MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
‘Hawanijui hawa’
Eddy alizungumza huku akishuka kwenye gari bastola yake akiwa ameichomeka kwa nyuma.
“Nyinyi ni wakina nani?”
Eddy aliwauliza huku akijiweka sawa kwa lolote litakao kwenda kujitokeza, ukimya wa barabara hiyo inayo elekea ikulu na majira haya ya usiku iliwafanya Lube na wezake kuweza kuilisikia swali hilo walilo ulizwa. Hapakuwa na aliye jibu zaidi ya wao kuanza kujitawanya na kumzingira Eddy na kumuweka kati tayari kwa kumshambulia.
ENDELEA
Eddy akawatazama kwa huku akiwahesabu jinsi walivyo kaa, taratibu akalivua shati lake na kubaki tumbo wazi, Lube akamuamrisha mwenzake mmoja kufanya shambulizi kwa Eddy anaye onekana kujiamini sana. Kitendo cha jamaa kumfikia Eddy, akakutana na teke zito lilotua kifuani kwake na kumuangusha chini kama mzigo. Ikawabidi wengine kushanga kwani kila mmoja hakuamini kama kiongozi huyo anaweza kufanya tukio la aina hiyo.
Wote watatu walio bakia wakamvamia Eddy kwa kasi, kila mmoja akijaribu kupiga sehemu yake anayo iweza kupiga katika mwili wa Eddy, ila kila walivyo jaribu kupambana, ndivyo jinsi walivyo weza kukutana na mapigo makali yaliyo wachanganya kiasi cha kuwafanya kila mmoja kujikuta akiwa na maumivu upande wake. Lube alipo gundua Eddy amewazidi kila jambo. Kwa bahati nzuri akaona gongo moja pembezoni mwa barabara. Akarudi nalo hadi sehemu wanapo endelea kupambana wezake, huku gongo hilo akiwa amelificha nyuma ya mgongo wake.
“EDDYYYYYYYYY……..”
Lube akamuita Eddy kwa sauti ya juu na kumfanya Eddy ageuke kutazama mtu anaye muita, ila gafla gongo zito likatua, kichwani mwake na kumfanya Eddy kuyumba, kijana mmoja akamsindikiza na teke zito lililo muangusha Eddy chini na kupoteza fahamu.
“Mbebeni haraka haraka”
Lube alizungumza, kabla hata hawajamnyanyua mwanga mkali wa gari ukawamulika, na kuwafanya wasimama kulitizama gari hilo ni la nani majira hayo ya usiku. Gari hiyo ikafunga breki na kusimama, akashuka mtu ambaye wote wanamfahamu.
“Huyu Samson amefwata nini hapa”
Mmoja wao alizungumza kwa sauti ya chini huku wakimtazama Samson akitembea na kuwafwata sehemu walipo.
“Bosi tufanyaje?”
Mmoja wao aliuliza huku kila mmoja akijiweka sawa. Samson akawatazama kisha akawakazia macho, wote wakajikuta wakishikwa na woga mkali kwani macho ya Samson yalibadilika na kutisha sana
***
    Agnes na Jaquline wakashuhudia jinsi Halima na wezake wanavyo pata mateso gerezani. Video hizo zikawamfanya Agnes kumwagikwa na machozi ya uchungu, uzuri wa wezao hao wote umepotea, alama nyingi za makovu zimetawala kwenye miili yao.
“Munaweza kuamua sasa, kufanya kazi na sisi au wezenu waendelee kupata mateso na mwisho wa siku hukumu ya kuuawa itakuwa dhidi yao”
Kabla hawajajibu mlio wa simu ukalia kutoka kwenye mfuko wa mmoja wa walinzi, akaitoa simu hiyo na kuipokea kisha akaiweka sikioni mwa John
“Ndio mkuu”
“Leo ninakuja mako makuu kila kitu ukiweke sawa”
“Sawa mkuu”
Simu ikakatwa John akashusha punzi kidogo, kwa taarifa aliyo weza kuipata kwa mkuu wake Mzee Godwin. Akaagiza ulinzi uzidi kuimarishwa na vijana waweze kujiandaa kumpokea mkubwa wao huyo anaye tokea barani Afrika.
