Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa

Ilipoishia….
Nikaachia msunyo mkali na kuirudiisha gari yangu upande wa kushoto nilipo toka na jamaa akanifwata nilipo,sikuwa na budi zaidi ya kutoka nje ya barabara kuepika kugongana uso kwa uso na gari hilo.Gari ikaanza kunishinda nguvu badala ya kufunga breki kwa kuchangunyikiwa nikawa na kazi ya kuongeza kasi.Nikastukia gari ikaanza kupiaga kubingiria kwa kasi ya ajaba.Jinsi inavyobingiria ndivyo jinsi ninavyo jigonga ndani ya gari hadi giza jingi likayavaa macho yangu na kutulia kimya…

Endelea…
….Kwa mbali nikaanza kusikia milio ya ndege,nikajaribu kuyafumbua macho yangu ila kichwa changu nikakuta kinaniuma sana.Nikakajikaza sana na kuyafumbua macho yangu yakakutana na mwanga mkali  wa juu unao ingi kwenye kioo cha mbele cha gari langu.Nikajaribu kujichunguza kwa umakini na kugundua mikono yangu imefungwa pamoja na mskani wa gari langu.Kila nanapovuta taswira ya sehemu nilipo,sijawahi kuiona siku hata moja.Miti mirefu iliyopo kwenye eneo zima lililo gari langu likazidia kunichanganya.

Baada ya muda kiogo nikastukia mlango ukifunguliwa na akasimama jamaa mwenye bunduki mbele yangu,huku akiwa amevalia mavazi meusi kuanzia juu hasi chini.Akanitazama kwa umakini kisha akaifungua mikono yangu na kunitoa ndani ya gari na kunitupa chini.Akaninyanyua na kuniweka begani,tukaanza kuondoka pasipo kuwezakujua ni wapi tunapo elekea,hatua kadhaa mbele nikaona jumba kubwa lililo zungukwa na miti mingi ambayo kwa mbali huwezi kugundua kama kuna jumba kubwa kama hili
Tukaingia ndani na jamaa akanibwa mbele ya watu wapatao ishirini walio shika bunduki zao.Mapigo ya moyo yakaanza kunienda kasi baada ya macho yangu kutazamana na mzee godwin ambaya jicho lake moja ameliziba na kitambaa cheusi.Mzee godwin akatabasamua na kumuamuru mtu aliye nilete katika sehemu hii kunifungua mikono yangu.
“eddy…..Eddy……Eddy my x-son”
Mzee godwin alizungumza kwa dharau kubwa huku akinizunguaka taratibu katika sehmu ambayo nimesimama.Kila niliye jaribu kumtazama sura yake haikuonyesha huruma hata kidogo japo kuna wasichana watatu ila nao sura zao zinaonekana zimejaa ukatili mkubwa.Kitu mabacho kinaniumiza
“usishangae sana kwa maana vita yangu mimi na wewe bado inaendelea”
Kwa haraka ninakumbuka kwamba huyu mzee niliambiwa kuwa amechanganyikiwa sasa sijajua imekuwaje hadi leo anamiliki kundi kubwa la watu kiasi hichi,gafla mzee godwin akanipiga mtama ulio niangusha chini vibaya sana na kunifanya niaanze kutoa miguno ya maumivu
“wewe ndio,chanzo cha kuipoteza mali yangu.Wewe ndio mtu uliye mteka mwangua.Wewe sio mwanangu niambie yupo wapi mwanangu?”
Maswali ya mzee godwin yanakizidi kunichanganya kwani sikujua mwanaye anaye mzungumzia ambaye anadai nimemteka ni nani
“mi…Mi mbona sikuelewi?”
“ahaa hunielewi?”
Mzee godwin akanipiga teke la kifua na kunifanya nijikunje huku maumivu yakizidi kunitawala kwenye kifua changu.Machozi mengi yakaendelea kunitoka
“ninakwenda kumuua mama yako?”
