Walimu wawili waliokuwa wakifanya mazoezi kwa vitendo katika shule ya sekondari ya Kikala wilayani Lushoto mkoani Tanga wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kufanya mapenzi na wanafunzi wawili wa kidato cha tatu shuleni hapo.

Akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, January Lugangika amesema waalimu wa wanafunzi hao wamekikuka maadili ya ualimu na kwamba watachukuliwa hatua zaidi huku akiongeza kuwa tabia hizo zinaleta kichefu chefu kwa jamii.

Aidha mwenyekiti huyo amedai kuwa ushahidi wa tukio hilo umethibitishwa na Daktari ambaye aliwafanyia vipimo na kuthibitisha ni kweli kitendo hicho kilifanyika

Kwa upande wa Afisa elimu wa sekondari Wilaya ya Lushoto Kassim Singato amesema endapo kutakuwa na masomo ya ziada ni lazima yafahamike muda yanapoisha ili wazazi waweze kufuatilia mwenendo wa watoto wao.

“Inabidi wazazi muwafatilie watoto wenu kwa kila hatua, mjue wanafanya nini shuleni na kama mzazi humfatilii anaweza kufanya mambo usiyoyajua na badala yake ukashtukia ana mimba ya miezi hata sita,” alisema Singato.

Watuhumiwa wa tukio hilo ni mwalimu Fredriki Shebila na Saddat Mohamed.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, January Lugangika
Afisa elimu wa sekondari Wilaya ya Lushoto Kassim Singato
Advertisements