MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA

ILIPOISHIA
Wapelelezi waliopo nje ya chumba hicho walizidi kuyafwatilia mazungumzo hayo kwa vinasa sauti walivyo weza kuvifunga ndani ya chumba hicho.
“Siwezi kumfahamu mtu gaidi kama wewe. Niambieni ni nini alicho kuambia baba yangu Eddy”
Shamsa alizungumza kwa hasira huku akimwagikwa na machozi, Briton kwa dharau akatabasamu kisha akajivuta kidogo kwenye kiti na kumtazama usoni Shamsa
“Baba……..baba gaidi kama Eddy. Ohoooo mimi ndio niliye weza kumuua, sahamani kwa hilo”
Shamsa akasimama kwa hasira na kumrukia Briton na wote wakaanguka chini na kuanaza kumshindilia ngumi za hasira Briton aliye fungwa pingu miguuni na mikononi.
 
ENDELEA
Wapeleezi wawili wa kike wakaingia ndani ya chumba hicho na kumtoa Shamsa juu ya mwili wa Briton anaye zidi kupigika na binti huyo. Ikawalazimu kumtoa kabisa nje ya chumba hicho na kumpeleka katika chumba chake walicho mpatia na chenye ulinzi mkali sana.
“Mwanangu mbona umekuwa hivyo?”
Mama Pudensia alizungumza huku akimtazama Shamsa machoni anaye mwagikwa na machozi akionekana dhahiri kwamba ana hasira kali iliyo mpanda, kwani kifua chake kiliweza kutanuka kiasi, mishipa yake ya shingo inaoenekana vizuri, uzuri wa sura yake umebadilika sana.
Mambo yote yakiwa yanaendelea, Bwana Mgwira aliweza kushuhudia tukio hilo akiwa katika chumba cha kusikilizia mazungumzo yaliyo kuwa yanafanywa kwenye chumba hicho.
‘Hakikisha hii siku haipiti lazima awe amesha kufa’
Bwana Mgira alimtumia meseji mmoja wa wapelelezi alio kuwa nao ndani ya chumba hicho kisha yeye akatoka na kuondoka zake.
                                                                                                        ***
   Kitu kilicho zidi kumuumiza kichwa Raisi Praygod ni wapi alipo Eddy, ambaye wananchi wengi wote wanafahamu kiongozi huyo amefariki. Anashindwa hata kuwatangazia wananchi kwamba Eddy ndio amehusika na vifo vya wanajeshi hao.
“Sasa hapatunafanyaje?”
Raisi Praygod alimuuliza mshauri wake bwana Mgwira, wakiwa ndani ya ofisi ya yake.
“Muheshimiwa hapo kusema kweli hatuwezi kufanya chochote zaidi ya kumtafuta kimya kimya, pasipo wananchi kuweza kulitambua hilo. Pia itakuwa ni nafasi ya kipekee kuweza kumuua, pasipo watu wengine kuelewa”
“Etieee?”
“Ndio muheshimiwa, kwa maana wananchi wanajua kwamba amekufa. Tunacho kifanya mwili wa yule mshenzi kule Muhimbili, unazikwa na jeshi kwa madai kwamba ni gaidi, hakuna muandishi wa habari atakaye karibia jeneza na kuipiga picha sura ya Eddy”
“Lakini tukiwabana waandishi wa habari wasifanya kazi yao, kunaweza kuzuka mambo ya kitata. Tuwape nafasi tuone itakavyo kuwa”
“Sawa muheshimiwa. Tuachane na hayo, vipi uchaguzi ndio mwaka huu, umejipangaje kaka”
“Kama kawaidia, miaka mitano ijayo ipo mikononi mwangu”
Raisi Praygod alizungumza kwa kujiamini, kwani anatambua kwamba wananchi wengi wa Tanzania wanamchukulia kwama kiongozi imara na sahihi katika maisha yao, ila nyuma ya pazia ni kiongozi katili asiye paswa kushikilia hata hiyo miaka mitano ya awamu ya pili.
