Mchekeshaji maarufu kutoka Timamu Tv, Ebitoke ameibuka na kumtolea povu zito Shilole huku akidai kuwa hamuelewi kama ni msanii au mama ntiliye maana hajui kazi yake hata moja.
Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv, Shabiki mmoja alimtaka ataje wimbo mmoja wa Shilole na kuuimba ndipo aliposema hajui wimbo wake hata mmoja kwani hajui kama ni msanii au ni mama ntiliye:
“Labda unitajie nyimbo zake mimi sijui kazi zake mimi najuaga yeye ni mpishi tu ila hapa Kwenye nyimbo mtanisamehe kwa kweli sizijui nyimbo zake…..Nisiwe muongo naongea ukweli wala sio kiki kama mlivyozoea mambo ya kiki siku hizi nimeacha”.
Shilole mbali ya kuwa msanii wa Bongo fleva Lakini pia ni mfanyabiashara ambaye anamiliki mgahawa wake unaoitwa Shishi Food ambapo anauza vyakula mbali mbali.
Advertisements