Kampuni-Ya-Magari,-Lamborghini,-Watengeneza-Simu-Kwa-Ajili-Ya-Wapenda-Misifa

Haya sasa wale wanaopenda sifa, hii yaweza ikawa ni habari njema kwao, kama unarafiki yako ambaye hana uwezo wa kununua gari la Lamborghini, ila anapenda kujinadi kwa kuvaa nguo au vitu vyenye thamani kubwa kwenye mitandao au hata kwenye maisha halisi, basi kampuni ya magari Lamborghini wameliona hilo hivyo wameamua kuja na simu maalumu kwa ajili ya watu hao wanaopenda vitu vyenye thamani kubwa kama gari lakini uwezo hawana.

Simu-hiyo-inayoitwa-Alpha-One-inauzwa-kwa-dola-2,450
Muonekano wa simu ya Alpha-One, nyuma, mbele pamoja na kasha ya ngozi

Simu hiyo inayoitwa Alpha-One inauzwa kwa dola 2,450 (zaidi ya milioni 5) inauwezo sawa na zingine ambazo tumezoea kuziona sokoni, haina tofauti sana licha ya kuwa bei yake ni ghali sana. Ikiwa na kasha la ngozi lililotengenezwa kwa mikono kutoka Italia, nembo ya ng’ombe kama aliyekuwa kwenye gari za Lamborghini, yenye kumaanisha “Uimara, uhodari, udhabiti, na ugumu,” pamoja uwezo wake wa ndani kama ifuatavyo:

Skrini yenye ukubwa wa inchi 5.5

Kichakato cha Qualcomm Snapdragon 820

Programu endeshi ya Android Nougat

Ramu yenye GB 4 ikiwa na ukubwa wa GB 64 pamoja na uwezo wa kuongeza hadi GB 128

Kamera yenye mega pikseli 20 nyuma na 8 kwa kamera ya mbele

Uwezo wa betri ni 3,250mAh

Unaweza tumia laini mbili pia na kitambazo cha alama za vidole

Kwa bei hiyo hapana kwani uwezo wake ni wakawaida sana, kuna baadhi ya simu zipo sokoni ambazo zinaweza zikawa na uwezo mkubwa au zikalingana na simu hiyo tena kwa bei ndogo sana zaidi ya hiyo milioni 5, labda kama mnunuzi atataka kununua hiyo nembo ya Lamborghini iliyokuwa nyuma ya simu hiyo pamoja na picha pweke za magari ya Lamborghini ambazo zinapatikana ndani ya simu hiyo tu ili awadolishie wenzake huko mitandaoni.

Advertisements