Mwanadada muigizaji na mchekeshaji maarufu nchini Ebitoke amefunguka kwa hasira na kusema kuwa hataki kumsikia Ben Pol katika masikio yake kwa sababu Ben pol amekuwa hatokei katika baadhi ya matukio yake muhimu pamoja na kwamba anakuwa amempa mwaliko wa sehemu hizo.

Akiongea usiku wa kutambulisha trailer ya filamu yao mpya ya Sema , Ebitoke amesema kuwa pamoja na kwamba yeye na ben wamekuwa pamoja na bado hawajaachana lakini anashangaa kwanini Ben pol hajatokea katika uzinduzi huo.
“Yaan hapa tunaongelea Sema, habari za Ben Pol calm down kwanza,nilimpa kadi kabisa na ninaona hajafika sijui ni sababu gani na nimempigia simu hajapokea… kwaio sitaki kumsikia kabsia Ben pol hapa sasa hivi.Mimi na Ben pol hatuwezi kuwa basi bado tuko pamoja na tuna slay a king na queen lakini kwa sasa tuongele movies tu.”
Wiki chache zilizopita mwanadada huyo alipofanya interview na waandishi wa habari alisema kuwa amechoshwa na mambo ya Ben Pol hivyo anaona bora kuachana nae lakini wikiend hii anaongea tena na kusema kuna muda wanakwazana na kufikia hatua ya kuwa na hasira hata kuona bora waachane lakini bado anamuitaji sana Ben pol.
Advertisements