Ukivuta kumbu kumbu wiki kadhaa nyuma utakumbuka kwamba Diamond Platnumzaliwahi kuropoka kwenye moja kati ya posts za Baby mama wake Zari The Boss Ladyna kuandika kwamba ana kiherehere kuisubiri siku yao kubwa sana maishani mwao, na Zari akaja ku-replay kwa kuandika “Shhhhhhh not now.”

Kitu ambacho kilizua story kibao kitaani na kusemekana kwamba wawili hao wako mbioni kufunga ndao siku za hivi karibuni.

Ukipekuwa kwenye makablasha ya kiswahili utakutana na msemo usemao “Lisemwalo lipo, na kama halipo laja.” Huenda ndio ambacho kinajiri saa hii baina ya wawili hao baada ya jana Diamond Platnumz kusemekana kumvisha baby mama wake huyo Pete ya gharama tayari kabisa kuelekea kwenye ndoa.

Bonyeza Play kwenye video hii hapa chini uweze kuishuhudia pete hiyo ambayo Diamond Platnumz amemvisha Zari.

Drop comment yako hapa chini kwenye uwanja wa comments, unahisi ni ndoa inanukia ama nini?