Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa
Ilipoishia….
Nikapata matumaini ya uwepo wake na moja kwa moja nikaufungua mlango wake na sikuamini macho yangu baada ya kumkuta akiwa ananyonyana denda na mwanaume mwengine ambaye kwa haraka nikamtambua ni derick mume wa madam mery

Endelea…
Sheila akastuka sana kuniona nikiwa nimesimama mbele yao,hata derick ambaye mimi na yeye ni maadui kama paka na paya akakastuka sana na wakaachiana.Macho yangu kwa hataka nikayazungusha katika enoe la chini kutafuta kitu kizuri ambacho ninaweza kupambana nacho ila sikuona.Nikatazama nje nikaona kupande cha mbao kilicho chongonga vizuri na kina unene mkubwa kiasi.

Nikakifwata kwa haraka na kurudi ndani na kumkumba derick ambaye alikuwa anakimbilia kuufunga mlango kwa ndani,akaanguka vibaya na kunipa nafasi ya kuanza kumshambulia kwa haraka.Kwa nguvu zangu zote nikakitulisha kipande cha mbao kwenye magoti yake na kumfanya anguke chini    akitoa ukulele wa maumivu makali.
Sheila akaanza kubabaika kwani siku zote ananijua nikiwa na hasira ninakuwa ziadi ya  mnyama mkali,kwa kutumia kigoti ya mguu wa kulia nikakitulisha kwenye kidevu cha derick na kumfanya arushwe juu kidogo huku meno kadhaa yakidondoka sakafuni
“eddy utamuua…..”
“wewe malaya funga bakuli lako”
Derick akajaribu kurusha teke,nikalidaka huku nikimtazama kwa hasira.Nikamsukuma na akajigonga kwenye kabati lenye tv na redio kubwa.Derick akaanza kutokwa na machozi akijaribu kuniomba msamaha ila sikumuelewa kabisa kwa kitu anacho niambia.
Kwa kutumia gongo nikaanza kumshambulia kwenye miguu yake,nikitumia nguvu zangu zote kuiamiza kwa kipande cha mbao na kuzidi kumpa maumivu derick.Sheila akanidandia mgongoni akijaribu kunizuia,nikageuka na kumshika sheila kichwa chake na kumtazama kwa macho makali.Nikampiga kichwa kichwa cha uso na kumfamya ayumbe kama tiara,nikampiga buti nililo muangushia kwenye sofa na kuanza kulia kwa maumivu kalali.
Nilipo hakikisha miguu ya derick haifanyi kazi yoyote,nikaingia jikoni na kuchukua kishoka cha kukatia nyama chenye makali,kabla sijatoka nikaona kamba ikiwa kwenye mfuko.Nikavichukua kwa pamoja na kutoka sebleni na kumuona derick akijiburuza akijaribu kwenda nje huku akilia.Nikaishika miguu yake na kumburuza hadi alipo sheila,
“eddy mpezi wangu,nakuomba unisamehe….Nisikilize nakuomba”
Sikuwa na haja ya kumsikiliza sheila,nikamshika sheila kichwa chake na nikachukua vipande vya vitambaa vya masofa na kumkandamiza navyo mdomoni na kumfanya ahangaike agaike,nikamfunga kwenye mikono na miguu.Derick wakati wote anakoroma kwa kulia na maumivu.Nikatoka nje na kulifunga geti na kurudi ndani na kuufunga mlango wa kuingilia
“sheila naamini mimi kwako si wakusimuliwa,ninaroho ya binadamu na shetani…..Leo nahitaji unijue mimi ni nani?”
Nilizungumza kwa hasira na sauti nzito iliyo jaa mikwaruzo mingi.Nikamshika derick mkono wake wa kulia,kumbukumbu ya mwanangu alivyompiga chini ikapita kwa haraka kichwani kwangu,nikanyang’ata meno yangu kwa hasira.Nikachukua kishoka na vidole vya derick nikavilaza sakafuni huku nikivikandamiza kwa kutumia mkono wangu wa kushoto
“no…Usinifa…….”
