikashusha pumzi nyingi huku nikilishuhudia geti likishushwa chini na kufungwa

“eddy natambua kwamba ni wewe, hapo ulipo ninahesabu hadi tatu ninaomba ujitokeze”

Victoria alizungumza kwa sauti ya juu, niliyo isikia vizuri masikioni mwangu

“mojaaaaaaa,”

Nikashusha pumzi nyingi, huku nikichungulia kuona sehemu alipo, sikuamini macho yangu baada ya kumuona john akiwa amemshika phidaya, anaye lia, huku akiwa amemuwekea bastola ya kichwa

“mbiliiiiiiiiiii”
Nikamtazama mke wangu aliye pauka sana uso wake, nikamtazama tumboni mwake na kukuta tumbo lake lipo vilevile, ikiashiria bado ni mjamzito

“ta……….”

Nikajitokeza kwenye nguzo niliyo jificha, walinzi kama hamsini, bunduki zao zote zikawa zimeelekea kwangu, nikaanza kutembea kuelekea katika sehemu walipo simama john, phidaya na victori, huku bastola yangu ikiwa mkononi mwangu

“eddy mume wangu”

Phidaya akataka kunifwata, ila john akamshika nywele zake na kumvuta kwa nyuma, hadi akatoa ukelele akijaribu kuzishika nywele zake, john akaachia tabasamu pana usoni mwake, taratibu akianza kulishika tumbo la mke wangu.

“eddy, umepata mke nzuri sana”

Victoria alizungumza kwa sauti ya dharau, john akamkumbatia phidaya kwa nyuma, kitendo kilicho anza kunikasirisha, mikono ya john ikashuka taratibu hadi kwenye sehemu za siri za phidaya, akaanza kumlazimisha kulifunua dera(gauni) lake, ili aizishike sehemu za siri za phidaya, sikuvumilia kitendo cha john kumfanyia mke wangu unyama kama huo, nikaminya traiga ya bastola yangu, kwa bahati mbaya nikakuta bastola imeisha risasi, nikastukia nikipiga goti moja chini, huku damu zikianza kuvuja kwenye paja la mguu wangu wa kulia ulio pigwa risasi na john, aliye onekana kukasirishwa na kitendo change cha kujaribu kumuua

“baby usimuue sasa hivi, bado hukumu yake”

Victoria alizungumza huku akimtazama john aliye fura kwa hasira  nyingi, akitaka animalizie kunipiga risasi nyingine.Geti likafunguliwa, yakaingia magari manne aina ya bmw, zinazo fanana rangi, ambayo ni nyeusi yakasimama nyuma yangu, wakashuka wanaume nane walio valia suti nyeusi pamoja na miwani, maumivu ya mguu yakazidi kuniandama, huku kilio cha mke wangu, kikizidi kuniumiza.

Akashuka mwanamke mmoja aliye valia suti yeusi, pamoja na kofia kubwa nyeusi, huku macho yake akiwa ameyafunika na miwani yeusi, nywele zake ndefu, zikiwa zimeufunika uso wake, akanipita na kusimama sehemu alipo simama victoria, wakakumbatiana kwa furaha, kisha akaelekea sehemu alipo simama john, akamkumbatia huku wakizungumza chini chini.

Akageuka nyuma na kunitazama mimi, taratibu akavua miwani yake, akafwatia kofia lake kubwa, taratibu nywele zake akazisogeza pembeni, nikabaki nikistuka baada ya macho yangu kutazamana na macho ya madam mery.Mwalimu aliyekuwa mpenzi wangu kipindi ninasoma

”mambo eddy”

Alinisalimia huku akitabasamu, akpiga hatua za taratibu na kusimama mbele yangu, taratibu akachuchumaa, kidole chake kimoja akakiweka chini ya kidevu changu, kisha akazilete lipsi zangu karibu, akihitaji kunibusu, nikausogeza mdomo wangu pembeni, ila akanishika kwa nguvu na kuninyonya midomo yangu kwa kutumia nguvu, jambo lilizidi kumliza phidaya mke wangu, madam mery akaniachia na kusimama

“mmmmmm ladha yako ya mate, imezidi kuwa tamu, baby wangu.Au huyu mwanamke wako wa kiarabu ameiongezea?”

Alizungumza kwa dharau, akamfwata phidaya, nikastukia kumuona phidaya akimzaba kofi la shavu madam mery, huku akisindikiza kofi hilo kwa mate yaliyo tua usoni mwa madama mery, aliye anza kuchecheka kwa dharau.Madam mery akampiga ngwala phidaya, na kumfanya aangukie mgongo, na kutoa ukelele mkali wa maumivu, mguu mmoja wa madam mery ukatua kifuani kwa phidaya, madam mery akanyoosha mkono, wake wa kulia akiomba kitu.Mlinzi wake mmoja akampa bastola, iliyo tengenezwa kwa dhahabu tupu.Akaikoki tayari kwa kumfyatulia mke wangu risasi

“mery tafadhali ninakuomba usimuue mke wangu”

Nilizungumza huku machozi yakinimwagika kwa uchungu mwingi, phidaya akawa na kazi ya kulia huku akimuomba mungu wake, amlaze mahali pema peponi

“please sorry madam, don’t kill my wife…..Kama mtu wa kumuua ni mimi na si yeye”(tafadali bibie, ninakuomba usimuue mke wangu………)

Niliendelea kuzungumza huku machozi yakinimwagika kwa wingi usoni mwangu, madam mery akanitazama kwa macho makili kisha akmachia phidaya, na kurudi nilipo simama mimi.

“eddy, mimi ni mwanamke katili sana, ulikuwa hujui ni jinsi gani ninavyo mpenda derick, ulimuua kinyama sana.Ulimkatakata kama kuku, na kumbanika.Wewe ni binadamu wa aina gani eheee? Unajua ni uchungu gani nilio upata juu ya kifo cha mume wangu wa ndoa derick”

Madam mery alizungumza kwa uchungu mwingi, huku aknitazama kwa macho makali sana, akanipiga teke la kifua, lililo niangusha chini, kwakutumia kitu chake chenye ncha kali ya kisigino, akanikanyaga kwenye jeraha langu na kuzidi kunipa maumivu pamoja na uchungu.Madam mery akamngong’oneza victoria, ambaye naye alimuuta mtu wake mmoja aliye ondoka katika eneo hili.

“eddy nilikupenda ila siwezi kukuacha mzima hata kidogo”

Madam mery aliendelea kuzungumza huku mara kadha akiniminya kwenye jeraha langu la risasi, meza kubwa ikaletwa na watu wa vitoria, wakaninyanyua na kuniweka juu ya meza hiyo, wakanifunga kamba kwene kila mkono na ziichanua, huku watu wawili wakiwa wanazivuta kamba hizo, kila mmoja upande wake.Wengine wawili wakaifunga miguu yangu na kila mmoja akaivuta upande wake.

Jamaa mmojaa akamkabidhi madama mery upanga wenye kumeremeta kwa rangi yake, madama mery akapiga hatua hadi kwenye meza niliyo lazwa mimi, akanitazama kwa macho ya dharau

“nafanya hii, kwa ajili yakulipiza kisasi cha mume wangu”

“ngoja kwanza, nipo tayari kufa, ila ninakuomba usimuue mke wangu”

Nilizungumza kwa ujasiri, nikiwa nipo tayari kwa kufa, madam mery akalinyanyua panga lake juu, akalishusha kwa kasi kwenye mkono wangu wa kulia

  Itaendelea…
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia mbukuzihuru.com