“hapana baba.Kumbuka kuwa mama ni mke wako wa ndoa.Mtu wa kuniua ni mimi hapa na wala si mama yangu.Nipo chini ya miguu yako”
Nilizungumaza huku nikiwa nimeishika miguu ya mzee godwin,akarudi nyuma na kunipiga teke lililo ifanya mikono yangu kuuiachia miguu yake
“yupo wapi,manka mwanangu?”
“manka,yupo arusha”
“arusha,arusha.Ndipo ulip kwenda kumficha si ndio?”
“hapana baba,mbona manka yeye ndio aliye watoroka nyinyi?”
“mimi sio baba yako na manka mwangu hawezi kunikimbia mimi”
Mzee godwin alizungumza kwa hasira huku akinitazama,akamuomba mwenzake mmoja waya wa umeme ambao unene wake  ni 1.5,akaukunja mara mbili na kuanza kunichapa nao kwa fujo huku akinitukana mimi na mama yangu.Nikazidi kulia kwa uchungu mkubwa,maumivu mengi yakazidi kuusonga mwili wangu.
Kila ninapojaribu kuizuia sehemu moja ya mwili wangu isichape basi sehemu nyingine ni lazima ichapwe kwa waya huu.Mzee godwin bila ya huruma akachukua pakti mbili zenye unga mwekundu na kuanza kunimwagia mwilini mwangu,hapa ndipo nikagunda ni unga wa pilipili ndio anao nimwagia.
Mauimivu ninayo yapata hayana mfano,kikubwa ambacho ninakilinda ni macho yangu yasiingie pilipili hii.Mzee godwin akawaamrisha watu wake wakamtafute manka na kumleta hapa mara moja.Mimi wakaniburura na kuniingiaza kwenye chumba kimoja ambacho kina giza nene.Baada ya dakika kama mbili nikastukia taa tatu kubwa zikiwaka zenye mwanga mkali ambao ukaanza kuniungaza mwili wangu,jasho ambalo linanimwagika kutokana na mwanga mkali,likazidi kunichoma kwenye vidonda vyangu.
Sehemu zote za majeraha ya mwili wangu,zikazidi kuniuma kiasi kwamba maumivu makali yakazidi kunitwala.Taa zikaendelea kuwa zaidi ya dakika kama kumi kisha zikazimwa.Nikabaki nikiwa nimekaa chini nimejikinyata mwili mzima huku nikiwa ninatetemeka kma nimepigwa na shoti.
Nikaendelea kukaa ndani ya chumba kwa muda mrefu,sikujua jinsi masaa yanavyo kwenda,mlango ukafunguliwa na ikawasha taa ya kawaida,mbele yangu akasimama mwanamke mrefu mwenye mwili mmnene kiasi.Mikononi akiwa ameshika sahani yenye chakua kingi,akachuchumaa na kuniwekea
“kama unaweza kula sawa,kama hutoweza kula acha”
Alizungumza na kutoka ndani ya chumba na kukifunga,nikaivuta sahani yenye chakula taratibu.Nikaanza kula wali uliopikwa vibaya kwani wala haukuiva vizuri,sikuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kuula huku nikiwa nimejikaza.Mwili mzima unanitetemeka kwa maumivu makali,chakula kingi kinamwagika chini kutokana na mikono yangu kutetemeka sana kiasi kwamba hata kukishika chakula ninashindwa.Sikumaliza kukila chakula kutokana na kutetemeka sana mwili wangu,
Masaa yakazidi kwenda pasipo kujua nini muafaka wangu wa kukaa ndani ya hili jumba.Nikaanza kukichunguza chumba sehemu yote na kugundua kimefungwa taa nyingi zenye ukubwa mbali mbali,nyengine zinaukubwa kama taa zinazo fungwa kwenye viwanja vya mpira ndio maana zina mwanga mkali sana.