Nishoka kikatua kwenye vidole vyake na kuvitawanyisha kwenye sakafu,dericka akatoa ukulele mkali ila nikamzaba ngumi ya shavu na akabaki akigugumia.Sheila akabaki akiwa ameyatoa macho kama amepigwa mshale wa mgongo.Nikavikunyanya vidole vyake vyote na nikaviweka kwenye meza ya kioo.
“derick leo utakufa kifo cha taratibu kama mwanangu ulivyo mfanya.”
Nikavua tisheti niliyo ivaa,nikaingia jikoni na kuchukua sahani na kurudi nayo ndani sebleni.Nikamfunga derick akamba za miguu,nikamsokomeza vitambaa na yeye kwenye mdomo.Nikauchukua mkono wake wa kushoto ulio na vidole vyake kamili.
Nikamtazama machoni kwa macho ya dharau,kisha nikaupitisha katikati ya miguu yangu na akabaki akinitazama,nikaizungusha miguu yangu na kuusababisha mkono kutoa mlio wa kuvunjika mifupa iliyopo kwenye mkono wake.Dericka akaendelea kulia huku akigaragara chini.Nikaibaeba sahani yenye vidole hadi jikoni,nikaweka kikaangio kwenye jiko la gesi na kuliwasha,nikamimina mafuta mengi ya kula kisha nikavidumbukiza vidole vyote kwenye kikaangio na kuongeza moto ili viive haraka na kurusi sebleni.
Sheila akanitazama huku machozi yakimwagika,mlio wa simu kutoka kweney mfuko wa suruali ya derick ukaanza kusikika.Nikaitoa simu yake ikiita na kukuta ni madam mery ndio anapiga simu kwani imeandikwa ‘wife’ na pembeni kuna picha yake.Nikamtazama sheila na kumfwata,nikamshika nywele za kichwa chake.
“sikia wewe malaya,zungumza na huyu mjinga mwenzako.Jitambulishe kuwa wewe ni mke mwenzake sawa?”
Sheila akatingisha kichwa,simu ikakata na baada ya muda ikaanza kuita tena,nikamtoa sheila vitambaa mdomoni.
“zungumza naye”
Nikaminya kitufe cha kupokea na kuiweka simu iwe kwa sauti kubwa(laudspeker) na kuisikia sauti ya madam mery ikaanza kuzungumza
“haloo mume wangu”
“wewe mshenzi nimekuambia achana na mpenzi wangu.”
“kwani wewe ni nani na namba ya mume wangu umeipataje?”
“ hadi hapo ujaelewa tuu,mimi ni mke mwezio”
“jamani kwa nini uanifanyia hivyo wewe dada kumbe wewe ndio umeficha mume wangu wiki nzima harudi nyumbana”
“mjini hapa”
Nikaikata simu na kuizima huku nikijiuliza maswali ni kwanini madam mery aliamua kurudia na mume wake baada ya tukio la kuuawa kwa mwanangu
“na yeye lazima afe”
Nilizungumza kwa sauti ya hasira huku nikimtazama sheila,nikamdumbukiza tena sheila vitambaa vya mdomoni.Nikakimbilia jikoni na kukuta vidole vya derick vikiungulia kwenye mafuta,nikazima jiko na kuvitoa kwenye vikaangio na kuviweka kwenye sahani,nikaona nyanya mbili juu ya friji,nikazikataka kata vizuri na kurudi sebleni nikiwa nimeishika sahani,nikaviweka juu ya meza na kumgeuza derick aliye lala kifudi fudi akiugulia maumivu.
“derick nimekukangia miskaki iliyonona,karibu ule”
Derick akanitazama kwa macho ya hasira,nikamuitamia na kuvitoa vitambaa mdomoni mwake kisha nikachukua kidole kimoja na kukikandamiza mdomoni mwake,gafla akanitemea kidole usoni na kuzidi kunipandisha hasira na nikaanza kumshindilia ngumi za pua hadi ikatepereka na kumwaga damu nyingi.
