Mwanamuziki wa Bongo fleva na video vixen maarufu Gifty Stanford maarufu kama Gigy Money amebahatika kupata dili nono la kuwa balozi wa Kondomu.

Baada ya Amber Lulu kutangaza wiki iliyopita kuwa amekuwa balozi rasmi wa Kondomu hatimaye na Gigy Mahoney amekuwa msanii wa pili kupata dili hilo.

Gigy Money alitangaza habari njema hiyo Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliandika:

“BALOZI WA BULL CONDOM (Jamani sahivi kwichi kwichi zangu zote natumia Kondomu mpaka Myrah akue)”.

Kwa upande wa gigy Money Dili hili limekuja katika wakati muafaka kabisa kwa sababu ndio kwanza amaetoka kujifungua hivyo ni wakati wake wa kusaka pesa.

Advertisements