Mahakama kuu ya Dar es salaam Aprili 5, 2018 itaanza kusikiliza kesi ya madai ya chama cha ACT Wazalendo dhidi ya jeshi la polisi

Tarifa iiliyotolewa jana na Afisa Habari wa ACT Wazalendo, Abdallah Khamisi ilisema kuwa kesi hiyo itasikilizwa chini ya Majaji watatu, Jaji Ferdinand Wambari, Jaji Sameja na Jaji Rose Teemba.
“Machi 18 tulizungumza na umma juu ya hali mbaya ya nchi Kiuchumi, na tukaeleza hatua ambazo kama chama tutachukua katika kutatua masuala kadhaa ya kinchi.
“Kwenye eneo la DEMOKRASIA tulieleza kuwa tumefungua Kesi ya Madai Na. 8/2018 Mahakama Kuu hapa Dar Es Salaam, kulishtaki Jeshi la Polisi, kutokana na Jeshi hilo kuingilia, visivyo halali shughuli za ziara yetu ya kuhamasisha maendeleo katika Kata tunazoziongoza.

“Leo Mahakama imeipangia tarehe kesi husika, itasikilizwa kwa mara ya kwanza, Aprili 5, 2018 chini ya Majaji watatu, Jaji Ferdinand Wambari, Jaji Sameja na Jaji Rose Teemba.”- Ilisema taarifa hiyo

Advertisements