Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ametangaza ziara yake ya muziki nchini Marekani ambapo atatumbuiza kwenye majiji 12 nchini humo.
Ziara hiyo inayoanza tarehe 22 June hadi 23 July 2018, Diamond atawapagawisha kwa burudani wakazi wa Majiji ya New York, Los Angeles, Minnesota, Houston, Seattle, Kansas City, Washington DC, Boston, Atlanta, Columbus, Philadephia, Dallas.
“Kuelekea kwenye Kuachiwa Rasmi kwa Albam ya #AboyFromTandale Ndugu zangu Mlio Marekani Jiandaeni kwa Ziara ya #AboyFromTandaleUSATour ndani ya State hizo 12 kuanzia tareh 22/06 hadi 23/07 Mwaka 2018!!“amesema Diamond Platnumz.
Ziara hiyo ya ‘A Boy From Tandale’ itakuja baada ya kuachiwa kwa album yake ya ‘A Boy From Tandale’ mwezi Machi 14, 2018.
Advertisements