Nikajibwaga kwenye sofa huku nikimtazama derick nikifikiria nini cha kumfanya ili apate uchungu kama nilio upata mimi kipindi alipo muua mwanangu.Nikapata wazo ambalo likanifanya nisimame na kumburuza derick hadi nje kisha nikarudi ndani na kumchukua sheila na kumbeba begani,nikafungua mlango wa gari na kumuingiza upande wa dereva huku mikono na miguu yake nikiwa bado nimeifunga kwa kamba.Nikaaingia ndani na kuchukua kishoka changu na kurudi nje nikamchukua derick na kumlaza chini ya gari,nikaingia ndani ya gari na kuifungua mikono ya sheila.
“washa gari lako”
Nilizungumza huku kishoka nikiwa nimekiweka kwenye shingo yake.Sheila akaanza kutetemeka na akafanya kama nilivyo muagiza
“endesha gari lako umkanyage huyo mwehu wako”
Sheila akatingisha kichwa,akiashiria kukataa.Nikamtoa vitambaa ambavyo nilimsokomeza mdomoni
“endesha gari”
“huoni tutamuua”
Nikamzaba sheila kofi la shavu,na kumfanya kuweweseka na akakanyaga mafuta na gari ikasogea mbele na kupanda kwenye mwili wa derick kama imepata kwenye matuta yaliyo tengenezwa barabarani.Nikashuka kwenye gari na kumkuta derick akiwa yupo katika hali mbaya,kwa kutumia kishoka changu nikamkata derick kichwa chake na kukirusha ndani ya gari alipo sheila na kumfaya akarupuke kwa woga
“sheila sali sala yako ya mwisho,unamfwata mwehu wako kuzimu”
Nilizungumza kwa sauti nzito isiyo na huruma hata kidogo…

 *****sory madam*****(44)

….“eddy ni nini  kimekupata unakuwa naroho mbaya kiasi hicho”
Sheila alizungumza kwa woga huku akitetemeka,nikapiga hatua za taratibu hadi sehemu aliyo simama pembezoni mwa gari,
“wewe ni mtu wa kunisaliti mimi?”
Swali langu likamfanya sheila kutingisha kichwani,nikamshika mkono na kuanza kumburuza hadi tukaingia ndani na kumsukumia kwenye sofa
“eddy,kumbuka mimi na wewe tumetoka mbali……..Nilikuwa nipo radhi kufa kwa ajili yako.Leo hii huioni dhamani yangu kwanini lakini eddy”
Sheila alizungumza huku akiendelea kumwagikwa na machozi mengi,hasiri ikazidi kunipanda kila nilipo kumbuka tukio la wao kukumbatia na derick.
“eddy mimi nilijua kuwa wewe umeniacha,tazama nilikuokoa kwenye ndege nikawa nipo tayari mimi kufa ili wewe upone,ila hata siku moja sijakuona hospitalini.Niliiungua kwa ajili yako wewe.Ila dhamani yangu ipo wapi au kwa sababu mimi ni mwanamke ndio unaamua kuninyanyasa?”
Sheila alizidi kuzungumza kwa uchungu na kunifanya niwe kimya nikimtazama huku asira ikinishuka
“eddy nipo tayari kufa,nichinje kama ulivyo mchinja derick,nichinje”
Sheila alinamisha kichwa chake mbele ya miguu yangu na kujikuta nikikinyanyua kishoka changu juu kwa hasira machozi yakinimwagika taratibu
“eddy ,najua nitakwenda kuzimu kwa maana nimekukosea sana.Ila sistahili kuendelea kuishi mip tayari uniue.”
Nikakitupa kishoka kwa nguvu kwenye meza ya kioo hadi meza ikavunjika.Taratibu nikakaa chini huku nikimwagikwa na machozi,sheila akainyanyua sura yake iliyo lowana machozi na kuniangalia kwa uchungu.
