MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA

ILIPOISHIA
. Taratibu akapiga hatua za uwoga, akaingia, ndani, mtoto huyo akaufunga mlango huo ulio kaa kama ukuta.
“Umepajuaje huku?”
“Babu yangu ndio alinionyesha huku”
“Babu yako”
“Ndio.”
“Kwanza unaitwa nani?”
“Naitwa Soroo”
Walizidi kushuka chini, wakakuta kordo moja ndefu iliyo jaa taa pembeni kwa juu,  mbele yake kwa mbali kuna mlango wa kuingilia kwenye chumba kimoja tu kilichopo kwenye eneo hilo. Wakazidi kupiga hatua, wakiwa umbali fulani kutoka kilipo chumba hicho, taa zikaanza kufifia. Wote wakajikuta wakiogopa, gafla taa zote zikazima na kujikuta wakipiga kelele za woga kwani giza zito lilitanda kwenye mboni za macho yao.
ENDELEA
   Haikupita hata dakika moja taa hizo zikawaka, wote wakanyamaza na kushusha pumzi zao. Kila mmoja woga ulimtawala.
“Turudi zetu”
Phidaya alizungumza huku akimshika mkono Soroo, habari ya kwenda alipo Black Shadow, ikayayuka moyoni mwake, hakutamani kuona anafia kwenye sehemu hiyo chini kabisa ya ardhi. Wakaanza kutembea kwenye kordo kurudi walipo tokea tena safari hii waliongeza hata mwendo wa kutembea. Kila mara Phidaya alitazama nyuma kuona kama kuna kitu kinakuja. Wakazipandisha ngazi kwa haraka, Soroo akafungua mlango, wakapita na kutokezea katika choo walicho ingia.
Wakarudishia kila kitu sehemu yake, na kutoka kwenye mabweni hayo. Moja kwa moja wakarudi katika sehemu ya mkusanyiko walipo watoto wengine pamoja na walezi wao.
“Mumefanikiwa kuona kitanda chake?”
Mlezi mmoja alimuuliza, huku akiachia tabasamu pana usoni mwake.
“Ndio, nimefurahi sana kuona mabweni yao. Nitahalkikisha kwamba tunaongeza mabweni ili mumweze kuchukua vijana wengi wamaoishi kwenye maisha magumu”
“Tutashukuru sana madam”
“Nipo pamoja nanyi. Naona muda wangu hautoshi basi ngoja niwaache muendelee na majukumu”
Phidaya alijikaza kuzungumza hivyo, ila mwili mzima alihisi kama umekufa ganzi kwa woga. Phidaya akamuaga Saroo, na kumuahidi atarejea kisha akangia kwenye gari lake na kuelekea hotelini wanap ishi Shamsa na mwenzake. Wakawakuta wakiwa wanafanya mazoezi ya viungo. Wakasalimiana kwa furaha, huku Phidaya akimbusu Shamsa kwenye paji la uso.
“Vipi mbona mupo kwenye mazoezi makali?”
“Kuna kitu mama nahitaji uweze kunisaidia”
“Kitu gani hicho?”
“Nihitaji kutafuta ukweli kuhusiana na kitu ambacho kilikupata wewe kwa maana inavyo onekana hukumbuki mambo ya nyuma”
Shamsa alizungumza huku akimtazama Phidaya usoni, anaye onekana kumsikiliza kwa umakini sana.
“Nahitaji kufahamu maeneo ambayo dokta Ranjiti anapenda kuyatembelea?”
“Kwa sasa yupo Korea Kusini”
“Mama hujanielewa swali langu, yaani sihitaji kujua yupo wapi ila nahitaji kufahamu maeneo anayo penda kwenda kutulia”
“Kusema kweli sifahamu, huwa Ranjiti muda mwingi anapenda kuutumia akiwa hospitalini, na hata akitoka ni sehemu chache sana ambazo anakwenda na kurejea”
“Au labda Yan yule rafiki yake aliye kuwa naye katika chumba cha Black Shadow anaweza kufahamu maeneo ambayo Ranjiti anapenda kuyatembelea kwa sana”
“Eheee umenikumbusha mama hivi siku ambayo uliwasikia wakizungumza kwenye chumba cha Black Shadow, Yan si alihusika?”
“Ndio lihusika”
“Basi mama nimeshapata kwa kuanzia, kila jambo kwa sasa litakwenda sawa, niachie mimi hiyo kazi”
“Sawa. Ila unataka kufanya nini?”
“Mama kila kitu nimekuambia niachie mimi, nikiimaliza kazi yangu nitakuletea ripoti kamili”
“Sawa ila kuwa makini kwa maana hawa watu mimi wala siwaamini sana”
“Usijali mama yangu, hivi nyumbani kwa Yan si unapafahamu?”
“Ndio napafahamu”
Phidaya akamuelekeza Shamsa na Sa Yoo nyumbani kwa daktari Yan, kutokana Sa Yoo ni mwenyeji sana katika nchi hiyo ya Japan, eneo hilo alilifahamu.
                                                                                                     ***
   Majadiliano ya dokta Ranjiti, dokta Yan na Kim ndani ya ndege, yalimchanganya rubani wake ambaye alikuwa ndani ya ndege hiyo pasipo bosi wake kuweza kufahamu. Mpango wa kwenda kumteka Black Shadow, kwenye hospitalini na kwenda kumuua kwa kumchoma moto. Aliweza kuisikia vizuri, rohoni mwake akajikuta akishindwa kuvumilia kuona tukio hilo likiwa linatendeka.