“Tumekubali, ila kwa sharti moja”
Jaquline alizungumza huku akimtazama John machoni huku akiwa amemkazia macho, John akatingisha kichwa chake kumruhusu Jaquline kuendelea kuzungumza.
“Hatuta weza kufanya kazi yoyote na nyinyi hadi pale tutakaopo waokoa wezetu”
“Mmmmmmm, nitarifikiria”
“Waandalieni sehemu inayo stahili wao kuwepo”
John akatoa agizo lake kwa vijana wake, wakawachukua Jaqulne na Agnes na kuwapeleka kwenye moja ya chumba kilicho na huduma za kila kitu wakisubiria juu ya jibu watakalo pewa na John.
Mzee Godwin akaagana na bwana Abdulah Mohamed mkuu wa kikosi cha kigaidi cha Al-Shabab, wakaingia kwenye ndege ya kifahari aina ya Jet inayo ingia abiria watano pamoja na marubani wawili. Tom na Manka tayari walisha ingia kwenye ndege hiyo wakimsubiria baba yao aliye kuwa akipiga stori za hapa na pale na kiongozi huyo waliye aihidiana kupanga baadhi ya mipango takayo kuwa kabambe katika kutawala baadhi ya maeneo kwa kutumia nguvu.
“Mumemechoka ehee”
Mzee Godwin aliwauliza wanae hao huku akijiweka vizuri katika siti aliyo kaa
“Ahaa kidogo tu”
Tom alijibu
“Mmmm mimi nimechoka sana tu baba, hapa natamani tufike huko tunapo kwenda”
“Musijali haita chukua masaa mengi tutakuwa tumefika”
                                                                                           ***
Mihemo mizito pamoja na mingurumo anayo itoa Samson ikawafanya Lube na wezake kuzidi kutetemeka, mmoja wao akachomoa bastola yake na kumfyatuia baadhi ya risasi kwa Samson, ila jambo la kushangaza risasi hizo ziliingia mwilini mwa Samson ila katika sehemu zilipo ingia jeraha lake likapona ndani ya sekunde chache.
Kwa kasi ya ajabu Samson akamkimbilia jamaa aliye mpiga risasi, akamkamata shingo, kwa mkono mmoja akamnyanyua juu, huku akizidi kukoroma na macho yake yakiwa yamebadilika na kuwa kama simba aliye na hasira kali.
“Ondokeni hapaaa”
Samson alizungumza kwa sauti nzito, huku akimuachia aliye mpiga risasi hakuhitaji kumdhuru na kuwafanya Lubne na wezake wote kuondoka katika eneo hilo, wakaingia ndani ya gari lao na kuondoka kwa mwendo wa kasi kila mmoja akiwa haamini alicho weza kukiona kwa binadamu huyo wanaye mtambua kama Samson.
Samson akambeba Eddy begani na kumuingiza kwenye gari lake na kuondoka naye.
“Madam nimempata”
John alizungumza kupitia simu yake huku akiwa amesimamisha gari lake pembezoni mwa barabara huku Eddy akiwa amemlaza siti ya nyuma.
“Safi sasa hakikisha unampeleka kwenye eneo ambalo si rahisi kwa mtu kuweza kutambua”
“Sawa madam”
Samson akakata simu na kuendelea na safari, Samson kitu alicho weza kukumbuka ni moja ya handaki ambalo Rahab alimueleza kwamba yalikuwa ni maficho yao kipindi walipo weza kukutana kwa mara ya kwanza, na handaki hilo lipo nje ya mji. Usiku huo huo akafunga safari hadi nje ya jiji la Dar es Salaam, akifwatisha maelekezo anayo tumiwa kwa njia ya meseji na Rahab aliyopo ndani ya ikulu
“Mke wangu leo unachati sana”
Raisi Praygod alimuuliza Rahab, mara baada ya kuingia ndani ya chumba chao dakika kadhaa zilizo pita, ila mapokezi ya leo yapo tofauti sana na siku nyingine za nyuma, kwani alisha zoea kufanyi mapokezi ya mabusu motomoto.
“Kuna taarifa ninaisoma hapa”
“Taarifa gani ambayo raisi siifahamu?”
“Aihusiani na Tanzania”
“Mmmm saw………..”