“eddy kwa nini umeua,ulishwa kutuambia kiustarabu”
Kiganja cha mkono wangu wa kulia kwa haraka kikatua shingoni mwa sheila na kuanza kuibana kwa nguvu,mikono ya sheila ikawa na kazi ya kuuzuia mkono wangu usiendelee kuibana shingo yake
“unamajua derick vizuri wewe?”
“mm..Mmmmmmmm…..?”
Nikaiachia shingo ya sheila na kumfanya asogee mbali kidogo na nilipo mimi.Ukimya ukatawala kati yetu huku ikisikika mihemo yangu ya hasira jinsi inavyo panda na kushuka.
“eddy ninakupenda sana,tena sana.Maishani mwangu nilikuambia kuwa sijawahi kupenda mwanaume yoyote kama wewe.Umenifundisha mengi eddy,upendo,ujasiri,huruma……Ila mimi sio kosa langu kuwa na derick”
“ila?”
“derick mimi alinisaidia sana kipindi nipo kenya,sikuwa na mtu wa kunilipia hata pesa ya hospitali ambayo nilikuwa ninatibiwa.Aliweza kunihudumia kwa kila jambo,alininunulia dawa za gharama kuwa zilizo nisaidia ngozi yangu kurudi katika hali ya kawaida kama awali.Nilikuwa nimebabuka mwili mzima mimi,nilikuwa sitamaniki na……”
“ukaamua kumpa mwili wako?”
“sio kama niliamua kumpa mwili wangu,aliweza kunishawishi na wewe sikujua ni wapi ulipo.Nilijariu kukuulizia shule ambayo ulikuwa unasoma ila sikupata jibu”
Nikaachia tabasamu la dharau lililo jaa hasira nzito inayo ifanya royo yangu kutamani niyanyofoe masikio ya sheila,nikawa ninajikaza nisifanye kitu ninacho kiwaza.
“tangu tupoteane,imepita kipindi gani?”
“miezi mitatu”
“ulishindwa kuzizuia hisia zako hadi utakapo niona?”
Sheila akaa kimya huku macho yake akiyakwepesha kukutana na macho yangu yalio jaa ukali kama chui aliye jeruhiwa mwili wake kwa risasi.
“dawa yako ipo jikoni”
Nilizungumza huku nikinyanyuka na kwenda njee,nikauvuta mwili wa derick na kuutoa chini ya gari,nikaurudi ndani na kumkuta sheila akiwa amejinamia chini akilia
“funguo ya handaki lako iko wapi?”
“ndani?”
“wapi?”
“kwenye dreasing table yangu”
Nikamtazama sheila kwa muda,nikafunga mlango wa kutokea nje kwa funguo zilizokuwa zikining’inia ndani ila kumfanya sheila asikimbie kwenda sehemu yoyote.Nikaingia chumbani kwake na kuiona rimoti ndogoi iliyopo juu ya kakabati kake kadogo kalicho jaa vipodozi.Nikaichukua kabla sijaondoka kwa bahati mbaya nikaangusha kichupa cha mafuta,nikakiokota na kukirudisha juu sehemu kilipo kuwa ambapo chini yake kuna karatasi iliyo geuzwa upande wa pili ambao hauna maandishi yoyote,nikaichukua karatasi na kuigeuza upande wa pili.
Nikaanza kusoma maandishi yaliyo andikwa kwa muandiko wa kulala na juu yake kuna jina la hospitali ambayo dokta huyo ndio ameandika vipimo vilivyo anza kuufanya mwili wangu kurudi katika hali ya hasira kali.Vipimo alivyo viandika daktari vinaonyesha sheila ni mjamzito wa mimba ya wiki mbili na kwa pembeni yake baba wa mtoto ni derick malki
“anamimba ya derick….?”
Nilijiuliza swali ambalo jibu lake ninalo kichwani,nikiwa ninaendelea kuitazama karatasi yangu ni kama mungu aliye niambia nitazame kwenye kioo,nikauona mkono wa sheila akiwa ameunyanyua juu huku akiwa ameshika kishoka nilicho kuwa nacho mimi.