Mzee Yo, aliyasikiliza mazungumzo hayo hadi mwisho, bosi wake alipo ondoka katika eneo la karakana kwa haraka akashuka kutoka ndani ya ndege. Hakumuaga mtu, akapanda pikipiki yake, iliyo mpeleka moja kwa moja hadi nyumbani kwake. Kichwani kwake mawazo mengi yalizidi kukiandama kichwa chake, kila alipo jaribu kufikiria jinsi ya kumuokoa Black Shadow, alijikuta akishindwa kupata jibu kabisa.
“Nitafanyaje wakati kazi hii ni hatari sana. Laiti bosi akitambua nitakuwa sina kazi na pia anaweza kuniua”
Mzee Yo alizungumza peke yake akiwa chumbani kwake amejiinamia kwenye sofa lake. Japo ni rubani wa muda mrefu katika kampuni ya dokta Ranjiti, ila leo ndio aliweza kufahamu kwamba dokta huyo ni mtu katili sana. Kila alipo mfikiria Black Shadow, kijana ambaye ana ujuzi mkubwa wa kupigana, hadi akamteka kihisia, hakukubali kuona anakufa mikononi mwa dokta Ranjiti ambaye amepewa jukumu la kumtibu. Hakuhitaji kufahamu ni kitu gani ambacho Black Shadow amekifanya kwa daktari huyo ila kitu alicho kihitaji ni kuhakikisha kwamba kijana huyo anakuwa hai.
Kwa haraka haraka, akilini mwake akafikiria ni mtu gani anayeweza kumsaidia katika kazi hiyo, kura yake ikatua bibi Eyna. Mwanamke aliye kuwa na mahusiano naye miaka mingi ya nyuma, kabla hawajatengana. Akakumbuka kwamba bibi Eyna anafanya kazi katika hospitali ya dokta Ranjit, kwa haraka akachukua kitabu chake cha kuhifadhia kumbukumbu. Akaanza kufungua kurasa kadhaa, akiitafuta namba ya simu ya bibi huyo. Akabahatika kuipata namba hiyo. Akaingiza namba hizo kwenye simu yake ya mkononi, akaiweka sikioni simu yake na kusikiliza, kwa bahati nzuri simu hiyo iliita kwa muda kisha ikapokelewa.
“Habari yako Eyna”
Sauti ya Mzee Yo, haikuwa ngeni masikioni mwake, moyo wa bibi Eyna ukajikuta ukikubwa na furaha kubwa.
“Safi tu Yo habari za siku nyingi?”
“Safi upo wapi kwa sasa?”
“Nipo kazini”
“Naweza kuja kukuona mpenzi?”
“Mmmm jamani, mpenzi si usubiri nikitoka”
“Hapana ni muhimu sana, nahitaji kukuona mida hii nina hamu sana na wewe”
“Waooo njoo basi nakusubiria”
Mzee Yo, akakata simu baada ya kutumia mameno ya ulaghai kwa mpenzi wake huyo, ambaye aliweza kuachana naye kutoka bibi Eyna enzi za ujana wake hakutulia na mwanaume mmoja. Ndani ya dakika thelathini akawa amefika katika hospitali ya dokta Ranjiti, hakupata tabu sana kuweza kukutana na Bibi Eyna, ambaye alimkumbatia kwa furaha mara baada ya kumuona.
Japo ni mzee ila bibi Eyna bado ana hulka za ujana, hakusita kumpiga mzee Yo busu la mdomoni.
“Baby nimefurahi kukuona jamani”
“Hata mimi, ila unaonekana una joto kali”
Mzee Yo, alitania, huku kiganja chake akiwa amekiweka shingoni mwa bibi Eyna.
“Ni joto la kulimisi penzi lako?”
“Kweli?”
“Ndio”
“Ninaweza kukupatia ubaraidi wakati huu?”
“Mmmm jamani, mbona unanisisimua”
“ Sikusisimui ila ninacho kizungumza nina kimaanisha baby”
Mzee Yo, aliweza kuutambua udhaifu wa mwanamke huyo, kwani anapenda sana ngono kuliko hata kula ndio maana walishindwana kipindi cha ujana wao.
“Sasa hapa tutafanyia wapi mume wangu?”
“Kwani hakuna chumba cha siri tukafanya mambo?”
Bibi Eyna akaichekecha akili yake kwa haraka huku akifikiria sehemu gani, akakumbuka kwamba ndani ya hospitali hapo kuna vyumba vya siri ambavyo vipo ardhini ila havitumiki kwa muda mrefu sasa. Hakujua uwepo wa Black Shadow ndani ya moja ya vyumba hivyo, kwani uwepo wa Black Shawod ni siri iliyopo kwa madaktari wakubwa tu, hata madaktari wengine hawatambui.
“Hembu kaa hapo niandae mazingira kisha naja kukuchukua”
“Mazingira gani baby”
“Ngoja kuna vyumba vipo huko ardhini nahisi huko kutatufaa mpenzi wangu”
Bibi Eyna akaondoka katika eneo hilo akiwa mwingi wa furaha na amani sana, haraka haraka akaelekea kweye ofisi ya dokta Ranjiti akagonga kwa muda, hakuitikiwa, akausukuma mlango na kukuta haujafungwa kwa funguo.