                                                                                                   ***
“Priscar twende kule kwenye handaki”
“Sawa mdama”
Priscar akazidi kujikaza kuliendesha gai hilo, kwani wote wawili kila mmoja ana uchungu wake kwa upande wake, yeye anamlilia Samson, ila bosi wake anamlilia Eddy. Kwa mwendao wa lisaa moja na nusu wakawa wamefanikiwa kufika kwenye handaki ambalo ndipo yalipo kuwa maficho ya Rahab na kikundi cha wezake walio kuwa wakidili na maswala ya ujambazi, wa kuua watu kazi hiyo ikiwa ni amri kutoka kwa raisi Praygod wao wakiifanya pasipo kujua kwamba ni kazi ya kiserikali,
Wakashuka wote wawili, huku Rahab akionekana kuwa na Shahuku kubwa ya kutaka kwenda kumuona Eddy akiwa ndani ya handaki hilo.
Wakafika ndani, hapakuwa na mtu wa aina yoyote, Rahab akafungua kila chumba kuhakikisha kwamba ni kweli hakuna mtu, ila ndivyo jinsi macho yake yalivyo weza kushuhudia kwamba hakuna mtu wa aina yoyote katika handaki hilo, akarudi eneo la sebleni akiwa amechoka, akamkuta Priscar akiwa ameshika karatasi nyeupe akiwa anasoma yaliyo andikwa humo ndani huku machozi yakimwagika, alipo maliza taratibu akamkabidhi Rahab aweze kuisoma karatasi hiyo.
{Madam R. Samahani sana kwa kile kilicho weza kujitokeza zidi ya wanajeshi hao, sikuwa na jinsi zaidi ya kuweza kuwaangamiza ili wasiweze kumdhuru mwanaume unaye mpenda kwa dhati.
Rahab natambu ya kwamba mapenzi yanauma sana pale unapo mkosa yule umpendaye, ndivyo jinsi hata wanafamilia wa wanajeshi nilio waua, ndivyo wanavyo umia kwa sasa. Madama, asante sana kwa kuweza kunipa nafasi ya pili ya kuweza kuishi, ila nikiwa kama si binadamu wa kawaidi, hali hii inadhidi kunidhuru siku hadi siku pale ninapo mwaga damu za watu, huwa natamani kila muda na kila mara niweze kumwaga damu za watu, natambua maamuzi ninayo yachukua ni magumu sana ten asana.
Ningependa niyachukue mimi kama mimi mwenyewe na nisimshirikishe mtu yoyote. Nitakufa kwa ajili ya kuto ua zaidi kwani kila nikiua ndivyo jinsi ninavyo zidi kupata nguvu, za kuendelea kuua. Namuacha Eddy ndani ya handaki hili ukija hakikisha hali yake inakuwa salama kwani bila ya hivyo anaweza kufariki muda na saa yoyote. Nakutakia kazi njema. Samson}
Ujumbe huo wa Samson ukazidi kumchanganya Rahab akajikuta akitoka mbio ndani ya handaki hilo na kuanza kuita kwa sauti kubwa huku na huko akiliita jina la Eddy. Milio ya ndega pamoja na upepo unao vuma ndani ya msitu huo havikutosha kuweza kusikia sauiti yoyote ya mtu akiliitikia jina lake. Uchungu mkali ukazidi kumtawala ndani ya moyo wake, akazidi kuita jina la Eddy ila hapakuwa na majibu ya aina yoyote.
Akajaribu kuweza kuvuta hisia, ila picha halisi ambayo inamjia kichwani ni jinsi Samson alivyo weza kuaondoka katika eneo hilo na gari lake, akiwa amefika eneo la barabara kuu, kuna mzee wa makamo alimsimamisha na kumuomba lifti, japo Samson kwa mara ya kwanza aliweza kukataa, ila mzee huyo alijaribu kuweza kumsihi sana kwamba anahitaji lifti. Samson ikambidi kumfungulia mlango mzee huyo mwenye mvi nyingi kichwani mwake, kisha akaondoka naye.
