Diamond Platnumz bado amezid kukamata headline mitandaoni kuhusu maisha yake ya kimahusiano, safari hii Harmonize naye katia neno katika hayo yanayoendelea.
Harmonize amesema hawezi kumshauri Diamond Platnumz awe na nani kwa sasa kati ya Zari, Hamisa au Wema ila ataonesha ushirikiano kwa yeyote akayechaguliwa na Diamond.
“Mimi yeyote; akiniambia leo tunarudi South Africa mimi nipo pale Pictorial, akiambia kwa wakati huu tuhamie Ununio, nipo pale kwa Madam, akiambia official tunachukua Hamisa tunaweka ndani nipo, sasa jamani kwani utamu napata mimi,” Harmonize ameiambia Wasafi TV.
Awali Harmonize alisema kuwa licha ya kufanya kazi na Diamond kwa ukaribu na kusaidiana katika mambo mbali mbali ni vigumu kwa yeye kumshauri kuhusu mahusiano yake ila watu wa karibu kutoka kwenye familia yake kama Romy Jons na Esma Platnumz wanaweza kufanya hivyo.
Advertisements