Akachungulia ndani hapakuwa na mtu, akaelekea ofisi ya Phidaya, akagonga pia akukuta hakuna mtu. Akaelekea katika ofisi ya dokta Yan, ambaye ni msaidizi wa dokta Ranjiti naku huko pia hakukuta mtu. Siku hiyo akajiona ni mtu mwenye bahati sana, akarudi sehemu alipo muacha Mzee Yo. Akamuomba amfwate kwa nyuma.
Wakaingia kwenye chumba ambacho kina lifti iliyo washusha chini. Kitendo cha kufika eneo hilo, bibi Eyna akamkumbatia kimahaba mzee huyo na kuanza kumpiga mabusu mfululizo.
“Baby tulia kwanza tuchunguze kuna weza kukawa na mtu humu akatuona ikawa tatizo”
“Baby hakuna mtu bwana”
Mzee Yo, akitazama saa yake ya mkononi inamuonyesha ni saa mbili usiku. Muda wa Black Shadow kuja kutolewa kwenye eneo hilo ni saa nne usiku. Kutokana na yeye ni mwanaume rijari, hakuona vibaya akampatia haki bibi Eyna, haraka haraka ili kuzidi kumchanganya na kumuweka karibu pale ataka anza kufanya mpango wake, kwa maana anatambu lazima Black Shadow yupo kwenye chumba hicho, kutokana alisikia jinsi Kim alivyo kuwa akielekezwa chumba alicho Black Shadow, kila alama aliyo isikia kwenye ndege ipo kwenye moja ya mlango.
Kwa haraka, akalipandisha gauni la bibi Eyna hadi kifuani, akamshusha chupi aliyo ivaa, na yeye akashusha suruali na nguo yake ya ndani. Agamshikisha ukuta bibi Eyna, bila hata maandalizi, ya kumuandaa mwenza wake, akaanza kumpa haki yake.
Bibi Eyna, akaanza kutoa miguno ya mahaba, kwa kasi ambayo anakwenda nayo Mzee Yo, ilimfanya apagawe na zaidi ya mara nne, bibi Eyna alijikuta anafika kileleni. Mzee Yo akafunga goli lake dakika kumi baada ya mchezo kuanza.  Bibi Eyna akajikuta akikaa chini kwa jinsi alivyo choka kwani ni muda mrefu hajakutana na mwanaume wa kumpeleka kasi namna hiyo.
Mzee Yo akapandisha nguo zake, akajiweka sawa, bila ya kupotaza muda akaanza kufungua mlango ambao alisikia maelekezo yake yakiwa yanatolewa. Kweli akamkuta Black Shadow akiwa amelala kwenye kitanda hicho akiwa hajitambui, ili kuhakikisha ni yeye akamsogelea karibu, kinyago cha Black Shadow alicho kivaa kilimuhakikishia kwamba ndio mwenyewe.
“Haaaa…….!!!”
Sauti ya Bibi Eyna ilimstua akageuka na kumkuta akiwa amesimama kwenye mlango huku mdomo wake ukiwa mdomoni.
“Shiiiii”
“Huyo si ndio mgonjwa mbaye alivamiwa majuzi?”
Bibi Eyna alizungumza huku akienda kumtazama Black Shadow kitandani alipo lala.
“Nahitaji kumtorosha hapa hospitalini”
“Kwa nini?”
“Kuna watu wanahitaji kumuua”
Macho yakamtoka bibi Eyna kwa kushangaa
“Usishangae, dokta Ranjiti  anahitaji kumua, sasa nahiyaji tumtoe kiakili pasipo mtu mwengine kutambu”
“Si unanitafutia matatizo jambo hili likijulikana”
“Una nipenda ua hunipendi?”
“Nakupenda”
“Fanya kama ninavyo hiaji akiendelea kukaa hapa ninaimani wakuu wako watakuja kumuua”
“Ina maana dokta Ranjiti anahitaji huyu kijana kumuua?”
“Hilo ni jibu na si swali, hatuna muda wa kupoteza nilaziama kumtoa humu ndani”
“Sasa utambeba wapi,  kwa maana hivi hivi ataonekena”
Mzee Yoo akatoka kwenye chumba hicho, akaingia kwenye chumba kingine, ambapo akakuta maboksi mengi makubwa yakiwa yamepangwa, akalifunua boksi moja na kukuta likiwa halina kitu ndani yake, kwa ukubwa wa boksi hilo akamini kwamba litamsaidia katika mpango wake.
Akarudi nalo kwenye chumba alipo Black Shadow, akamkuta bibi Eyna akiwa amelifunua shuka lililo kuwa limemfunika Black Shadow nusu mwili, msho uliopo kwenye mbavu zake ukmfanya Mzee Yoo aumize kichwa kufikiria jinsi ya kumuingiza humo.
“Unataka kumingiza kwenye boksi?”
“Ndio”
“Sasa si ataumia sana?”
“Hakuna jinsi, mshike huko miguuni”
Bibi Eyna akamshika Black Shadow miguuni, Mzee Yo naye akamshika mabegani, taratibu wakamuingiza kwenye boksi wakimkunya, kidogo, akalalia ubavu ambao hauna jeraha. Wakaichomo mirija ya madripu ya maji.  Walipo fanikisha zoezi lao, wakatoboa matundu mawili madogo ya kuingizia hewa.
“Yo ttukikamatwa?”
“Hatuwezi kukamatwa?”
“Getini tutatokaje?”
“Gari lako si lipo?”