Nikauchunguza mwili wangu na sehemu kubwa imeujeruhiwa.Nikiwa nimesimama nikastukia mlango ukifunguliwa,nikakaa kwa muda ila sikuona mtu akiingia ndani ya chumba.Taratibu nikaanza kupiga hatua za kwenda nje,nikachungulia wala sikumuona mtu wa aina yoyote.Nikapiga  hatu na kwenda nje kabisa na sikuona mtu wa aina yoyote katika eneo hili
Nikazidi kwenda mbele na yumba nzima inavyumba vingi sana,nikaendelea kuchunguza hadi nikafika sebleni.Nikachungulia dirishani na kumuona mzee godwin akiwa amesimama na watu wake wakilitazama gari linalo simama,baada ya gari kusimama wakashuka watu wawili walio valia mavazi meusi kish mmoja akafungua mlango wa nyuma akashuka manka akiwa na madam mery.Mzee godwin akamkumatia manka kwa furaha ila manka hakuonekana kuwa na furaha ya aina yoyote
“mama yangu mbona huna furaha?”
“baba kwa nini siku zote ulinificha?”
“nilikuficha na nini mwanangu?”
“baba kumbe eddy ni ndugu yangu.Umecha hadi nimefanya naye vitendo vya ajabu nikidhani ni mtu wa kaiwada kama wengine”
Maneno ya manka yakaibadilisha kabisa sura ya mzee godwin,akikunja kana kwamba amepigwa na mshale wa mgongo
“ina maana eddy amekubaka?”
“sio amenibaka,eddy alikuwa ni mpenzi wangu na hadi amenipatia ujauzito ila kwa bahati mbaya mimba ikatoka”
Mzee godwin akajishika kichwa na kuzunguka mara mbili huku akisunya misunyo mkali
“nitamuua eddy leo mbele yako”
Mzee godwin alizunguza na kuanza kupiga hatua za kuingilia kwenye mlango wa sebleni.Kabla sijafanya kitu chochote nikastukia nikishikwa kwa nyuma na kuzibwa mdomo
“shiii”
Ilikuwa ni sauti ya kike,mwanamke aliye nishika kwa nyuma akaanza kunivuta kwa nyuma huku tukielekea gizani.Tukatokea upande wa pili wa nyumba kwenye miti mingi,ndipo nikagundua mtu aliye nishika ni yule dada aliyekuwa ameniletea chakula
“kimbia kabla kifo hakija kukuta hapa”
Msichana alizungumza,huku akiwa amenitazama kwa macho makali,
“asante”
“amina ninaitwa”
“eddy”
“ninakujua,haya nenda”
Nikaanza kujikaza na kutokomea porini,japo mara kwa mara ninaanguka ila nikazidi kujikaza na kwenda mbele,giza likatawala anga  na sikujua ni wapi nielekeaa,nikajiegemeza kwenye mti mmoja huku nikiwa ninahema sana kwani umbali nilio ukimbia ni mrefu sana.Nikiwa nimeegemea mti nikasikia milio ya mbwa kwa mbali.
Nikatazama nilipo toka na kuona mianga mingi ambayo kwa muonekano ni mianga ya tochi na si watu wengine wanao nifwata ila ni mzee godwin na watu wake.Nguvu za mwili zimeniishia,nikaendelea kukimbia ila ikafikia sehemu nikashindwa kwenda mbela zaidi n kujikuta nikiangua chini na watu wa mzee godwin wakazidi kunikaribia nilipo anguka,nikasimama ila kabla sijapiga hatua hata moja nikastukia mbwa mmoja akinidaka mguu na kuniangusha tena chini

*****sory madam*****(50)
 

Kwa haraka nikaokota kigongo cha mti kilichopo karibu yangu, nikambamiza nacho mbwa cha kichwa  na kumfanya atoe ukelele huku akiniachia mguu wangu.Nikarudia tena kumbamiza  na kigongo kwa nguvu zangu zote hadi akalala chini na kutoa milio ya kuaga dunia, watu wa mze godwin hawakuwa mbali sana kutoka sehemu ambayo nipo, nikajikaza na kunyanyuka na kuendelea kukimbia kwa mwendo wa kuguchia kwani mwili mzima umejaa maumivu mengi yanayo nifanya nisikimbie sana.