Mwendo kasi wa gari anayo iendesha Samson kukamfanya mzee huyo kuanza kumuomba Samson aweze kupunguza mwendo huo, ila Samson hakuhitaji kuweza kupunguza, zaidi na zaidi ndivyo jinsi alivyo zidi kuongeza mwenda kasi hadi mzee huyo akaanza kumwagikwa na machozi.
Simu ya Samson ikaanza kuita, alipo ona ni jina la Rahab, akaiacha simu hiyo iite hadi ikakatika, ikapigwa tena, ikaita hadi ikakatika, ikapigwa kwa mara kadhaa ila Samon hakuweza kuipokea zaidi alipo ona inampigia kelele, akafungua kioo cha upande alipo kaa mzee huyo, kisha akaitupia kwanye nyasi nyingi zilizopo kandokando ya barabara, kurudisha macho yake barabarani, kufumba na kufumbua gari yake ikagongana uso kwa uso na gari la mafuta, likauburuzwa kwa urefu fulani, huku tanki lake la mafuta likiwa limetoboka na kumwaga mafuta. Mikwaruzo ya ya vyuma vyuma kwenye lami, vikazalisha cheche, zilizo ingia kwenye mafuta ya petrol na kusababisha mlipuko mkubwa, ulio pelekea gari hiyo kurushwa pembeni ya barabara na kuendelea kuteketea kwa moto.
“Am sorry madam” (Samahni bibie)
Yalikuwa ni maneno ya mwisho ya Samson kabla hajafariki kabisa. Kwa hasira Rahab akajikuta akipiga kelele kali, hadi miti ikatingishika, huku ndege wakipupuruka kwa woga wa sauti hiyo ambayo hawakuwahi kuisikia.  Priscar naye akajikuta akianguka chini na kupoteza fahamu, kwani hakuweza kustahimili mtingisho na nguvu ambayo inazunguka ndani ya msitu huo.
***
      Kwa kupitia kifaa maalumu kilichomo ndani ya mwili wa Briton, maeneo ya mgongoni mwake, vijana wanne wa Al-Shabab waliweza kugundua ni jengo gani ambalo Briton yupo. Kila mmoja akiwa na simu yake yenye uwezo ya kuonyesha alama nyekundu sehemu Briton alipo, wakajigawa wawili wawili, kwenda kulisoma jengo hilo kabla hata wajafanya uvamizi majira ya usiku, kwani muda wa sasa ni jioni.
Pasipo kustukiwa wakalichunguza gorofa hilo, walipo hakikisha kwamba ulinzi wa eneo hilo umeimarishwa sana, ikabidi warudi kwenye nyumba ya wageni walipo fikizia kuendelea kupanga mipango yao.
Kila mmoja alihakikisha anajiandaa vizuri, kwani hawakuhitaji zoezi hilo liweze kuwachukua muda mrefu, wakiwa katika kutazama luninga iliyomo ndani ya chumba hicho, wakaona taarifa ikiwaonyesha binti waliye agizwa akiwa kwenye ulinzi mkali wa askari na kuingizwa kwenye gari.
“Watakuwa wamempelea kwapi?”
“Nahisi kwenye kituo kikubwa cha polisi”
“Una uhakika huo?”
“Ndio kwa maana hawezi kupelekwa eneo jengine lolote zaidi ya kuwa katika kituo kikuu cha polisi”
“Basi nyinyi wawili mutaenda katika kituo cha polisi usiku huu, kisha na sisi wa wili tutakwenda kumkomboa bosi”
“Sawa mkuu”
Mipango ya vijana hao wanao jiamini kupita maelezo ikakamilika vizuri majira ya saa mbili usiku wakatoka vijana wana kwenda kwenye kituo cha polisi, wakiwa na lengo la kwenda kuhakikisha kwamba wanatoka na Shamsa, wakiwaancha wezao wanao kwenda kwenye jengo la alilo shikiliwa Briton.
                                                                                                   ***
“Mama Pude”
Shamsa aliita kwa sauti ya unyonge huku akimgeukia mama huyo aliye kaa karibu naye kwenye kitanda.