“Ndio lipo”
“Basi utanisaidia kumtoa getini kisha utanipatia mbele kwa mbele”
“Mmmmmm haya”
Wakalinyanyua boksi kwa umakini, wakaingia nalo kwenye lifti, wakafika hadi juu, bibi Eyna akamuelekeza Mzee Yo mlango wa nyuma wa hospitali hiyo, ambapo kwa bahati nzuri hakuna kamera za ulinzi. Bibi Eyna akaenda hadi kwenye maegesho ya magari, ambapo akachukua gari yake aina ya Toyota hardbody. Akaipeleka hadi eneo lilipo boksi na mzee Yo, wakalipakiza boksi kwa nyuma, kisha mzee Yo akaelekea alipo iacha pikipiki yake. Bibi Eyna akaliendesha gari lake hadi getini ambapo alisimamishwa na askari wanao linda hapo getini.
“Bibi leo naona mataka taka yamekuwa mengi sana”
Askari huyo alimtania bibi Eyna pasipo kutilia shaka kwamba ndani ya boksi hilo ndani yake kuna mtu
“Ndio mjukuu wangu, kuna kazi ya usafi nilikuwa ninaifanya basi nayapeleka dampo”
“Nikusindikize?”
“Hapana kuna sehemu nitapitia kwanza”
“Ahaa sawa bibi niletee pipi”
“Usijalii mwaaaaaaaaaa”
Askari hao walimzoea bibi huyo kwa tabia yake ya ucheshi, Mzee Yo akashusha pumzi nyingi baada ya kuona gari la bibi Eyna limeruhusiwa, akawasha pikipiki yake, akaelekea hadi getini akakaguliwa, alipo onekana yupo salama akaruhusiwa na kuondoka.
Akaelekea njia aliyo kwenda bibi Eyna, akalipita gari lake na kumuomba amfaywa sehemu wanapo elekea. Wakatoka kidogo nje ya mji, wakaingia kwenye barabara ya vumbi. Mwendo wa kilimita mbili, wakasimama kwenye moja ya kilima,
“Tumefika”
Mzee Yo alizungumza huku akizunguka nyuma ya gari, bibi Eyna naye akazunguka mara baada ya kushuka, wajalishusha boksi hilo.
“Wewe nenda uwahi kazini kwako”
“Saa ngapi?”
“Saa tatu kasoro”
“Mungu wangu. Ngoja nikuache baby, utanijulisha kila kitakacho endelea”
“Sawa”
Bibi Eyna akaondoka kurudi hospitalini, Mzee Yo, akalifungua boksi na kumtoa taratibu Black Shadow. Kutokana ana nguvu za kutosha akambeba kiungalifu, taratibu akapenya naye kwenye mwanya wa mwamba mkubwa uliopo kwenye kilima hicho. Akawasha taa zilizo onyesha eneo zima la ndani, ni pango moja kubwa ambalo anahifadhia vitu vyake vya thamani sana. Ndani ya pango lake ameweza kuweka huduma muhimu kwa binadamu, ambazo mtu anaweza kukaa ndani ya pango hilo hata zaidi ya mwezi mmoja asitoke nje kabisa.
Akamlaza Black Shadow kwenye moja ya kitanda, akamfunika na blangeti zito kutokana na baridi kali iliyomo ndani ya pango hilo.
Alipo hakikisha kuna usalama, akafungu mlango na kuanza kutembea kwenye kordo ndefu. Akafika kwenye ngazi kabla hata hajaanza kuzipandisha, mlango unao fanania na ukuta ukafunguliwa, akaingia mtoto anaye mpenda kama mjukuu wake anaye ishi kwenye kituo cha kulele yatima.
“Soroo vipi umefwata nini huku usiku huu?”
“Nimekuja kukuangalia wewe babu kama upo”
“Sawa tena umenirahisishia, nilikuwa ninakuja huko huko. Ila twende nikakuonyeshe kitu”
“Umeniletea zawadi nini?”
“Wewe twende”
Akampeleka Soroo, hadi kwenye sehemu alipo muacha Black Shadow. Soroo alishangaa kumuona mpiganaji hiyo, kwani aliishia kumuona kwenye luninga tu. Mzee Yo akamuomba mtoto huyo alicho kiona iwe siri yake asimueleze mtu wa aina yoyote hata walezi wa chuo chake wanao mlea.
                                                                                                      ***
   Majira ya saa tano usiku dokta Yan akasimamisha gari lake kwenye maegesho ya nyumbani kwake, ukimya uliopo kwenye nyumba yake kidogo ukaanza kumpa wasiwasi, kwani walinzi wake wanao zunguka zunguka katika eneo la nyumba yake leo hawapo.
Akazama ndani ya gari, akachukua bastola yake na kutoka akiwa ameishika vizuri mkononi mwake. Akaanza kutembea kwa tahadhari kuelekea ndani ya nyumba yake. Akafungua mlango kwa tahadhari kubwa, akawasha taa ya ukutani kwake. Macho yake yakatua  sebleni juu ya meza alipo mkuta Black Shadow amemuwekea kisu cha shingo mke wake huku mtoto wake wa miaka mitatu akiwa amezibwa mdomo, na kufungwa mikono na miguu kwa nyuma na kulazwa sakafuni akiendelea kubingiria bingiria huku akilia. Dokta Yan akahisi haja ndogo ikipenyeza kwenye nguo ya ndani huku taratibu ikishuka kwenye mapaja yake, kwani hakufikiria kumuona Black Shadow nyumbani kwake kwa wakati huo wa usiku.

 

SORRY MADAM (60)  (Destination of my enemies)

 

“Umefwata nini nyumbani kwangu?”
