Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amefunguka mazito kwa mumewe staa wa Bongo fleva Dogo Janja ambapo amedai kuwa ni moyo wake na kukiri kuwashangaa watu wanaosema yeye ni mdogo.
Ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya ilishangaza watu wengi ilipofungwa mwaka jana mpaka hivi sasa kuna watu ambao hawaamini kuwa wawili hao wameoana.
Na imekuwa ngumu kwa watu wengi kuzoea Mahusiano hayo hasa kwa sababu tofauti kubwa iliyopo baina yao kuanzia umri mpaka vitu vingine ambavyo vinaonekana baina yao.
Lakini kadri siku zinavyozidi kuenda wapendanao hao wameendelea kuuthibitishia uma wa Watanzania kuwa wanapendana na watazidi kuwa pamoja.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Uwoya kamfungukia mazito mumewe Dogo Janja ambapo amekiri kuwa anampenda mumewe na kusema anawashangaa watu ambao wanekazana kumsema ni mdogo kwani yeye anamuona mtu mwenye akili sana:
“Nakupenda sana sijawahi kukutana na mwanaume mwenye akili kama wewe na muelewa kama wewe….mdogo lakini mmmnh mimi ndio ninajua ndio maana wakiongea nawaangalia tu nasema iiiiii Dogo Janja wewe ndiye moyo wangu”.
Dogo Janja naye anaonekana amekolea na penzi la Irene kwani mara kwa mara anamposti mkewe na kumwagia sifa lukuki kama mke mwema na mwaminifu na kadhalika.
Advertisements