Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Rayc amewatolea povu zito watu wote ambao waliowahi kumsema kuhusu ubonge wake siku za nyuma.
Rayc ni moja kati ya wasanii wa kike ambao miaka kama kumi iliyopita enzi za ustaa wake alikuwa anavutia sana hadi kufikia hatua ya kuitwa kiuno bila mfupa.
Lakini alinenepa sana miaka ya hivi karibuni baada ya kuacha kutumia madawa ya kulevya kupelekea watu kumkejeli alipokuwa anashindwa kukata mauno kama zamani kutokana na mwili mkubwa.
Lakini saivi Rayc amepunguza kilo nyingi tu na kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka picha yake inayomuonyesha akiwa mwembamba kupita kiasi ambapo ameweka picha hiyo na kusindika kwa maneno haya: Wale wote walionikejeli nilivyonenepa mat.. yenu!”.
Advertisements