Dokta Yan alizungumza huku taratibu akipiga hatua za kusonga mbele huku akielekea sehemu alipo simama Black Shadow na bastola yake akiwa ameitanguliza mbele.
“Unajua ni kitu gani kilicho nileta hapa”
Sauti ya kike ndio ilimstua dokta Yan, anatambua fika kwamba Black Shadow ni mwanaume, huyu aliye kuja kwake usiku huu ni nani
“Weka silaha yako chini la sivyo nitamchinja mke wako”
Dokta Yan akayatupia macho yake kwa mke wake anaye tetemeka mwili mzima. Sura ya woga ya mke wake iliyo jaa machozi mengi ndio ilimfanya achukue uamuzi wa bila kupinga kuiweka bastola yake chini.
“Niambie yupo wapi Black Shadow?”
“Sifahamu kusema kweli”
“Acha uongo wewe na doka Rnjiti mulipanga kumuu kwa kumchoma moto”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya ukali, macho yakamtoka dokta Yan kwani hakuamini mambo hayo kuna mtu anayatambua kati yake yeye, dokta Ranjiti pamoja na Kim, ambaye wamempa jukumu hilo.
“Moja, mbili, ta……”
“Nasema nasema usimuue mke wangu”
Dokta Yan, alizungmza huku mwili ukimtetemeka baada ya kuona kisu alicho kishika huyu Black Shadow wa kike kikianza kupita kwenye shingo ya mke wake.
“Ni kweli tulipanga hivyo ila alitoka”
Dokta Yan alizungumza huku akipiga magoti chini mikono yake yote miwili akiwa amevikusanya viganja vyake kwa pamoja kwa ishara ya kumyenyekea Black Shadow huyo.
“Muongo wewe”
“Kweli Ranjiti ndio anayejua ni wapi al……..”
Hata kabla dokta Yan hajamalizia sentesi yake, risasi moja iliyo ingilia kwenye upenyo mdogo wa kioo, ikatua kichwani mwa dokta Yan na kumchangua ubongo, watu wote ndani ya nyumba wakashangaa. Ukunga mkali wa kelele alio utoa mke wa dokta Yan ndio ulimfanya Shamsa kustuka. Macho yake akayatupia dirishani risasi ilipo tokea hakuona mtu. Kwa haraka akatoka nje huku akiwa anakimbia, akatizama kona zote ila hapakuwa na mtu. Kwa haraka akarudi katika sehemu alipo isimamisha pikipiki yake na kuondoka kwa kasi katika eneo hilo na kuanza safari ya kurudi hotelini.
Alipo fika njiani, akavua nguo alizo zivaa na kubakiwa na nguo za ndani, akafungua begi lake dogo la mgongoni na kuvaa suruali yake pamoja na tisheti, akaziweka nguo za Black Shadow ndani ya kabegi kake na kuendelea na safari yake ya kwenda hotelini.
Haikumchukua muda sana akawa amefika, akashuka kwenye pikipiki yake na kuanza kutembea kwa haraka kuelekea kwenye lifi, akaminya kitufe cha kufungulia lifti hiyo, ilipo funguka akaingia huku kichwani mwake akiwa amejawa na msongamano mkubwa wa mawazo.
‘Ni nani atakaye kuwa amemuua’
Shamsa aliwaza kichwani mwake huku akiwa ameegemea kwenye lifti hiyo huku macho yake yote akitazama juu. Alipofika kwenye gorofa ya saba lifti ikafunguka na kuanza kutembea kwa mwendo wa kasi hadi kwenye mlango wa chumba chao, akagonga, baada ya dakika mlango ukafunguliwa na Sa Yoo.
“Vipi umefanikiwa?”
“Hapana dokta Yan amekufa”
Shamsa alizungumza huku akijibwaga kwenye sofa na kibegi chake akakitupia pembeni
“Weeee, umemuua?”
“Hapana sijamuua mimi”
“Sasa imekuwaje amekufa?”
“Amepigwa risasi hata mimi sitambui ni nani aliye fanya hivyo”
Sa Yoo akabaki katika alama ya mshangao kwani swala alilo lisikia nalo ni jipya masikioni mwake.
                                                                                                       ***
  Hali ya Black Shadow, ikaanza kuleta matumaini machoni mwa Mzee Yo, aliye amua kuchukua jukumu la kumtibu Black Shadow kwa dawa za miti asilia. Baada ya Black Shadow, kuzinduka kutoka usingizini, Mzee Yoo aliweza kumtuliza kwa maana muda wote aliweza kuliita jina la Phidaya. Baada ya kumtuliza kwa muda na Black Shadow kuweza kutulia,  Mzee Yo alimueleza kila kitu alicho kisikia kwenye ndege kikijadiliwa na madaktari ambao walikuwa wakimtibu.
Mzee Yo, hakusita kuzungumza jitihada ambazo alizifanya akiwa miongoni mwa mashabaki wake, jinsi alivyo mtorosha hospitalini na kumleta huku mapangoni. Eddy akajipapasa usoni mwake na kukuta kinyago chake kikiwa kichwani. Kwa maelezo ambayo Mzee Yo amempatia, aliamini kwamba huyo ni mtu mzuri kwake na mwenye busara nyingi. Hakuona haja ya kuendele kukaa na kinyago hicho, taratibu akakifungua na kukivua.
