Mwanamuziki wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amemjibu msanii mwenzake Amber Lulu ambaye wiki iliyopita alisema Ommy hana muonekano wa kiume.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Jonijoo wiki iliyopita Amber aliulizwa kati ya Jux na Ommy Dimpoz ni mwanaume yupi ambaye anaweza akawa naye kimapenzi na moja kwa moja Amber Lulu alisema Jux kwa sababu Ommy hana muonekano wa kiume
“Jux sawa, Dimpoz hajakaa kama mwanaume, Ommy Dimpoz hawezi kukaa au kushindana na Jux ni zero, hana mvuto wowote , hamna chochote kinachonivutia kutoka kwake”.
Baada ya video clip hiyo kutrend sana ambayo ilikuwa inamuonyesha Amber akiongea hayo Ommy Dimpoz alijibu tuhuma hizo za Amber Lulu kuwa hana mvuto na hana muonekano wa kiume ambapo ameweka nyeusi kwa kusema hataki kumuongelea mtu huyo (Amber Lulu).
Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5 Ommy Dimpoz alifunguka maneno haya:
“Mimi sijui chochote na sijui hizo stori zimetoka wapi na zimeanzia wapi lakini kikubwa sisi kama wasanii unajua kila siku vitu ambavyo vinatuzunguka ni mambo ya mitandao, kwa hiyo in short no comment”.
Advertisements