Siku mbili hizi kuna stori zilienea Kwenye mitandao ya kijamii zilizosema kuwa Msanii wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize amempachika mimba mwanadada ambaye ni msanii wa nyimbo za Injili kutoka Kenya.
Msanii huyo anayejulikana kama Veronica Wanja ‘Nicah The Queen’ amekataa tuhuma hizo na kudai kuwa hazina ukweli wowote, awali Nicah alikuwa katika mahusiano na mchekeshaji Dr. Ofweneke’s.
Tetesi hizi zimekuja mara baada ya wasanii hawa kuonekana pamoja mara kwa mara hali iliyozua minong’ono.
Kwenye Interview aliyofanya na gazeti moja nchini humo Veronica alisisitiza kuwa yeye sio mjamzito na hapendi kuongelea sana hayo mambo kwa sababu yeye ni Msanii wa injili hivyo si vema kuongelea.

Advertisements