Mzee Yo, akaonekana kushangaa kidogo, ila akajizuia kwani sura hiyo mara kadhaa aliweza kuiona kwenye vitua vya televishion vikidai kwamba mtu huyo ni mualifu.
“Natambua wewe ni mwema kwangu, huto weza kuzungumza kitu mbele za watu kitakacho hatarisha maisha yangu”
Eddy alizungumza kwa sauti iliyo jaa unyonge mwingi, hadi Mzee Yo akamuonea huruma.
“Ndio, wewe si Eddy unaye tafutwa na polisi”?”
“Ndio ni mimi”
Eddy akaanza kumuelezea Mzee Yo historia nzima tangu alivyo weza kuingia ndani ya Japani, lengo lililo mleta ndani ya nchi hiyo hakuweza kulitimiza kutokana na matatizo ambayo yalimpata. Mzee Yo akatokea kumsikitikia Eddy kwani ni kijana ambaye hana hatia, ila nchi yake ndio inamuhitaji yeye kuweza kurudi kuendelea kutumikia taifa lake.
“Kuna mjukuu wangu anaitwa Soroo, huwa mara kadhaa anakujaga humu kwenye hili handaki nakumba asiijue sura yake, na endapo kama atakuja nakuomba uvae hicho kinyago chako”
“Sawa, hilo halina tatizo”
   Siku mbili zikakatiza Eddy akiendelea kutibiwa na Mzee Yo. Dawa alizo zitumia zikazidi kumpa unafuu wa kupona, maumivu yakaanza kutoweka siku hadi siku. Siku ya tatu asubuhi Eddy kwa mbali alihisi vishindo vya mtu akija ndani ya pango hilo akipitia njia nyingine, kwa haraka akavaa kinyago chake kama alivyo ambiwa na Mzee Yo, aliye toka asubuhi kwenda mjini kuangalia hali halisi inavyo kwenda. Akamuona mtoto ambaye moyo wake ukampasuka alipo muona kwa mbali, mtoto huyo anafanana sana na mwanaye Junio. Ila huyu anaonekana ni mdogo kwa Junio wake.
Mtoto huyo hakuonekana kumshangaa sana Black Shadow kutokana alimuona tangu siku ya kwanza. Mtoto huyo alipo mkaribia Black Shadow akamsalimia huku akimpa mkono. Taratibu Eddy akachuchumaa na kuushika mkono wa mtoto huyo, huku kwa mbali macho yake yakimlenga lenga.
“Marahabaa, wewe ni Soroo si ndio”
“Ndio ni mimi”
Uchangamfu wa mtoto huyo ukazidi kumpagawisha Eddy, kwani Junio wake naye alikuwa hivyo hivyo, ila sema ndio hivyo hayupo tena duniani.
“Unaendeleaje?”
“Nipo fiti, vipi mbona umeniuliza hivyo?”
“Juzi babu alikuleta ukiwa unaumwa sana”
“Ahaa nipo safi, umekuja kumfwata yeye?”
“Ndio ila pia nimekuja kukujulia hali wewe”
Uongeaji mwingi wa mtoto huyo huwezi kuamini kwamba ana umri wa miaka minne. Vitu vingi aliweza kufanana na Junio ila ni vitu vichache tu ambavyo hajafanana na Junio. Mchana wa siku hiyo wakapika chakula cha mchana na Black Shadow huku wakizungumza mambo mengi sana. Wakala kwa pamoja na jioni ilipo fika Soroo, akaaga na kuondoka zake,
 Siku kadhaa zikakatika Eddy akiendelea kurudi katika afya yake, taratibu akaanza kufanya mazoezi ya kukimbia milimani kujiweka fiti. Kadri ya siku zilivyo zidi kwenda ndivyo jinsi alivyo zidi kuwa fiti sana, urafiki wake na Mzee Yo, ukazidi kukomaa hadi ikatokea kipindi akamchukulia kama baba yake, kwani mzee huyo aliweza kumlea na kumchukulia kama mwanaye.
“Malengo yako ni nini Eddy?”
Mzee Yo alimuuliza wakiwa katika meza ya chakula ndani ya pango hilo.
”Sina familia kwa sasa, kama nilivyo kueleza mke, mwanangu na mama yangu walifariki siku moja. Sitamani kurudi Tanzania kwasasabu ni nchi ambayo nikirejea nitaumia sana pale nitakapo ona makaburi ya familia yangu”
“Huna mpango wa kuoa?”
Eddy akatulia kwa muda, kumbukumbu zake zikarudi kwa nesi aliye weza kumuona kwenye hospitali aliyo kuwa anatibiwa, nesi  huyo aliweza kufanana sana na marehemu mke wake ambaye ni Phidaya.
“Kuna nesi mmoja niliweza kumuona kwenye hospitali niliyokuwa ninatibiwa. Yule nesi amefana sana na mke wangu. Ukiachilia mbali sana huyu Soroo naye anafanana sana na mwanangu”
“Kweli……!!!?”
“Kweli, sema mwanangu alikuwa ni mkubwa kumpita yeye”
“Huyu Soroo, ni mtoto wa marehemu rafiki yangu, alifariki kwa ajali ya ndege akiwa yeye na mke wake, basi nikaona nimchuku mwanae na kumkabidhi katika kituo cha kulelea yatima”
“Hapo analelewa na mara kadhaa huwa ninamleta huku, sikuweza kuishi naye kutokana sina mke wala mtoto, isitoshe kazi yangu ni yakusafiri safari sana”
“Ahaaa ulilo lifanya ni jambo jema. Ila laiti kama mke wangu angekuwa hai basi ningemchukua huyu mtoto na kumlea kama mwanangu”
Eddy alizungumza huku machozi yakimlenga lenga, taratibu akanyanyuka na kutoka nje ya pango hilo kupunga upepo.