“Ndio mwanangu”
“Nahitaji kwenda kuzungumza na yule kijana tena”
“Una uhakika huto fanya vurugu tena?”
“Ndio ninauhakika”
“Basi ngoja”
Pudensia akapiga simu kwa mkuu wa upelelezi kumtaarifu kwamba binti huyo anahitaji kwenda kuzungumza na gaidi waliye mkamata. Ofisi nzima kila mmoja akajiweza sawa kuweza kusikiliza mazungumzo yao, kisha Shamsa akaruhusiwa kwenda kwenye chumba cha mahojiano. Shamsa alipo ingia kwenye chumba hicho akasimama mlangoni kwa muda huku akimtazama Briton. Akilini mwake akawa amepata jibu kwamba mtu huyo kuna sehemu amesha wahi kumuona, japo hana uhakika naye sana.
Akatazama kamera za ulinzi zilizomo ndani ya chumba hicho, kisha taratibu akaanza kupiga hatua kuelekea kwenye kiti kilicho wazi, akakaa na kutazamana na Briton aliye mvimbisha maeneo ya jichoni kwa ngumi alizo weza kumpiga.
Shamsa akaazidi kumtazama Briton, kwa umakini, akamtazama sehemu ya kushoto chini kabisa ya shingo yake, hapo ndipo alipo weza kumkumbuka kwamba mtu huyu ndio aliye weza kumsaidia maisha yake kipindi alipo kuwa anaanza kuingia katika kambi ya Al-Shabab.
“Briton……..!!!”
Shamsa aliita kwa sauti ya chini, huku akimtazama Broton, aliye achia tabasamu pana huku akitingisha kichwa akimuashiria kwamba ndio yeye. Shamsa akajikuta machozi yakimwagika, matumaini yake ya kuweza kupata mtu anaye mjali yakaanza kufufuka taratibu moyoni mwake. Wapelelezi wakabaki wakishangaa, kumuona Shamsa analia, kila mmoja akatega sikio lake huku wakitazam kupitia kioo kikubwa kinacho watenganisha na chumba walichopo Shamsa na Briton.
Shamsa akataka kusimama kwenda kumkumbatia ila Briton akawahi kumshika mkono, na kumkonyeza kumzuia asifanye hivyo kwani ni hatari kwake.
“Kwanini lakini umefanya hivyo?”
“Nimekuja kukuchukua turudi nyumbani, Tanzania si kwenu Shamsa”
Shamsa akabaki kimya, Briton akaipeleka mikono yake, iliyo fungwa pingu taratibu usoni mwa Shamsa na kuyafuta machozi yanayo mwagika Shamsa.
“Uliniacha kipindi chote nikiwa ninateseka na kuhangaika, sasa ni muda wa kurudi nyumbani Sh…….”
Kabla hata Briton hajamalizia sentesi yake zaa za jengo zima zikazima, ving’ora vya hatrari vikaanza kulia ndani ya jengo zima, huku milio ya bunduki kutokea nje ikianza kurindima.

 

SORRY MADAM (38) (Destination of my enemies)
Halikuwa ni jambo la kushangaza kwa Briton kwani alitambua muda wowote na saa yoyote ni lazima wezake watakuja kumuokoa katika jengo hilo. Shamsa akasimama wima baada ya mlango wa chumba walichopo kufunguliwa, walinzi watatu walio shikilia tochi, waliingia huku wakihitaji kuweza kuweka ulinzi kwa Briton pamoja na Shamsa, huku walinzi wengine wakiendelea kupambana nje na magaidi walio jipanga vilivyo kwani silaha zao, zina uwezo wa hali ya juu huku wakiwa wamevalia miwani ambazo zinawasiadia kuona usiku vizuri gata kama kuna giza zito.
Kitendo cha mpelelezi mmoja kuweza kumshika Shamsa mkono wake wa kulia, ikawa ni kosa kubwa kwa kijana huyo kwani Shamsa, alijigeuza haraka, kwa kutumia mkono wake wa kulia, akamkaba kabala mpelezi huyo, bila hata ya kumuonea huruma akamvunja shingo.