“mungu nisaidie”

Nimaneno ambayo hayakuacha kutoka kinywani mwangu, kila ninapozidi kwenda mbele ndivyo jinsi ninavyo choka.Milio ya risasi inayo tokea nyuma yangu ikazidi kunichanganya na kunifanya niaanze kwenda mbele.Mwanga wa mbala mwezi kiogo ukawa unanisaidia kuona mbele ninapo elekea, nikazidi kupanda mlima ambao unamajabali makubwa sana na yakutisha.Kwa haraka haraka kwa elimu yangu ya jografia ambayo nimeisoma nikatambua sehemu hii nilipo itakuwa ni maeneo ya milima ya usambara, sema sehemu ndio siifaamu bado
Nikaingai kwenye moja ya jabali ambalo linashimo kubwa na kijibanza kwa ndani huku nikihema sana kwa huku woga mwingi ukiwa umenitawala.Mianga ya tochi ikazidi kunisogelea katika sehemu niliyo jificha, nikaendela kujibanza huku nimelala chini ndani ya chimo ili isiwe rahisi kwa wao kuweza kuniona.Nikawaona jamaa watatu wenye bunduki mkononi pamoja na tocho kubwa wakikipita nje ya jabali kubwa nililo jificha mimi.Wakapita na kuelekea mbele, nikawashuhudia watu wengi wanne wakiendela kutafuta kila sehemu
“huyu jamaa, atauwa amekimbilia sehemu hii hii”
Jamaa mmoja alizungumza huku akiendelea kumulika mulika kwenye mawe mengine.Mmoja wao akasimama pembezoni mwa jabali nililopo mimi na kuanza kumulika mulika ndani na kunifanya nijibanze kwenye sehemu ambayo mwanga wake wa tochi hauta weza kunimulika.
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda kasi baada ya jamaa kuanza kupiga hatua za kuingia ndani ya jabali,nikastuka baada ya kuona joka kubwa lililo jiviringisha na kukificha kichwa chake likiwa ndani ya jabali, hii ni baada ya jamaa kumulika mulika kwa tochi yake.
Mwanga wa tochi ukaanza kulifanya joka hili kuanza kujichezesha chezesha huku likaanza kujiachia, nikashusha pumzi huku macho yangu yakilitazama joka na jamaa ambaye anatembea kwa mwendo wa kunyata akiingia ndani ya pango huku akiwa ameshika bastola na tochi kwenye mikono yake.
Nikaanza kuhesabu moja hadi tatu kimoyo moyo na kuchomoka kwa kasi na kumpiga kikumbo jamaa na kumfanya kutoa ukelele ambao ukasababisha joka lililomo ndani ya jabali kujifyatua mwili wake, nikawa ninazisikia kelele za jamaa akito maumivu makali kwa nyuma na mimi nikazidi kutokomea nisipo pajua.Milio mingi ya risasi nikaisiki sehemu nilipo tokea na kunifanya nizidi kukimbia, sikujua hata nguvu za kukimbia zimetokea wapi.Niasimama kwenye moja ya mti na kuinama huku mikono yangu ikiwa imeshika magoti yangu na kuhema sana
“simama, na mikono juu, lasivyo nitakifumua kichwa chako”
Sauti kali ya  mwanaume niliisikia nyuma yangu ikiniamrisha, sikuwa na jinsi zadi ya kusimama huku mikono nikiwa nimeinyanyua juu.Nikataka kugeuka
“usigeke, pumbavu”
Nikabaki nikiwa nimesimama, nikisikilizia mtu huyo ataniamrisha nifanye kitu gani kingine.Nikastukia akinishika mikono yangu kwa nyuma na kuishusha chini,nikageuza shingo yangu kwa haraka na kukutana na watu wawili wa mzee godwin, huku aliye nishika akinigunga pingu mikoni.
