Image result for agano la kale na jipya image

 

Wapenda katika bwana, Bwana Yesu  asifiwe.

Leo nimeona tujifunze juu ya roho mtakatifu ambapo tutaangalia juu ya kunena kwa lugha

ROHO MTAKATIFU NI NANI AU NINI?  . Roho mtakatifu ni nguvu ya mungu ambayo inakaa ndani yetu (YOHANA 14:16-17,  Matendo 1:8 na matendo 10:38). Kwa maelezo ya biblia kama bwana yesu alivyoeleza katika mafungu hayo.

Katika somo la leo la kunena kwa lugha sehemu ya kwanza  tutajifunza namna ya unenaji unavyo tumika sasa na fundisho la biblia linasemaje?.

MATENDO YA MTUME 2:1-10

mafungu haya yanaonesha kuwa lugha zilizokuwa zikinenwa zilikuwa zikieleweka kabisa kila mmoja au kila taifa lilisikia lugha yake.

1WAKORINTO 14:5

fungu hili linasisitizwa kuwa  itolewe tafsili ili kusudi kanisa lijengwe.

1KOR 14:7

linasema kuwa sauti zipo nyingi lakini zinafahamika itakuaje ikitoka sauti isiyofahamika?

1KOR 14:8-10

mafungu haya yanaonesha  kuwa kunena huko kwa lugha maneno  yenye kufahamika nasikwamba hatamnenaji awehajui anenacho na hatakama atakuwa hajui basi na mwingine afasili.

1KOR 14:11

fungu hili linatuambia ukinena kwa lugha na mtu asiyekuelewa mtakua wote wajinga.

1KOR 14:15-17

Mafungu haya yanaonesha ni jinsi gani kunena huko kwa lugha tusipo kuwa makini kuna vitu tutaona tuko sawa kumbe hatuko sawa.   

1kor 14:22

inatuambia kuwa hizo lugha tuzinenazo ni kwaajili ya wasio amini. Inamaana tukiwa watu wa imani moja hakuna sababu ya kunena kwa lugha.Na mwisho napenda kumalizia fungu la mwisho katika

1KOR 14:23

fungu hili linatuasa tujipime katika imani tulizo nazo  ilikwamba hatawasio tuamini kwa kupitia mfano wetu.

Na hapa natafikia mwisho katika somo la roho mtakifu  katika somo la kwanza la kunena kwa lugha.

 

Asanteni na tukijaaliwa tukutane somo hilihili lakini sehemu ya pili.

MUSA NDAHANI  email: ndahanimusa5@gmail.com

facebook: musa ndahani