Kishindo cha mwenzo kuanguka kikawastua wapelelezi wengine ambao wamemuweka kati Briton, wakajaribu kumulika alipo anguka mwenzao, wakakuta Shamsa ananyanyuka huku akiwa amesha ichomoa bastola iliyo kuwa kiunoni mwa mpelelezi huyo.
Risasi kadhaa zikatua vifuani mwa wapelelezi hao, walio simama pembeni ya Briton, kisha kwa haraka Shamsa akamfwata Briton na kumkumbatia kwa nguvu. Wakajikuta wote wawili wakiikutanisha midomo yao na kuanza kupeana mabusu mazito mazito, kuto kujali kwamba wapo kwenye hatari kubwa.
“Tafuta funguo unifungue”
Briton alizungumza huku akimuachia Shamsa, aliye anaza kupekua mifuko ya wapelelezi hao walio ingia mmoja baada ya mwengine. Kwa bahati nzuri akafanikiwa kuipata funguo hiyo kwa mmoja wa wapelelezi wanao endelea kuwamgikwa na damu mwili ni mwake kwa risasi zilizo weza kumpata. Kwa haraka Shamsa akamfungua Briton na kumpa moja ya bunduki aina ya SMG, walio ingia nazo hao wapelelezi.
“Upo vizuri?”
Shamsa alizungumza huku akiwa anatazama mlangoni
“Ndio”
“Tutoke”
Kwa umakini mkubwa wakatembea hadi mlangoni ambapo, Shamsa akachungulia, akashuhudia jinsi wapelezi wakipambana na watu ambao wamewavamia. Bila ya kupoteza muda Shamsa na Brito wakawa na kazi moja ya kuhakikisha kwamba wanatoka ndani ya jengo hilo na kila aliye weza kujipendekeza kwao ni lazima mauti yatamkuta.
                                                                                                      ***
    Pikipiki aina ya boksa ikasimama mbele ya kituo kikuu cha polisi, vijana wawili walio ficha nyuso zao kwa vinyago maalumu, wakashuka wakiwa na bunduki aina ya AK47, pamoja na mabomu ya kurusha kwa mkono(Granade). Shambulizi la kwanza, wakarusha mabomu hayo ya kituo hicho, mlipuko mzito ukatokea ndani ya kituo hicho huku kukisikika kelele za maumivu makali kutoka kwa watu walimo ndani ya kituo hicho.
Mmoja akasimama nje na kuanza kushambulia askari ambao walikuwa nje, mmoja akaingia ndani ya kituo hicho kwa lengo la kwenda kumchukua Shamsa mahali popote alipo fichwa. Askari ambao wengi wamejeruhiwa na bomo hilo wakajikuta wakimaliziwa kwa risasi za gaidi huyo asiye na huruma.
Askari walipo nje wakazidi kupambana na gaidi ambaye amesimama nje ya kituo chao akiwa amejibanza kwenye moja ya gari za polisi. Idadi ya polisi wengine ikazidi kuongezeka kituoni hapo kuongeza nguvu yta ziada. Gaidi aliye ingia ndani ya kituo akaanza kutafuta chumba kimoja baada ya kingine kuangalia kama Shamsa yupo, na endapo anawakuta mahabusu, akawatwanga risasi wote pasipo kuwa na huruma.
Gaidi aliyepo nje ya kituo kwa bahati mbaya, akazidi nguvu na askari na kupigwa risasi nyingi sana mwilini mwake na kupoteza maisha, askari walio jipanga kikamilifu wakaanza kuingia ndani kwa umakini mkubwa huku wakiwa wameshika silaha zao. Gaidi aliyomo ndani ya kituo pasipo kuweza kujua nje tayari mambo yamesha kuwa mabaya, akaendelea kupita chumba kimoja hadi kingine, ofisi moja hadi nyingine kuhakikisha kwamba wanatoka na Shamsa, akiwa anatoka kwenye moja ya ofisi, risasi moja ikampiga kwenye mguu wake ulio kuwa umetangu lia mbele kwenye kupiga hatua ya kutokea ndani ya chumba hicho.