“nimekwisha”
Nilijisemea kimoyo moyo,jamaa wakanichukua safari ya kurudi katika ngome ya siri ya mzee godwin,baba aliye nilea kuanzia utotoni hadi hapa nilipo fikia na siku zote niliamini ni baba yangu kumbe sivyo kama nilivyo dhania.
“jamani, semeni kiasi chochote cha pesa mimi nitawapa ili tu muniachie”
“pumbavu wewe, hatuna haja na pesa yako.Sisi kazi yetu ni moja tu.Kukurudisha mikononi mwa mkuu wetuu”
“sikilizeni, nyinyi ninwanaume wezangu,jaribuni basi kuniurumia.Mimi ni sawasawa na mdogo wenu.Hembu pigeni picha nikienda kuuawa, nyinyi mutafaidika na nini?”
Nilizidi kuashawishi jamaa waweze kuniachia ila hakuna ambaye ananisikiliza.Hadi tunafika kwenye jumba la mzee godwin hakuna hata mmoja aliye nikubaloa ombi langu.Tukaingia sebleni na kumkuta mzee godwin amekaa na manka pamoja na watu wake wengine, kitendo cha mimi kufikishwa sebleni kikamfanya mzee godwin kusimama kwa haraka na kuichoma kiunoni bastola yake na kukoki kabla hajanipiga risasi manka akamzuia
“baba, unataka ufanye nini?”
“acha nimuue mshenzi mkubwa huyu”
“baba ninakuomba,usimuue edd……”
Mzee godwin akamtandika manka kibao kilicho muangusha chini manka,akaninyooshea bastola huku akiwa amenilenga kichwani
“najua unataka kunai,ila ninakuomba nizungumze kitu kimoja”
Nizungumza kwa sauti ya upole sana
“nampenda sana mama yangu, yeye ndio kila kitu kwangu.Ninakuomba nitakapo kufa usimsumbue, najua kulea mtoto ambaye si wako ni kazi kubwa na mbaya zaidi ulikuwa unajua kama ni wako”
“nipo tayari kufa, ila ninakufa kwa ajili ya mama yangu.Please dady don’t hurt my mother”(……….Tafadhali baba ninakuomba usimuumize mama yangu)
Nilizungumza huku machozi yakinimwagika, sikuwa na ujanja wowote kwani sikujua ni jinsi gani ninaweza kujiokoa kutoka mikononi mwa mzee godwin
“ila kumbuka baba, kumbuka baba yangu ni ndugu yako wa damu.Damu yake ni damu yako,iweje leo mimi niwe adui yako,iweje leo niwe kitu cha chuki,iweje leo mama yangu awe adui yako.Kumbuka alikuuinua kiuchumi.Kumbuka alikugharamia na kukutibu tatizo lako, ila vyote umeona hakuna kitu”
Nilizidi kuzungumza huku machozi yakiendelea kunimwangika, taratibu nikapiga magoti chini kisha nikainyoosha mikono yangu juu
“unaweza kuniua ukihitaji”
Nilizungumza huku nikimtazama mzee godwin usoni, hakuonekana hata kuwa na lepe la huruma kwenye macho yake.Macho yangu nikayahamishia kwenye bastola yake na kukiangalia kidole chake kilicho ingia kwenye traiga kikianza kurudi nyuma taratibu,gafla milipuko mkubwa nje ukasikika na kuwafanya watu wote tuliopo sebleni kulala chini.Risasi nyingi kutoka njee zikaanza kushambulia mlango wa kuingilia na kunifanya nitambae kutafuta sehemu ya kujificha nyuma ya soma ambalo halikubana ukutani.Watu wa mzee godwin wakaanza kujipanga ndani na kuanza kujibu mashambulizi ya watu wanao fyatu risasi nje.
“eddy”
Nilisikia sauti ya chini ikiniita pembeni yangu,nikatazama na kukutana na msichana aliye nifungualia mlango na kutoroka jana.
