Kutana-na-Kampuni-inayoweza-kukupa-nafasi-ya-kuishi-milele-hapa-Duniani

Je! upo tayari kulipa milioni 400, ili kuendelea kuishi milele hapa Duniani? kama ni ndio basi kampuni inayofahamika kama Alcor kutoka nchini Marekani ipo tayari kukufanya kuwa mtu usiyeweza kufa (Immortal) na kuweza kuishi hapa Duniani milele.

Unaweza ukadhani ni jambo la masihara lakini ni jambo ambalo linafanyika kweli huko Marekani na idadi ya watu wanaotaka kufanyiwa hivyo ikiongezeka kila mwaka, mpaka kufikia sasa tayari watu 147 wameshagandishwa miilii yao na tayari ipo kwenye majokofu ili kufufuliwa wakati ukifika, huku idadi ya wanachama wanaojisajili kugandishwa miili yao ikiongezeka tangu mwaka 1980, ambapo takwimu za kampuni hiyo zinaonesha walianza na watu 12 na mpaka kufikia sasa tayari zaidi ya watu 1000 wanasubiri kugandishwa miili yao pindi wakifariki.

Cryonics ni nini haswa, Cryonics ni kitendo cha kuugandisha mwili au ubongo wa mtu ambaye amefariki kwa matumaini ya kuweza kuwarudisha kuwa hai tena hapo baadae. Kitendo hicho huwa kinafanyika kwa uharaka sana punde tu mtu aliyesajiliwa kufanyiwa hivyo akifariki basi mwili wake au ubongo utagandishwa, kisha utawekewa kemikali kama glycerol na propandiol ambazo zitasaidia mwili kuwa katika hali yake bila kuoza pamoja na kuuepusha dhidi ya madhara ambayo yatatokana na kuhifadhiwa kwenye jokofu lenye joto la chini kwa muda mrefu sana.

Inafanyikaje, pindi daktari akithibitisha kifo cha mgonjwa basi timu ya wataalamu kutoka Alcor wataandaa jokofu lenye barafu kisha mwili wa muhusika utapatiwa aina 16 za madawa ikiwamo glycerol na propandiol, kisha kuugandisha mwili mpaka joto lake litakapo poa kabisa.

“Jambo gumu sana ni kuwahi kumfikia muhusika na kuanza kumgandisha haraka iwezekanavyo, lasivyo jambo zima litashindikana kama tukichelewa.” alisema mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Max More, hivyo ili kuepusha matatizo kama hayo kampuni hiyo imeweka timu ya wataalam Uingereza, Canada, pamoja na Ujerumani ila wanachama waliokuwa nchi zingine wanatakiwa kulipia dola 10,000 (zaidi ya milioni 22) kisha watauliwa na kuhifadhiwa kwa urahisi zaidi ndani ya dakika 35 tu, tofauti na wale ambao mpaka wafariki ndipo waanze kushughulikiwa.

mkurugenzi-mtendaji-wa-kampuni-hiyo-Max-More
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Alcor, Max More

Mwanachama ataweza kuchagua kati ya kuhifadhiwa mwili mzima au kichwa pekee ambapo bei huwa zinatofautiana. Kuhifadhiwa kichwa peke yake ni dola 80,000 (zaidi ya milioni 170) ambapo daktari maalumu ataondoa kichwa cha muhusika kisha kitahifadhiwa kwa ajili ya kuwekewa kwenye mwili mwingine hapo baadae, na ndiyo njia ya bei rahisi zaidi na nyingine ndo ya kuhifadhiwa mwili mzima ambapo mwanachama atatakiwa kulipia dola 200,000 (zaidi ya milioni 400).

Hivi karibuni mwanamke mmoja wa kutoka Uchina amegandishwa mwili wake kwa mara ya kwanza kutoka nchini humo. Mwanamke huyo aliyefariki akiwa na umri wa miaka 49 kutokana na kansa ya mapafu, mume wake Gui Junmin alijitolea kugandishwa kwa mwili wa mke wake huyo.

Si huyo tu mwingine ni huyu Elaine Walker mwenye umri wa miaka 47 kutoka nchini Marekani amejitolea kugandishwa ubongo wake pindi akifariki.

elaine-walker-amejitolea-kugandishwa-ubongo-wake-pindi-akifariki
Elaine Walker ajitolea kugandishwa ubongo wake pindi akifa / Picha na Facebook
Advertisements