                                                                                                           ***
  Watumishi wengine wa tume ya taifa kwa haraja wakamnyanyua bwana Barnaba Lukas, na kuanza kumpa huduma ya kwanza, watu wote walio weza kuhuduria kwenye viwanja vya tume kuu ya taifa ya uchaguzi walijikutwa wakibaki katika hali ya sinto fahamu, kwani kila mmoja alizungmza yake. Kuna walio sikika wakisema kwamba atakuwa ametupiwa jinni, wengine walisema labda alichukua pesa za watu na matokeo yamekwenda ndivyo sivyo.
Bwana Baraba Lukas akawahishwa hospitali kuu ya Taifa ya Muhimbili, huku jukumu lake akilichukua makamu msaidizi. Akili na mawazo ya kumfikiria bwana Lukasa Barnaba yakafutika vichwani mwa watu walio kusanyika katika eneo hilo. Mawazo yao wakayarudisha kwenye matoekeo yanayo kwenda kusomwa dakika chache zilizo pita.
Makamu wake, Bi Mwenda, hakuhitaji kurembesha wala kuwa na hofu yoyote juu ya kuyatangama majibu hayo. Akaanza kuwataja walio pata kura chache za chini kabisa, kisha akabakisha vyama viwili vilivyo kuwa na ushindani mkubwa sana.
Akameza fumba la mate kusuuza koo lake, akaiweka vizuri miwani yake kuziona idadi ya kura zilizo andikwa kwenye karatasi hilo, bila ya kujishauri mara ya pili. Akamtaja mshindi wa uchaguzi huo kwamba ni Mzee Godwin.
Wanachama wa chama DTPP, waliopo katika eneo la viwanja vya tume ya taifa wakajikuta wakinyanyuka kwenye viti vyao na kushangilia kwa nguvu. Kelele na vifijo vikatawala maeneo yote ya Tanzania.
Shangwe na vigelegele, vikazidi kutawala kwa watu wote walio kiunga mkono chama cha DTPP, wanachama wa chama tawala walio kuwa wakimuunga mkono Raisi Praygod Makuya, wengine walishindwa kuyazuia machozi yao kuona raisi wao akiwa ameshindwa kwenye kura zilizo pigwa Tanzania nzima.
Wengine walijikuta wakimbeza raisi wao mpya kwamba ni gaidi, wengine walijaribu kuleta fujo kwenye baadhi ya vituo ambavyo walikwenda kupiga kura wakidai kwamba kura zimechakachuliwa. Ila walicho ambalia ni kipigo kikali kutoka kaika askari wa kutuliza ghasia FFU. Na wengine wakajikuta wakisota maabusu kwa kutokana na kukamatwa.
Raisi Praygod hakuamini kwamba ndio hivyo ameng’atuka madarakani, mambo aliyo mfanyia mzee Godwin, yakaanza kujirudia kama mkanda wa video kichwani mwake, akakumbuka jinsi alivyo hakikisha kwamba anamsaka kwa udi na uvumba kama gaidi, leo hii anampisha ikulu gaidi huyo.
‘Si ataniua huyu?’
Raisi Praygod alizungumza huku akiwa amejilaza kwenye sofa lake, machozi yakimlenga lenga.
                                                                                                ***
  Kitendo cha dokta Yan kuuawa kilizidi kumkosesha amani Shamsa, hata asubuhi kulipo pambazukafuraha yake haikuwa kama siku nyingine. Kitu cha kwanza alicho kifanya ni kuwasha Tv, iliyopo chumbani kwao, akatazama kitu gani kinacho endelea. Kweli akakuta taarifa ya dokta Yan kuuawa ikiwa imeshika vichwa vya habari, huku ikisadikika kwamba muuji aliye fanya tukio hilo la mauji alikuwa nje ya nyumba hiyo.
Polisi wakatangaza kufanya uchunguzi mkali kwa daktari huyo kuuawa. Mlango ukagongwa, Shamsa kwa haraka akayatupia macho yake kwenye mlngo huo, wasiwasi mwingi ukamjaa na kujiuliza ni nani ambaye anagonga mlango asubuhi hiyo.
  Akanyanyuka na kwenda kuufungua, akamkuta Phidaya akiwa amesimama nje ya mlango huo akiwa na wasiwasi mwingi huku amevalia nguo nyeusi tupu.
“Mama vipi mbona hivyo?”
Shamsa alizungumza baada ya kuufunga mlango kwa ndani, huku akimfwata Phidaya kwa nyuma kuelekea kwenye sofa.
“Niambie ukweli mwanangu si wewe uliye muua dokta Yan?”
Phidaya alizungumza kama mtu aliye changanyikiwa, kidogo Shamsa akastuka, akashusha pumzi nyingi chini na kujiweka vizuri kwenye sofa huku akimgeukia Phidaya.
“Mama amini mwanao wa kike siwezi kufanya mauji”
Phidaya kusikia kuali hiyo ya Shamsa akamkumbatia kwa furaha, kwani mpango mzima wa Shamsa kwenda kwenye nyumba ya dokta Yan, Phidaya aliuelewa vizuri sana.
