Video vixen alijizolea umaarufu Kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuanika picha za utupu siku za nyuma Sasha Kassim ameibuka tena na kukiri kuwa ataendelea kuweka picha zake za utupu mitandaoni.
Mwezi uliopita Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza alitangaza vita na wasichana wote ambao wanaanika picha zao za utupu mitandaoni na kuahidi kuwafungia kazi zao za sanaa endapo wataanika picha hizo.
Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu hatimaye Sasha Kassim amefunguka kuwa ataendelea kupiga picha za nusu uchi.
Kwenye mahojiano na Gazeti la Amani, Sasha alisema kuwa anajiandaa kupiga picha nyingine ambazo kama ni nguo za ndani zitaonekana nadhifu na zenye kuvutia na pia zitapungua ‘ukali’.
“Nilipotea kwa sababu niliibiwa akaunti yangu ya Instagram, si unajua ilikuwa na picha nyingi sana ila sasa hivi najiandaa kupiga picha nyingine mpya zitakuwa zikinionyesha sehemu zangu za mwili lakini zitakuwa zenye kujistiri kidogo”.
Advertisements