Ziwa Viktoria (Viktoria Nyanza, Ziwa Nyanza) ni ziwa kubwa la Afrika ya Mashariki lililopo baina ya Tanzania, Kenya na Uganda.

Ni ziwa kubwa kuliko yote barani Afrika, na la pili duniani, baada ya Ziwa Superior ambalo lipo Amerika ya Kaskazini.

Ziwa Viktoria lipo mita 1134 juu ya usawa wa bahari na lina eneo la kilometa za mraba zaidi ya 68,100.

Maji ya ziwa Viktoria yanamiminika kwenye mto Nile na kuelekea bahari ya Mediteranea kwa umbali wa maili 4,000.

Ziwa hili linapata maji yake mengi kutokana na mvua -80% na kutoka vijito vingi vidogo. Mto mkubwa unaoingia Viktoria ni Mto Kagera unaotiririka kutoka magharibi.

Ziwa Viktoria ni miongoni mwa maziwa yenye visiwa vingi vidogovidogo.

Ziwa hili lina kina cha wastani cha mita 40 na mwambao wa urefu wa kilomita 4,828, visiwa vyake vikiwa vimechangia 3.7% ya urefu huu.

Eneo la maji ya ziwa limegawanywa 6% -4,100 km2 , nchini Kenya, 45% 31,000 km2 , nchini Uganda, na 49% 33,700 km2 , nchini Tanzania.

TAARIFA YA UCHUNGUZI

Wanasayansi wanasema kwamba ziwa kubwa zaidi lenye maji tulivu barani Afrika Victoria linalounganisha nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, lipo katika hatari kubwa ya kukauka.

Wanasema kwamba uvuvi haramu na uliopitiliza pamoja na uvamizi wa mazingira kuzunguka maeneo ya ziwa ni sababu kubwa.

Maji machafu pia yanayotiririshwa kuelekea kwenye ziwa yanahatarisha usalama wa viumbe vya majini.

Mwandishi wa BBC anasema jeshi la Uganda limeweka mipango maalum ikiwa ni pamoja na kuharibu nyenzo za uvuvi zinazotajwa kuwa miongoni mwa sababu.

Advertisements