Nikakikwepa na kuruka pembeni,sheila akakirusha kishoka,nikainama na kikanikosa na kutua kitandani.Kama gari iliyo poteza breki zake,nikajirusha na kwakutumia bega langu la mkono wa kulia,likatua tumboni mwa sheila na sote tukaanguka chini,sheila akaanza kutoa kilio cha maumivu.Nikainyanyua ngumi yangu na kushusha kwa kasi na kabla haijafika usoni mwake nikaisimamisha na kumtazama jinsi alivyo fumba macho akiogopa mzigo utakao shuka kwenye uso wake
“unataka kuniua wewe malaya si ndio?”
Sheila hakunijibu chochote zaidi ya kuwa kimya.Nikampiga vibao vinne vya mashavu ili kuiweka akili yake sawa.
“upendo wangu kwako usije ukageuka ukawa kifo chako,sheila….Nimezaliwa siku moja nia nitakufa siku moja,hakuna kama mimi eddy na hatotokea kama mimi.Pumbavu”
Nikamalizia na kibao cha tano kilicho mfanya azidi kuwagikwa na machozi.Nikamnyanyua na kumuweka begani nikakichukua kishoka changu na tukatoka nje.Nikambwaga kwenye sofa kama zigo wa kuni na kabla sijatoka nje sheila akaniita
“nini?”
“naomba unisamehe,haikuwa akili zangu”
“zilikuwa akili za nani?”
“ni shetani amenipitia,nikatamani kukuua”
Sheila alizungumza huku akiwa amejishika tumbo lake.
“sheila mimi sina roho mbaya,ila inapobidi niwe na roho mbaya itakuwa.Mimi siwezi kumuua mtoto wa derick uliye naye tumboni kama yeye alivyo fanya kwa mwanangu”
Sheila akakosa la kuzungumza na mimi,nikaufungua mlango na nikatoka nje,kwa kutumia kirimoti nikaufungua mlango wa handaki na kisha nikabeba mwili wa derick hadi ndani.Nikarudi juu na kuchukua kicha chake na kuingia nacho ndani.Nikalichunguza handaki na kugundua lina majiko mengi ya umeme ambayo yana sehemu ya kuwokea mikate.Nikaisogeza meza kubwa iliyipo pembeni yangu na nikauweka mwili wa derick juu
“eddy”
Sauti ya sheila ikanifanya nimgeukie,akainisogelea karibu na kunishika mkono wenye kishoka
“hii roho ya kikatili umeitoa wapi?”
“kwenye kazi zangu huwa sihitaji kuingiliwa,ondoka kabla sijafanya maamuzi mabaya kwako”
“eddy,mimi ndio nilikuwa ninakupunguza hasira zako.Hakuna mwanamke ambaye aliweza kufanya hivyo kama si mimi au mama yako”
“mama anakutaka uende nyumbani,amekutafuta kwa kipindi pasipo mafanikio yoyote.Nakuomba twende sote kwa mama leo”
Nikayatazama macho ya sheila na kuyaona yanamaanisha kitu anacho kizungumza.
“rudi ndani?”
“unataka kuufanya  nini huo mwili?”
“rudi ndani usiniulize chochote”
Sheila taratibu akasogea pembeni yangu.Pasipo kuwa na haruma nikaanza kuucharanga kwa kishoka mwili wa derick,nikaufanya mwili wa derick kuwa katika vipande vipande.Nikaliwasha jiko kubwa lenye visahani vinne vya kupikia.Nikaviingiza vipande vya mwili wa derick.
“mungu ninaomba unisamehe katika hili”
Niliomba sala ya msamaha kwa mungu wangu,nikaifanya kazi yangu ya kuvikausha vipande vya mwili wa derick hadi nikamalizia na kichwa chake kwa kukipasua.Nikaviweka kwenye turubai kubwa la kufunikia gari la sheila kisha nikatoka nje,nikamkuta sheila kusafisha sehemu zote zenye damu.Macho ya sheila yamevimba kidogo kwa kulia huku mashavu yake yakiwa na alama za vidole vyangu
“eddy,hii ni siri kati yangu mimi na wewe.”