Akarudi ndani huku akiwa analalama kwa maumivu makali, akaichomo magazine yake na kuweka nyingine iliyo jaa risasi, Akachomoa bomu moja lililo salia, alilokuwa amelining’iniza kwenye jaketi la kuzuia risasi. Akalishikilia vizuri kisha akalitupia sehemu ambayo polisi wapo, kamanda mmoja mrefu kwenda juu, alipo liono bomu hilo, hata kabla halijasimama, ili kuachia mlipuko, akalipiga teke na kulirudisha ndani ya chumba lilipo tokea.
Mlipuko mzito ukatokea ndani ya ofisi hiyo na kumuangamiza gaidi huyo, hali ilipo anza kutulia taratibu askari wakaanza kujongea kwenye ofisi hiyo, wakaukuta mwili wa gaidi huyo ukiwa umechakaa kwa mlipuko wa bomu hilo la kurusha kwa mkono.
                                                                                                    ***
   Majira ya saa tano usiku Priscar akastuka, kutoka usingizini na kumkuta Rahab akiwa amekaa pembeni yake. Taraibu akajinyanyua kitandani na kutazama kila mahali ya sehemu walipo ila kidogo kuna tofauti japo amelala juu ya kitanda.
“Madam nipo wapi?”
Rahab akamtazama kwa muda Prisacar anaye endelea kudodosa dodosa ndani ya chumba hicho ili mradi avute kumbukumbu na kutambua kwamba ni wapi alipo, ila hakuweza kutambua ni sehemu gani alipo.
“Upo sehemu salama”
“Hapa ni wapi?”
“Ni ndani ya handaki ambalo uliingia kwa mara ya kwanza ila hakuweza kufika ndani ya chumba chake hata kimoja”
Priscar akatazama saa yake ya mkononi kukuta muda umekwenda sana, kwa haraka akakurupuka na kushuka kitandani akionekana kuchanganyikiwa.
“Madam ikulu……………..!!!!!?”
“Kuna nini?”
“Fanya twende”
Rahab akatabasamu huku akiendelea kumtazama Priscar anaye onekana kuweweseka kwa wenge lililo mjaa.
“Leo haturudi”
“Ahaaa madam, kibarua change kitaota nyasi kumbuka kwamba mimi nimepewa dhamana ya kukulinda wewe popote utakapo kwenda na kuomba basi twende”
“Nimekuambia kwamba hakuna kuondoka, nimekuandalia chakula sebleni twende ukale”
Rahab akatangulia kutoka ndani ya chumba hicho, Priscar na yeye akafwata kwa nyuma huku akionekana kuwa na maswali mengi sana juu ya bosi wake huyo. Akakuta meza ya chakula ikiwa imeandaliwa vizuri, huku vyakula pamoja na vinywaji vikiwa vimo juu ya meza hiyo.
“Madam umevitolea wapi hivi vyakula?”
“Nilikwenda kuvinunua, kwa ajili yetu. Mimi nimesha kula bado wewe”
Priscar akakaa na kuvuta meza huku akiendelea kuvitazama vyakula hivyo, Rahab akawasha Tv iliyomo ndani ya chumba hicho, kuangalia ni nini kinacho endelea.
‘SHAMBULIZI KITUO KIKUU CHA POLISI CHAUA ASKARI KUMI NA MOJA HUKU MAGAIDI WAWILI NAO WAKIPOTEZA MAISHA’
Habari hiyo ikamfanya Priscar kukisitisha kidogo kijiko kuto kuingia mdomoni mwake na kuitazama taarifa hiyo ambayo imemuacha mdomo wazi.
“Masikini weee tazama askari wa watu walivyo kufaa”
Priscar alizungumza kwa sauti ya huruma, Rahab akawa na kazi ya kutabasamu kwani damu yake tayari imesha anza kufanya kazi mwilini mwa Priscar.
