Msanii Nay wa Mitego ametoa neno katika ngoma mpya ya Diamond Platnumz ya ‘Iyena’ ambapo amesema hata angetupa ngoma hiyo barabarani inge – hit tu.
Nay amesema kuwa licha ya kwamba ngoma hiyo ni kali, lakini yupo na mzazi mwenzie mwenye nyota na mafanikio, Zari The Bass Lady. Amemtaka Diamond aache kupuyanga na wachafua nyota.
“Mzee Mwenzangu Diamond platnumz Hii Ngoma Iyena Ata Ungeenda Kuacha Tu Barabarani Ukajifanya Kama Umeitupa Inge Hit Tu. Licha Ya Kwamba Ngoma Kali Pia Upo Na Mkeo Original Mama Tee Mwenye Nyota Ya Hela Na Mafanikio. Sasa Wewe Endelea Kupuyanga Na Hao Mapugi Machafua Nyota. Nitaongea Na Mama Tee Yaishe Tu.Haya Fanya Muende YouTube,” ameandika Nay wa Mitego kupitia mtandao wake wa Instagram.
Advertisements