“ukiitoa nikufanye nini?”
“nifanye chochote upendacho”
“sawa”
Tukasaidia kufamya usafi,nilipo hakikisha hakuna uchafu wa ina yoyote tukarudi ndani na sheila akawa wa kanza kuoga kisha nikafwatia na mimi,nikavaa suruali ya sheila ambayo inanitosha na tisheti yake hii ni kutokana na kutokuwa na nguo.Mida ya saa mbili usiku tukafunga safari hadi nyumbani kwa mama,sheila akapiga honi na geti la nyumba likafungulia na akaingiza gari hadi sehemu ambayo kuna magari yetu mengine.Nikashuka ndani ya gari ila sheila akaniomba atangulie.Akaufungua mlango na kuanza kumuita mama ambaye niliisikia sauti yake akiitika.
“ohoo karibu mwanangu”
Nikawachungulia ndani na kumuona sheila akikumbatiana na mama.Nikaingia na kumfanya mama kunishangaa kwa muda huku akionekana kama kuto amini kwa kile anacho kiona mbele yake.Kwa furaha mama akanikumbatia na sote machozi yakaanza kunimwagika.Mama akanikaribisha ndani huku akiwa na furaha kubwa
“mwanangu eddy ndio umevaa nini?”
Mama alinitazama kuanzia juu hadi chini na kumfanya sheila kucheka
“nimempisha pamba zangu zimemtoa chikopa kama nini?”
“mwanangu ungekuwa mwanamke ungevutia kama nini”
“mama…..!!”
“ndio….Ila ndio hivyo umezaliwa dume la mbegu”
Mama akatukaribisha mezani na kutakapa chakula cha usiku.Kutokana na mawazo mengi sikuweza kuzungumza sana na mama.Nikapanda gorofani kulala,nikajitupa kitandani ila usingizi haukunichukua kabisa.Tukio la uuwaji wangu wa kikatilii ulianza kunisumbua sana akilini mwangu.Taswira ya madam mery ikaanza kukisumbua kichwa changu,nikanyanyuka na kwenda cumbani kwa mama.Niifungua droo yake ambayo anahifadhia astola yeke.Kwa bahati nzuri nikaikuta.
Nikaitazama na kuikuta na risasi za kutosha,nikafungua droo nyingine na kukuta pesa za kutosha,nikachukua kibunda kimoja na sikujua idadi ya pesa iliyopo.Nikashusha pumzi vya kutosha,nikatoka chumbani kwa mama nikiwa ninakatiza kwenye kordo nikirudi  chumbani kwangu nikayasikia mzungumzo ya mama na sheila
“wee unataka kuniambia kuwa mwangu amekuwa na roho mbaya kiasi hicho?”
“ndio mama,mbele ya macho yangu amemuua mwanaume mmoja ambaye anadai kuwa alimuulia mtoto wake”
“mtoto?”
“ndio mtoto ila sijajua huyo mtoto amezaa na mwanamke gani?”
“ina maana eddy alikuwa na manamke mwengine zaidi yako?”
“ndio mama,imeniuma sana mama yangu”
“ila mama chonde chonde ninakuomba usimuambie eddy chochote kwa maana,amekuwa kama mtu aliye changanyikiwa”
“nani kachanganyikiwa”
Nilishindwa kuvumilia ikanibudi nizungumze,taratibu nikiwa ninashuka kwenye ngazi na mkononi nikiwa nimeshika bastola na kuwafanya mama na sheila kustuka…..
ITAENDELEA….Usikose kufuatilia hapa hapa mbukuzihuru.com.  Pia unaweza kupata riwaya hiyo yote,SHE IS MY WIFE na SEX DEALER kwa bei nafuu tu, whatssap no. 0753503331.