Raisi Praygod hakuimalizia sentesi yake simu yake ikaita, akaitoa kwenye mfuko wa koti lake la suti na kukuta Lube ndio anaye mpigia, akamtazama Rahab kwa macho ya kuiba kisha akaipokea.
“Mmmmmm”
“Mkuu tumeshindwa Samson sio binadamu”
Raisi Praygod akashindwa kuzungumza chochote zaidi ya kutoka ndani ya chumba chake cha kulala na kwenda kuzungumzia sebleni, na kumpa nafasi Rahab ya kumpigia simu Samson.
“Sio binadamu kivipi?”
“Yaaani yaani macho yake yamekuwa kama, samba”
“Ahahaa Lube hembu pangilia sentesi zako nikuelewe”
“Yaani Samson ni jinni”
“Jini, mupo wapi?”
“Ndio tunaingia hapa getini”
“Basi njooni ofisini kwangu”
Raisi Praygod akakata simu na kujikuta uchovu wote alio kuwa nao ukimuishia na kuanza kutembea hatua za haraka kuelekea ofisini kwake.
“Samson imekuwaje ukaonyesha uhakisia wako”
“Samahani madam”
“Siku nyingine hakikisha kwamba uhalisia wako unapo uonyesha kwa mtu yoyote, usiye muamini hakikisha kwamba unaitoa roho yake”
“Sawa madam”
“Mumesha fika”
“Ndio tunafika”
“Kesho nitakuja hakikisha kwamba humuachi peke yake”
 Samson akasimamisha gari lake pembezoni mwa handaki alilo elekezwa akashuka na kufungua mfuniko wa chuma ambao pembezoni mwake akakuta jiwe kubwa. Mazingira ya eneo hilo yanaonyesha kuna watu wametoka katika eneo hilo siku chache zilizo pita.
Akaingia ndani ya handaki hilo akiwa peke yake, akalichunguza handaki hilo kwa umakini, alipo hakikisha usalama upo akarudi kwenye gari akambeba Eddy na kumpeleka kwenyemoja ya chumba chenye kitanda, akamlaza vizuri kisha yeye akatoka na kukaa kwenye moja ya kiti kilichopo kwenye seble kubwa ndani ya handaki hilo
Raisi Praygod akajikuta akishusha pumnzi nyingi baada ya kuambiwa mambo yaliyo tokea, kichwani kwake akajikuta akimuwa Eddy na Samson.
‘Rahab’
Raisi Praygod akakumbuka kwamba mtu aliye weza kuurudisha uhadi wa Samson ni Rahab, kwa haraka akanyanyuka na kuwaacha vijana wake ndani ya ofisi hiyo na moja kwa moja akaelekea chumbani kwake na kumkuta Rahab akiwa amelala. Jinsi anavyo zidi kumtazama ndivyo jinsi uchungu na wivu unavyo zidi kumtawala kila akimkimbuka Eddy na kuvuta baadhi ya kumbukumbu jinsi Eddy alivyo mfanya mke kitandani hasira kali ikazidi kumpanda hadi akahisi kifua chake kumpasuka.
Akavua nguo zake zote na kubaki kama alivyo zaliwa, akalifunua shuka alilo jifunika Rahab na kumkuta akiwa kama alivyo zaliwa, kwa papara akajikuta akianza kumpapasa kila eneo la mwili wa Rahab ila kitu kilicho mshangaza siku ya leo, jogoo wake halikuweza kusimama kitu kilicho mfanya Rahab kuyafumbua macho yake na kumtazama mumewe kisha akatabasamu kwa dharau
“Endelea kufanya unacho kifanya”
Maneno ya Rahab yakamfanya raisi Praygod mapigo yake ya moyo kumuenda mbio kiasi cha kujikuta jasho likimwagika mwili mzima na kujikuta akijilaza pembezoni mwa Rahab ikiashiria kwamba ameshindwa jogoo wake ameshindwa kuwika
ITAENDELEA….Usikose kufuatilia hapa hapa mbukuzihuru.com.  Pia unaweza kupata riwaya hiyo yote,SHE IS MY WIFE na SEX DEALER kwa bei nafuu tu, whatssap no. 0753503331.
Advertisements