Image result for agano la kale na jipya image

 

Agano ni makubaliano baina mtu na mtu, mtu na mahakama au mtu na mungu, Lakini sisi leo tunaangalia Agano juu ya MUNGU na wanadamu(mtu).

AGANO LA KALE

Agano lililowekwa na mungu juu ya wana waisraeli lilikuwa ni juu ya upatanisho kati ya wao na MUNGU,japo makubaliano yalikuwa ni mengi lakini kikubwa ni juu ya kumsafisha binadamu awe safi mbele za MUNGU wake na hapo kale ilitumika damu ya wanyama tunaweza kulisoma hilo

Kut 24:8, inaonyesha jinsi Musa alivyotumia damu ya mnyama kuwapatanisha na mungu.

Mwanzo 4:4 ,inaonesha jinsi habili alivyopeleka sadaka kwa mungu sehemu zilivyonona za wanyama na akambaliki habili kwa sadaka hiyo.

Mwanzo 22:7-13, inaonesha ibrahimu alivyomuacha mwanae na akamuona kondoo akamuchukua kwaajili ya sadaka mbele za mungu.

Mambo hayo yote  na yanayo fanana na hayo yalitumiwa  kwa wanyama yaani kafala ya damu, hilo ni agano la kale. Ambalo liliendelea hadi ikafika pahala wana wa israeli wakaliacha na kufuata mambo yao.

AGANO JIPYA

Baada ya waislaeli kuikataa njia ya awali na kufuata mambo yao ndipo sasa mungu alimutuma nabii yeremia  kuwapasha ujumbe wa  Agano jipya, YEREMIA 31:31-33.

Lakini katika agano hili jipya ndipo tunaona kupitia damu ya YESU  imekuwa ndio njia ya kuu ya utubu wa mwanadamu kwa MUNGU.

 MATHAYO 26:28,  Inaonesha jinsi bwana Yesu alivyojidhihirisha kwa wanadamu kwamba pasipo kumwamini yeye hakuna uzima kwa mtu huyo.

Kipindi hajazaliwa bwana yesu alitokea mtu aliitwa Yohana mbatizaji akibatiza nyikani na kutangaza habari za yesu. Marko 1:4, 1:15.

YOHANA 17:3, Andiko hili linasisitiza juu ya aganojipya na utalatibu wake.

Agano hili ni agano linalomleta mtu kwa mungu wake na kumfanya awe safi kiroho,

watu wamungu ifahamike kuwa agano la kale ni utalatibu wa mwazo uliotumika kumwokoa mwanadamu ambao uliambatanishwa na wanyama lakini agano jipya ni utalatibu unaotumika hadi sasa kumwokoa mwanadamu au kumsafisha mwanadamu kiroho kwa kumwamini yesu kristo aliye hai.

kadilili tutakavyojifunza tutazidi kuangalia zaidi juu ya agano la kale na jipya.

Asante, ninawaomba tuombe tukutane somo lijalo.

 

MUSA NDAHANI  email: ndahanimusa5@gmail.com

facebook: musa ndahani

 

 

 

 

 

 

Advertisements