“Nisikudanganye mwanangu tangu nilipo sikia taarifa ya dokta Yan kuuawa basi nilitambua kwamba wewe ndio umefanya hivyo”
“Hapana mama siwezi kufanya hilo swala”
“Eheee niambie imekuwaje kuwaje”
“Nilikwenda hadi pale lisaa moja kabla sijaingia nyumbani kwake, niligundua kwamba anaishi na mke wake pamoja na mtoto wake, nyumba yake ilikuwa na walinzi wanne hivi….”
“Lengo langu lilikuwa ni kumbana akiwa anashuka kwenye gari ila nikaona ni wazo baya, nilicho fanya ni kuwazimisha moto walinzi wote kisha…..”
“Ngoja kwanza, mwanangu. Kuzimisha moto ndio nini?”
“Hahaa mama, kuwazimisha moto ni kuwazimisha”
“Ahaaa kwahiyo uliwapiga hadi wakazimia?”
“Ndioo, hujakosea”
“Ehee niambie ikawaje?”
Phidaya alizungumza kwa furaha huku meno yake yote thelethini na mbili yakiwa nje
“Walinzi wenyewe wachovu hao, basi niliingia ndani na kumbananisha mkewe pamoja na mwanaye, haikupita muda sana akaja kuingia tu ndani mtu mzima mwili mzima ulikuwa unamtetemeka”
“Ila kwa bahati mbaya sikufanikiwa kutambua Black Shadow ni sehemu gani alipom kwani mauti yalimpata”
“Mmmm mwanangu unatakiwa kuwa makini, yaani sitambui nikupe zawadi gani leo”
“Zawadi kwa kazi gani niliyo ifanya?”
“Htahiyo uliyo ifanya ni nzuri?”
“Kwanza dokta Ranjiti amerudi nyumbani?”
“Bado yupo Korea, nilijaribu kumtafuta hewani namba yake haipatikani, sasa sijajua kama taarifa za mwenzake amezipata”
“Mmmmm sijui”
“Muamshe na mwenzako twende kwenye maduka ya nguo mukachague nguo kisha mimi nitakwenda msibani si unajua inabidi kuwa karibu  na wanafamilia yake”
“Ahaa sawa mama”
Shamsa akamuamsha Sa Yoo, akamueleza juu ya safari hiyo ya asubuhi, Sa Yoo kutokana na kupenda kwake kuvaa haraka haraka akaanza kujiandaa, kwa siku hiyo wala hakutamani kunywa chai, walipo maliza wote wakatoka kuelekea kwenye maduka makubwa kwenda kuchagua nguo watakazo
                                                                                                             ***
    Asubuhi na mapema Mzeee Yoo na Eddy aliye valia kofia iliyo shuka kidogo na kuuficha uso wake, huku akiwa amejipachika ndevu za bandia zilizo mbadilisha muonekano wake, waliianza safari yako kutoka kwenye msitu wanai ishi kuelekea mjini, wakiwa kwenye pikipiki. Utaalamu wa uendeshaji wa pikipiki wa mzee Yo, ulimfanya Eddy kuufurahia kwani aliweza kwenda kasi sana kupita hata magari ambayo yamewatangulia.
Wakaingia mjini majira ya saa tatu, habari ya kifo cha dokta Yan ndio ilikuwa ikizungumziwa kila mahali walipo pita. Wakaingia kwenye moja ya mgahawa kujipatia kifungua kinywa.
“Huyu dokta ni mmoja wa madaktari walio kuwa wakikutibu?”
“Weee”
“Yaa na ndio daktari ambaye alihusika katika mipango ya kutaka kukuaa. Masikini ya Mungu katangulia yeye kabla yako”
“Doo dunia hii, alitaka kuniua mim kisa nini?”
“Wala sielewi”
“Mungu amsam……”
Eddy hakuimalizia sentensi yake akamuona nesi aliye muona hospitalini akitoka kwenye moja ya duka kubwa la nguo lililopo upande wa pili wa barabara, akiwa amevalia nguo nyeusi huku akizungumza na simu.
Akaweka kikombe cha chai taratibu mezani, Mzee Yo naye aliweza kumshuhudia Phidaya mke wa bosi wake dokta Ranjiti akiwa amesimama kwenye duka hilo kubwa maarufu kwa uuzaji wa nguo za kike. Taratibu Eddy akasimama kutoka kwenye kiti alicho kuwa amekalia, akaanza kupiga hatua za haraka kuelea barabarani huku macho yake akiwa amemkazia Phidaya ambaye yupo bize kwa kuzungumza na simu.
Gafla hata kabla hajaanza kuvuka barabara, gari moja jeusi aina ya haisi, likasimama sehemu alipo simama Phidaya, wakashuka watu wawili walio valio vinyago vyeusi wakamata kwa nguvu na kumuingiza ndnai ya gari hilo na kuondoka naye kwa nguvu, kitendo kilicho shuhudiwa na Eddy pamoja na Shamsa, kupitia kwenye kioo kikubwa akiwa ndani ya duka hilo.
Eddy akavuka kwa kasi bilia kujali magari yanayo pita kwenye barabara hiyo huku Shamsa naye akitoka kwa kasi nje, wote wawili wakajikuta wakisimama katika sehemu aliyo tekewa Phidaya na macho yao wakilishuhudia gari hiyo ikitokomea kwa mbali.

Tunashukuru kwa kututembelea(mbukuzi blog) tunakuahidi hatutakuangusha tutakupa habari zote kila siku tutembelee kwa kuandika MBUKUZI BLOG..endelea kusoma hapo chini.