***
   Shamsa na Briton wakafanikiwa kufika chini ya gorofa, ambapo maiti nyingi za askari wanao linda jengo hilo zimesambaa kila mahali, wakaanza kukimbia kwenye moja ya barabara yenye giza ili kuto onekana na askari. Wakafanikiwa kupata usafiri wa bajaji ambao moja kwa moja ukawapeleka hadi maeneo ya bahari beach, kutokana hapakuwa na aliye na pesa mfukoni mwake ya kumlipa dereva huyo wa bajaji, gafla Shamsa akapiga dereva huyo maeneo ya nyuma ya shingo yake na kumfanya apoteze fahamu.
Wakaona viboti vidogo vya watalii, vikiwa vimesimamishwa ufukweni, kwa haraka wakaingia kwenye moja ya kiboti na kukiwasha, wakaondoka na kutokomea kusipo julikana
Magaidi walio ingia katika jengo la usalama wa taifa, wakajikuta wakizidiwa nguvu, na kuwekwa kati, huku silaha walizo kuwa nazo zikiwaishia. Hapakuwa na aliye tamani kuweza kukamatwa na kikiko hicho walicho weza kukifanya ni kujilipua kwa mabomu ambayo waliyavaa miilini mwao na huo ndio ukawa ni mwisho wa maisha yao.
  ***
Msakao mkali ukazidi kufanyika katika maeneo yote na kuingi mipakani mwa Tanzania, kwenye vituo vya mabasi pamoja na bandari, msako ukaendelea kufanyika kuwatafuta Shamsa pamoja na Briton walio toroka katika jengo la usalama wa taifa. Kazi hiyo haikufanywa na askari polisi pekee bali vikosi vyote vya ulinzi vikaingia kazini. Hapakuwa na muda wa kuweza kupumzika, boti nyingi za ulinzi pamoja na na helicopter za kijeshi zikaendelea kufanya doria kwenye maeneo yote ya nchi kavu pamoja na majini.
Amri kutoka kwa raisi, iliwaruhusu vikosi hivyo vya majeshi kuwaua Briton na Shamsa pale watakapo weza kuwakamata kwani hakuhitaji mlolongo wa mauaji wa wanajeshi wake na raisi uzidi kuendelea ndani ya nchi yake, hofi ya kiusalama ikazidi kutanda kwa wananchi wa Tanzania, kila mmoja hakuhitaji kwenda mbali kabisa nyumbani kwake kuhofia usalama wake pamoja na familia yake. Baadhi ya huduma za kijamii, hususani kwa wafanya biashara wadogo wadogo na wakubwa, walijikuta wakiingia katika hofu ya kuto kufungua maduka yao, huku kukiwa na taarifa kwamba Al-Shabab wameingia jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya ujumbe mfupi wa maneno(meseji), zilisambaa baina ya mfanya biashara mmoja hadi mwengine, wakitarifiana kuto kuyafungua maduka yao pale kutokapo pambazuka kwani kufanya hivyo yanaweza kutokea maswala ya Mlimani City.
Hadi kuna pambazuka asubuhi hapakuwa na kauli yoyote kutoka serikalini, jambo lililo pelekea watu wengi kujawa na hofu zaidi. Foleni ambazo zimezoeleka kuonekana kwenye barabara za jiji la Dar es Salaam hazikuwepo kabisa, Magari moja moja ya wananchi wanao jiamini ndio yalkiyoweza kukatiza katika barabara hizo. Mabasi ya mikoani hayakuweza kuingia ndani ya jiji la Dar es Salaam, wala mabasi ya ndani ya jiji kutoka nje ya jiji la Dar es Salaam.
Kiufupi hali ya amani ilipotea kabisa, kwani hata tetesi za chini chini zilidai kwamba mke wa raisi amepotea na inasadikika ametekwa.
“Kama mke wa raisi amete kwa wewe je? Hembu kalisha makalio yako hapo mume wangu na kama ni hiyo kazi bora tu ufukuzwe, ila sinto hitaji kuona ninakupoteza wewe mume wangu sawa”
Dada mmoja mjamzito alisikika akizungumza huku akiwa amesimama katikatai ya mlango akimzuia mume wake kutoka nyumbani baada ya kumaliza kujiandaa kwenda kazini.
“Lakini mke wangu…..”