“nifwate”
Nikatambaa kuelekea sehemu ambayo yupo pasipo watu wengine wote kuona kwani macho yao yote wameyaelekezea nje sehemu ambapo risasi zinatokea.Tukanyanyuka sote na kuanza kukimbia huku nikimfwata kwa nyuma.Tukazunguka hadi mbele ambapo risasi zinapigwa.Nikashangaa kukuta bunduki kubwa yenye kutumia risasi zilizo kwenye mkanda ikizipiga mlangoni huku sehemu yenye traiga ikiwa imefungwa na mpira,jambo linalo wazubaisha mzee godwin na watu wake wakidhania wanashambuliwa na maadui
“usishangae mimi ndio nimefanya hivyo”
Alizungumza huku akinistua,akanirushia funguo za gari langu ambalo kidogo limebonyea sehemu za pembeni.Nikaingia ndani ya gari na kuichomeka funguo sehemu yake na kuliwasha, nikashusha pumzi na kumshukuru mungu baada ya gari kuwaka bila ya matatizo.Ili nisitumie nguvu sana nikaibadilisha mfumo wa kuendesha na kuweka ‘automatic’ na kuliondosha kwa kasi katika eneo la jumba hili
“asante dada”
“na wewe pia asante”
Sikujua asante yangu inatokana na nini, akawa na kazi ya kunielekeza njia za kupita na kusema kweli si rahisi sana kwa watu kugundua sehemu lilipo jumba la mzee godwin kwa maana lipo kwenye mlima mkubwa ulio jaa miti mingi na hapana nyumba ya mwananchi wa aina yoyote ambaye yupo kwenye huu mlima.
Nikaendele kuliendesha gari kwa umakini huku mara kwa mara nikitazama kupitia kioo cha pembeni kama kuna gari zinanifwata ila sikuona gari lolote
“nilijaribu kuliwasha hili gari lako ila nikashindwa”
“hili gari si rahisi kwa mtu kuliiba kwani namba za siri ninazijua mimi mwenyewe”
“mimi ninaitwa dorecy”
“ninashukuru kukufahamu”
“kunja kusoto kwani mbele kuna geti na kuna watu ninaamini watakuwa wanatusubiria”
Nikakanyaga breki kidogo na kukunja kushoto nilipo elekezwa na kuiacha njia ambayo niyakunyoosha,
“huku twende taratibu taratibu kwa maana kuna kona nyingi sana”
“sawa”
Nika ninakwenda kwa mwendo wa kawaida ambao hata nikikutana na kona ya gafla niweze kukunja isitoshe sehemu ya upane wa pili wa barabara kuna korongo kubwa kwenda chini na laiti kama mtu unaanguka ni lazima ukafie chini huko kwani kuna mimawe mingi iliyo chongoka.
“eddy simamisha gari”
Nikafanaya kama dorecy alivyo niambia, akachomoa bastoa mbili kwenye mifuko ya suruali yake nyeusi aliyo ivaa na kunikabidhi moja.
“unaweza kutumia?”
“ndio”
Macho yate yakawa na kazi ya kutazama sehemu za juu kwenye milima ambayo kwa chini tunapita na gari.
“endesha taratibu”
Nikafanya kama dorecy anavyo niagiza,gafla tukaiona gari moja mbele yetu, aina ya pick up ikiwa na watu wenye bunduki zao huku mmoja wao akiwa ameshika bomo aina ya rocket ambalo upigaji wake analiweka begani na kulifyatulia.Sote tukafunga breki za magari yetu na majamaa wakaanza kushuka huku mwenye bomo akiwa ametuelekezea kwetu akijiandaa kutufyatulia

 ITAENDELEA….Usikose kufuatilia hapa hapa mbukuzihuru.com.  Pia unaweza kupata riwaya hiyo yote,SHE IS MY WIFE na SEX DEALER kwa bei nafuu tu, whatssap no. 0753503331.

Advertisements