Muigizaji wa Bongo movie Sabby Angel ameibuka na kumtolea povu zito Staa wa Muziki wa Bongo fleva Ali Kiba baada ya kauli tata aliyoitoa kuhusu warembo wa Bongo.
Sabby Angel ambaye alishawahi kukiri kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Ali Kiba siku za nyuma kidogo ameshindwa kuvumilia na kumpa ukweli Staa Huyo aliyeoa hivi karibuni.
Hivi karibuni Kwenye mahojiano aliyofanya na Clouds Fm, Ali Kiba alifunguka kuwa sababu ya yeye kuwaacha warembo wote wa Bongo na kwenda kuoa Kenya ni kwa sababu wasichana wengi wakibongo wanaendekeza vigodoro na wengi sio wasomi.
Sabby Angel ameonekana kukasirishwa na kauli hiyo kutoka kwa mpenzi wake wa zamani na ameandika ujumbe huu:
“Ni jambo la Kheri kwa Ali K kuoa lakini sijapenda comment yake eti kusema eti Tanzania hakuna wanawake wasomi wa kuoa.
“Binafsi kama mtu umeamua kuoa we oa tu kwa manufaa yako lakini sio kukashifu wanawake wote. Kwani hapo wakati anatoka na hao wanawake wa Kitanzania haukuona hayo mapungufu? Kwani watu wanaoa vyeti? Wanaoa kukimu mahitaji yao binafsi na kuzaana?.
“Hiyo ni kumaanisha hata wazazi wetu wa kike na hata mama yake ni wale wale it is very immature”.
Ali Kiba alifunga ndoa na binti kutoka Mombasa Kenya wiki chache zilizopita.
Advertisements