“Hakuna cha lakini hapo, wewe unahitaji mimba yangu itoke si ndio”
Ikabidi jaama kuwa mpole na kuanza kuvua nguo moja baada ya nyingine na kurudi chumbani huku akiwa analalamika sana.
   ***
“Muheshimiwa bado mke wako hajarudi na kila tukipiga simu yake na mlinzi wake, hazipatikani”
Habari hiyo ikazidi kumchanganya Raisi Praygod aliye jikuta akizunguka zunguka ndani ya ofisi yake kama mtu aliye changanyikiwa. Hapakuwa na amaini kwa kila aliye fanya kazi kwenye ofisi yake,. Kwani kila taarifa inayo letwa ni mbaya kupindukia, vikosi vya uvamizi vinavyo vamia majengo ya serikali, vilizidi kumchanganya Raisi Praygod huku akiwa na hofu ya kuuendea uchanguzi kwani wananchi wengi watapoteza imani na serikali yake iliyopo madarakani.
“Hakikisheni munamtafuta mke wangu popote alipo sawa”
“Sawa muheshimiwa”
“Muheshimiwa kuna simu yako”
Mmoja wa sekretari wake wakamuita, raisi Praygod akaiendea meza yake na kuchukua mkonga wa simu na kuuweka sikioni na kuusikilizia ni nani anaye ipiga simu hiyo.
“Haloooo mr president”
Sauti nzito na yenye mikwaruzo ilisikika upande wa pili wa simu hiyo na kumfanya raisi Praygod kuweza kustuka.
“Ni nani wewe mwana haramu?”
“Hahahahaha president Praygod, umenisahau mara moja hii. Ok sina muda mwingi wa kupoteza ila tangu waziri wako wa ulinzi atokemadarakani na kufariki, inchi yako haina amani. Hujiulizi kwa nini muheshimiwa raisi”
Sauti hiyo ikasikika kwenye vipaza sauti vyote vilivyomo kwenye ofisi ya raisi Praygod, watu wote waliomo ndani ya ofisi hiyo wakaacha kazi walizokuwa wakifanya na kuisikiliza sauti hiyo yenye mikwaruzo ya kutisha.
“Washa televishion yako”
Mmoja wa wafanyakazi wa ofisini akawasha Tv kubwa iliyomo ndani ya chumba hicho cha raisi Praygod, macho yao yote yakatua kwenye bomu kubwa la nyuklia. Lililo tegwa vizuri kwenye vishikizo vyake.
“Hilo ni bomu lenye uwezo wa kutembea kwa spidi 1,000,000 ndani ya dakika moja, hilo ni Russian bomu, ambalo limeandaliwa mahususi kuja kwenye nchi yako na kutua katikati ya jiji la Dar es Salaam”
Raisi Praygod akajikuta jasho likimwagika, wasiwasi mwingi ukamtawala, mapigo ya moyo yakazidi kumuenda mbio mithili ya mtu aliye kimbia kwa umbali mrefu pasipo kupumzika.
Akajikuta akipunguza uzito mwilini mwake, akalivua koti alilo livaa, na kubakiwa na shati.
“Ukihitaji bomu hilo lisije kwenye nchi yako, kuna mambo mawili unahitaji kuyafanya.”
“Moja, hakikisha kwamba unaurudisha uhai wa Eddy Godwin”
“Mbili ndani ya masaa 48, Eddy awe amerudi madarakani la sivyo bomu hili litaisambaratisha ikulu yako”
Simu hiyo ikakata, huku video iliyo kuwa inaonekana kwenye tv hiyo ikapotea na kubakisha mwanga wa bluu wa tv hiyo kubwa, watu wote waliomo ndani ya ofisi hiyo wakabaki wakimtazama raisi Praygod azungumze kitu juu ya hilo.
ITAENDELEA….Usikose kufuatilia hapa hapa mbukuzihuru.com.  Pia unaweza kupata riwaya hiyo yote,SHE IS MY WIFE na SEX DEALER kwa bei nafuu tu, whatssap no. 0753503331.
Advertisements